(Mama wa marehemu Steven Kanumba, Bi. Flora Mutegoa.)
Habari na Gazeti la Mwananchi:
Wiki mbili baada ya kifo cha aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba, wazazi wake; Charles Musekwa Kanumba na Mama yake, Flora Mutegoa ambao hawaishi pamoja, wametofautiana kuhusu suala la mali na mirathi.
Habari na Gazeti la Mwananchi:
Wiki mbili baada ya kifo cha aliyekuwa msanii nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba, wazazi wake; Charles Musekwa Kanumba na Mama yake, Flora Mutegoa ambao hawaishi pamoja, wametofautiana kuhusu suala la mali na mirathi.
Juzi, Mzee Kanumba aliibuka na kudai kuwa
kuna kundi la watu linalomdanganya mama huyo wa marehemu kwamba linajua
zilipo mali za Steven jambo ambalo alisema ni uongo na kumtaka awe na
subira na asidanganyike.
Hata hivyo, kauli hiyo imepingwa na
Mutegoa ambaye amehoji sababu za mumewe huyo..
kuzungumzia mali za mwanaye wakati huu. Alidai kuwa Mzee Kanumba hajawahi kuwa na mawasiliano na marehemu tangu mwaka 1999 alipoondoka kwao, Shinyanga.
kuzungumzia mali za mwanaye wakati huu. Alidai kuwa Mzee Kanumba hajawahi kuwa na mawasiliano na marehemu tangu mwaka 1999 alipoondoka kwao, Shinyanga.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na
gazeti hili juzi, Mzee Kanumba alimsihi mkewe kutodanganyika kwa kuwa
yeye akiwa baba mzazi wa Kanumba anajua mali zote za mtoto wake na ndiye
pekee anayeweza kumtendea haki katika kuzigawa.
“Mali za marehemu mwanangu nazifahamu
zote, kwa hiyo hakuna shaka tutazigawa kwa sababu hakuna baba mwingine
na haki yangu ipo palepale hakuna atakayeinyang’anya,” alisema na
kuongeza:
“Nisingependa tuwape watu faida ya kuanza
kuvutana mahakamani, tunatakiwa suala hili tulimalize sisi wenyewe kama
tulivyompata mtoto wetu. Ninasisitiza mali zote zisifanyiwe vurugu
ziachwe kama zilivyo.”
Katika kuthibitisha kwamba anazijua mali
hizo, mzee huyo alisema Steven ameacha magari matatu, Sh40 milioni,
viwanja viwili na akaunti mbili za benki na Kampuni ya Filamu.
Akerwa na tambiko
Mzee Kanumba alisema anasikitishwa na
tambiko la Kihaya lililofanyika katika kaburi la mtoto wake, jambo
ambalo alisema halikutakiwa kwa kuwa marehemu alikuwa Mkristo na
alizikwa kwa imani hiyo.
“Mimi ni Mkristo, mtu aliyezikwa Kikristo
huwezi tena kuanza kumfanyia mambo ya kipagani na kuanza kumtambikia,
hiyo kwetu hairuhusiwi,” alisema Mzee Kanumba na kuongeza:
“Hata hivyo, marehemu alikuwa Msukuma, si
Mhaya, itakuwaje wamtambikie Kihaya na kumwaga pombe aina ya rubisi huku
marehemu alikuwa hatumii pombe na mimi pia situmii pombe?”
Kuhusu tambiko, Flora alisema hakuna kitu
kama hicho kilichofanyika kwenye kaburi la mwanaye isipokuwa Wahaya wana
mila zao kwa mwenzao aliyepatwa na msiba.
“Kilichofanyika siyo tambiko bali, ni mila
zetu za Kihaya. Unapofiwa wenzako wanakuletea vitu kama kreti ya soda,
bia na mkungu wa ndizi. Lile siyo tambiko ni mila tu, mimi pia ni
Mkristo, siwezi kushiriki matambiko,” alisema.
Alisema suala hilo la kugawa mali au
msimamizi wa mirathi walitakiwa kukutana pande mbili, yaani yeye na
mkewe baada ya kupita siku 20 tangu alipozikwa waangalie namna ya kugawa
huku akisisitiza kuwa hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kuingilia
masuala hayo.
Mama amkana
Kwa upande wake, Mutegoa ambaye sasa bado
yupo nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican, Dar es Salaam alisisitiza
kwamba marehemu hajawahi kuwasiliana na baba yake huyo tangu mwaka 1999.
Alieleza kushangazwa na taarifa hizo
kutoka kwa mzazi mwenzake huyo na kusisitiza kuwa ni mapema mno kuanza
kujadili mali za mtoto.
“Nasikitika kulisema hili kwani bado niko
kwenye msiba wa mwanangu. Hata hivyo, sidhani kama mwenzangu anajua
chochote kuhusu Steven, achilia mbali mali zake, hawajawahi kuwa na
ukaribu mpaka kuweza kujua mali zake,” alisema na kuongeza:
“Hata hivyo, mbona anazungumzia mali tu,
hivi anafahamu kama Steven alikuwa na madeni? Ninamsihi aachane na hizo
habari kwa wakati huu kwani hazina uzito wowote ukilinganisha na thamani
ya mtoto niliyempoteza,” alisema.
No comments:
Post a Comment