Timu ya inayoundwa na Watanzania wanaoishi DMV na mabingwa wa Vijimambo 2
Years Soccer Tournament, Jumapili April 29, 2012 wataanza Mashindano
ya 2012 Diaspora World Cup kwa mechi na Ghana katika kiwanja cha Heurich
Stadium ulipo Hyattsville (uwanja wa Simba na Yanga).mechi hii
itachezwa saa 3 asubuhi. (9:pm)
Jumla ya timu zinazoshiriki mashindano hayo ni 20 Tanzania ipo kundi B
ikiwemo Ghana, Malawi, Armenia, Uingereza, Ethiopia, Nigeria, Morocco,
Ureno na Hispania.
Kundi A lina timu za African Union, Cameroon, Ivory Coast, Ufaransa, Gabon, Kenya, Niger, Scottland, Zambia na Senegal.
Kila Group litacheza mechi 35, Vijimambo ikiongea na Jabir Jongo amesema
anaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kuipa nguvu timu yao. Wakati
huo huo Kocha wa Tanzania DMV Dedi Luba amesema vijana wapo fiti na
anaomba sapoti ya Watanzania kwenye mechi hizi..
Sherehe za ufunguzi ni leo Jumamosi April 28th ndani ya Discovery
Stadium uliopo Germantown SoccerPlex. Stadium. kuanzia saa 6 mchana
(12pm)
| |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
No comments:
Post a Comment