Pages

NUHA Blogging Prize 2013


NUHA Foundation
Our friends over at the NUHA Foundation have announced their third annual blogging prize competition. The competition encourages people of all ages to think and write about topics in global education.
Getting involved is simple: Choose your topic, write a 500-1500 word argument about it (don’t worry too much about language) and send it in.
There are at least 3 cash prizes up for grabs, based on 3 age categories. The following are the topics for each age category:
Young Writers Prize (born between 1999 and 2003, winner gets £50):
  1. Why do grown-ups read fairy tales?
  2. In the future, will children still use pencils?
  3. “Imagination is more important than knowledge. Knowledge is limited. Imagination encircles the world.” by Albert Einstein. Do you agree? Why?
Youth Prize (born between 1995 and 1998, winner gets £100):
  1. Myths, legends and fantasies: why do we read them, why do we watch them?
  2. “To be or not to be…” Is that what school is about?
  3. “Education is not the filling of a pail, but the lighting of a fire.” Attributed to WB Yeats. Do you agree? Why?
Adult Prize (born before 1995, winner gets £150):
  1. If there was one thing you could change to improve education in your country, what would it be and why?
  2. In an era of tight public finances, should students be entitled to subsidised higher education no matter what they choose to study?
  3. “Those who can’t laugh at themselves leave the job to others.” (Anonymous quote.) Discuss.
Depending on the number of submissions, second-place cash prizes will also be awarded.
All entries are due to editor(at)nuhafoundation.org by 6th October 2013, and must be accompanied by a submission form (download Word version here).
Winners will be announced on 9th December 2013. Good luck!

Mshindi wa The Vodacom Mic King 2013 ni Martin Fundi

MARTIN FUNDI
...Akiliwasha gari lake.Vodacom Tanzania, Matina NkurluMeneja wa Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akimkabidhi ufunguo wa gari mshindi wa The Vodacom Mic King 2013, Martin Fundi. Katikati ni Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho.  The Vodacom Mic King 2013, Martin FundiMartin Fundi akifungia mlango wa gari lake.
 The Vodacom Mic King 2013, Martin FundiMashabiki wakiwa wamelizunguka gari la Martin kutoka Kimara usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea katika shindano la The Vodacom Mic King 2013 na kujinyakulia gari jipya aina ya Toyota Funcargo (new model). Shindano hilo lililokuwa likidhaminiwa na Kampuni ya simu ya Vodacom lilidumu kwa takribani miezi sita na usiku wa kuamkia leo ndiyo limefika tamati.

Mwanaume Achomwa na Maji ya Moto na Mkewe Mombasa (Video)

Mwanamume mmoja mjini mombasa amefariki kwa kile kinachodaiwa kusababishwa na mgogoro wa kinyumbani kati yake na mkewe. Inadaiwa marehemu alimwagiwa maji moto na mkewe siku chache zilizopita hali ambayo imepelekea kifo chake. Ilibidi polisi kuingilia kati kumnusuru mama huyo dhidi ya hasira za umati uliotaka kumshambulia

TAIFA STARS WAKIWA NDANI YA SUTI ZILIZOTENGENEZWA NA NGOWI

Taifa Stars
Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakiwa ndani ya suti walizokabidhiwa na wadhamini wakuu TBL huku zikiwa zimetengenezwa na mbunifu wa mavazi Tanzania Sheria Ngowi.

Katuni ya Leo

Katuni

Waliofeli Kidato cha Nne Waula, Ufaulu Sasa Waongezeka

Ratiba ya Bunge
Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya...

WATU 293 WAMEKAMATWA KWA KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA UFARANSA.

Manuel Valls
Polisi jijini Paris, Ufaransa wamekabiliana na maelfu ya waandamanaji wanaopinga sheria iliyoidhinishwa na bunge kuruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.
Maandamano hayo ambayo awali yalianza kwa amani yaligeuka kuwa vurugu pale ambapo polisi walilazimika kuingilia kati kuwatawanya waandamanaji hao ambao walianza kuharibu mali.
Waandishi kadhaa wa habari walishambuliwa na waandamanaji hao, hali iliyowalazimu polisi kuingilia kati kuwanusuru kutokana na kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kuwatuhumu kuunga mkono ndoa hizo.
Polisi jijini Paris wanasema kuwa inawashikilia watu zaidi ya 293 ambapo watu sita ndio wanaoelezwa kujeruhiwa kutokana na maandamano hayo wakiwemo polisi wanne waliokuwa wakishiriki kwenye operesheni hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Manuel Valls amelaani maandamano hayo yaligeuka kuwa vurugu, na kuyashutumu makundi yenye msimamo mkali kuhusu ndoa za jinsia moja nchini humo.
Maandamano hayo yamefanyika wakati huu ambapo jopo la majaji wa tamasha la filamu la Cannes wakitoa tuzo ya filamu bora ya mwaka kwa mtunzi mwenye asili ya Tunisia na Ufaransa aliyetengeneza filamu inayoitwa :Blues is the Warmest Colour" ambayo inaelezea maisha ya wanawake waliooana.
Waandaji wa maandamano hayo wanasema kuwa zaidi ya watu milioni moja walijitokeza kwenye maandamano hayo kuoinga sheria hiyo inayoruhusu ndoa za watu wa jinsia moja.(RFI)

Serikali Kupitia Wizara ya Elimu Imependekeza Kuhuisha Mfumo wa Elimu

Serikali kupitia wizara ya elimu imependekeza kuhuisha mfumo wa elimu na mafunzo kwa kujumuisha elimu ya msingi na elimu ya Sekondari ngazi ya kawaida kuwa elimu msingi ambayo itatolewa kwa miaka kumi ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

HAWA HAPA WASHINDI WA TUZO ZA HIP HOP 2013

DJ ChokaDJ Choka (kushoto) akimpatia tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop Mwanamuziki Kala Jeremiah.
Suma MnazaretiSuma Mnazareti (kushoto) akimpatia tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi wa Hip Hop, Young Killer.
All BauchaProdyuza All Baucha akimkabidhi Kiboya tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Hip Hop (Legendary) kwa niaba ya Joseph Haule 'Profesa Jay' (GPL)

Lema Amvaa Lowassa kwa Helikopta Monduli

Helikopta Monduli
Monduli. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana aliongoza kampeni za Chadema za udiwani katika Kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli kwa staili ya aina yake, akitumia helikopta huku ikidondosha vipeperushi vya mgombea wa chama hicho, Japhet Sironga.
Akizungumza katika kampeni hizo, Lema alisema: “Chama chetu kina uhakika wa ushindi kwani Sironga ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Ilboru, ana uwezo mkubwa kwa kuwa ni msomi.
Lowassa ndiye aliyepewa mikoba na CCM ya kumnadi mgombea wa chama hicho na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wabunge wa chama hicho Mei 19, mwaka huu Mjini Dodoma alisema kiongozi huyo anatosha kukipa ushindi katika kata hiyo.
Lema alisema: “Makuyuni, hamna maji, hamna huduma za afya, hakuna barabara za vijiji, wafugaji ardhi yenu inaporwa sasa ukombozi wenu umefika kama mkimchagua msomi Sironga.”
Alimkabidhi mgombea huyo taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kumtaka kazi yake ya kwanza iwe kuibua ufisadi na kumfikishia bungeni ili kuiokoa Halmashauri ya Monduli.
Akizungumza katika kampeni hizo, Sironga alisema ameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho, ili kuokoa jamii ya Makuyuni na Monduli kutokana na shida zinazowakabili.

ADC Kigamboni
Chama cha ADC kimezindua kampeni ya nyumba kwa nyumba ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Mianzini, Kigamboni, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Kigamboni, Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Temeke, Salum Sudi alisema kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo kero ya maji, barabara, elimu ya msingi na soko, hivyo wakipewa ridhaa hiyo kero hizo zitakwisha...
Nyongeza na Pamela Chilongola.
Mwananchi