Pages

Documentari ya #Wilfred Moshi na Mlima Everest {Sehemu ya 1 na 2}

Wilfred Moshi na Mlima Everest ni Documentari inayozungumzia safari ya kusisimua na kutisha ya Kijana shujaa wa Kitanzania anayefanya kazi ya upagazi kwa kuwahudumia watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro nchini. Wilfred alieweka maisha yake rehani kwa ajili kuweka rekodi mpya ya kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest ambao ni mlima mrefu kuliko yote duniani na kuiletea Tanzania sifa kubwa Kimataifa.
Sehemu ya pili ya "Wilfred Moshi na Mlima Everest" inaendelea kueleza kisa cha kusisimua na kutisha cha kijana aliyekuwa Mwafrika wa tatu na Mtanzania wa kwanza kupanda mlima mrefu kuliko yote duniani.
Je ilikuwaje? Nini hasa maana ya safari hii iliyotupa sifa Watanzania duniani? Je ushujaa wake Wilfred Moshi unahusu nini hasa?
Urban Pulse Creative Media, Freddy Macha wakishirikiana na Ubalozi wetu Uingereza wanakuletea habari hii ya kusisimua kwa majuma matano mfufulizo ili tuone na kujifunza kutokana safari yake ya hatari.

No comments: