Pages

MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYA BIASHARA WA MWANJELWA JIJINI MBEYA YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO.

Mbeya
Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa
Mbeya
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo
Mbeya
Hakika kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa ...
mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Mbeya
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo

Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake

Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto

Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box

Hakika jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia

Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele

Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo

Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto


Asubuhi hii moto ndiyo unaishia

Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia

Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo




Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo yanayozunguka maghala yalioteketea kwa mtoto kwa ushirikiano wao kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili wamekamatwa kwa kutupiaaskari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa zinaokolewa


Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani.

PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

No comments: