Pages

MSAADA KWA HUYU KIJANA

Zuberi Mgeni ZuberiKufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.
Zuberi Mgeni Zuberi alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.

Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.
Shughuli wanazo fanya ni Uvuvi na Ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwahiyo walikuwa wa kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika Mwaka 2011 Juni.

Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo.
Zuberi Mgeni Zuberi Chakusikitisha nikuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa Tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6000 za Kimarikani sawa na Shs.9,600,000/= za Tanzania.

Zikipatikana anaweza kusafirishwa na Msaidizi wake mmoja. Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia Nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492 Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui na Mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.

Msaada wa ki Fedha unaweza kutumwa kwenye Akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa Fedha za Kigeni Bank ya Exim Tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.
Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.
SHUKRAN

MELI KUBWA YA MIZIGO KULIKO ZOTE DUNIANI!!

MELI kubwa ya Mizigo Kubwa kuliko zote duniani. Inaitwa Maersk triple E.
Ina UREFU wa wastani wa zaidi ya Viwanja VINNE vya mpira (Wastani wa Mita 400). UPANA ni Mita 59. Urefu wa Kwenda Juu (KIMO) cha Mita 79.
Inaweza kubeba zaidi ya magari ELF30.
Meli hiyo iliyotengenezwa na "Mkorea" ni mali ya kampuni ya Kidenmark ya MAERSK.
Itatumika kwa kusafirisha mizigo kati ya bara la ASIA na ULAYA.
MAERSK
CNN

MTOTO WA MIAKA 14 ALIEZAA MAPACHA WATATU BABA PIA NI MTOTO ANA MIAKA 16..

Kakamega
Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye umri wa miaka 14 Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika kijiji cha Harambee katika wilaya ya Kakamega amejifungua watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana wawili kati yao
wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine akiwa na uzito wa Kilogram 1.3.
Nesi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Bugoma Bi,Mary Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini hapo. Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba Mzazi wa watoto hao watatu waliozaliwa bado ni mtoto mdogo kama alivyo Mama yao kwani Baba yao ana Umri wa Miaka 16 ambae pia bado anasoma, Zaidi aliishukuru sana Serikali kwa kuweza kuondoa garama kwa wajawazito wakiwa wanajifungua na ivyo kuweza kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo Garama zozote zile.

TIMU YA CRICKET YA WAMASAI AMBAYO IPO ZIARANI LONDON UK

CRICKET
 CRICKET
CRICKET
CRICKET
 CRICKET
Jestina-George

Dayna - Naumia (Audio)

Dayna

Shuhudi Mwanamke Alivyokamatwa na Dawa za Kulevya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Leo Mchana

ANTHONIA OJOJitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.
Anthonia Ojo (25) Raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya baada ya kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways. Msichana huyo aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye atafikisha mahakamani.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi.

ANTHONIA OJO AKIWASILI KITUO CHA POLISI CHA JNIA BAADA KUKAMATWA.
ANTHONIA OJO
ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA
ANTHONIA OJO
PASPORT YAKE

HILO NDO BEGI MADAWA HAYO YALIKUWEMO

Nigeria
AKIZITOA KWENYE MIKEBE YA POWDER NA SHAMPOO

SEHEMU YA KETE 99 ALIZOKAMATWA NAZO.
Nigeria
HUYO NDO ANTHONIA OJO AKIWA KITUO CHA POLISI
Nigeria
MADAWA HAYO YAKIRUDISHWA KWENYE VYOMBO BAADA YA KUONESHWA KWA WANAHABARI.
Anthonia Ojo
RECORD ZA ANTHONIA ALIWAHI KUJA TENA MWAKA 2011
Na Robert Okanda

Mr Blue - Pesa (Audio)

Mr Blue - Pesa

Weird Therapies

Join Violet Otindo tonight at 9pm as she looks the lengths people go for remedy and cure on Weird therapies!

Quadruple Take Masterclass

DJ Khaled - I Wanna Be With You Ft. Nicki Minaj, Rick Ross, Future (Audio)