Pages

Urgent Solution Needed for F1 'crisis'. F1 British GP

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/68466000/png/_68466321_tyreblowoutstill.png
 Watching the unfolding dramas of the British Grand Prix, with tyres exploding at high speed on a regular basis, the over-riding emotions were anxiety and alarm - that the drivers' lives were being put at unacceptable risk.
As the dust begins to settle, those feelings are beginning to shift to disbelief at how Formula 1 has managed to get itself into such an unacceptable situation. Some would - and doubtless will - call it a crisis. To many minds, that would not be an exaggeration.
Perhaps the biggest concern is the fact that it should never have happened. It is not, after all, as if it is completely unexpected. As Lewis Hamilton pointed out after the race, tyres have been failing all season.

"We've had this trouble for a long time," said Hamilton, who suffered the first of six on-track tyre failures, all of them at more than 100mph, some of them at nearly twice that.
Sergio Perez's McLaren "It already happened in Malaysia (the second race). And then it happened in Bahrain (the fourth race) and then we did a test to prevent it and they didn't prevent it." He could have added that failures happened in Spain as well.

All of the failures at Silverstone were worrying, but the one that demonstrated most clearly the risks involved was the one in which the left rear tyre on Sergio Perez's McLaren exploded on Hangar Straight - just as Ferrari's Fernando Alonso was shaping up to pass him. 
  The Spaniard had to take rapid avoiding action. And the concern in these situations is not just that a car can hit another - and at more than 160mph that would have been quite an accident - but that the debris can hit the driver.
That debris, as Jenson Button put it, is "rubber that has metal in it". Which at those speeds could kill someone.
Alonso is as brave as they come, but even he admitted to being "so scared and so lucky because I missed the contact by one centimetre".
"Make no mistake about it," Red Bull team boss Christian Horner said. "Fernando Alonso is a very lucky boy today to be going home."
Are there reasons to believe a solution could be delayed, that F1 could muddle on until a long-term solution is found?
The next two races, at Germany's Nurburgring and the Hungaroring near Budapest, are at circuits nowhere near as demanding on tyres as is Silverstone.
Read More..  http://www.bbc.co.uk/sport/0/formula1

Baada ya Obama, George Bush, Mkewe nao Kutua Tanzania Kesho

Obama, George Bush, RAIS mstaafu wa Marekani, George W. Bush na mkewe, Laura wanatarajiwa kesho kuwa nchini kuhutubia kongamano linalojadili wajibu wa wake wa marais katika kuinua wanawake duniani.

Kuwasili kwa Bush, ni mwendelezo wa wiki hii Jiji la Dar es Salaam kuwa katika pilikapilika za kupokea ugeni wa watu maarufu. Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya George Bush na litafanyika kesho na keshokutwa.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo kwa vyombo vya habari , inasema kongamano hilo litahudhuriwa na wake mbalimbali wa marais akiwemo mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama.

Pia Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie Blair atahudhuria. Wake wa marais wa Afrika watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete, Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba (Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone), Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba wa Zambia.

Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha Afrika lakini pia wajibu wa wake wa marais katika kuhamasisha wanawake katika maeneo ya elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.

Ujio wa rais huyo mstaafu wa Marekani utakuja ikiwa ni saa kadhaa tangu mrithi wake, Barack Obama kutua Tanzania kwa ziara ya siku mbili ambapo anatarajiwa kuondoka kesho baada ya kumaliza shughuli mbalimbali alizopangiwa.

VIDEO ya MKUTANO KATI YA OBAMA NA WAANDISHI WA HABARI IKULU..!!

Video streaming by Ustream

Video ya Rais Obama Akiwasili Uwanja wa Ndege wa Mwl JK Nyerere - Dar es Salaam

Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere July 1.

MAMA OBAMA NA MAMA KIKWETE WATEMBELEA WAMA FOUNDATION JIONI HII

Mchelle Obama

Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo...
Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.
Mchelle Obama
Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii. Salma Kikwete
Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi. Salma Kikwete
 Salma Kikwete
Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama Salma KikweteAnna Mkapa
Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii EPTFMakachero wa Marekani wakiwa kazini  EPTF
Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wake wa Viongozi wakati alipowasili katika ofisi za WAMA tayari kwa kumpokea mgeni wake Mama Michelle Obama.

RAIS BARACK OBAMA AMEWASILI NCHINI MCHANA HUU


Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba na watoto wao,wakiwasili mchana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku mbili hapa nchini.
Michelle Obama
Ndege ya Rais wa Marekani ikiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere,mchana huu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Marekani,Barack Obama aliewasili nchini Mchana huu kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili.

Rais Barack Obama akikwagua Gwaride maalum alilioandaliwa akiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenelari Davies Mwamunyange.

Rais Barack Obama na Mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wakiangalia ngoma za asili zilizokuwa zikitumuiza uwanjani hapo.kushoto ni Mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama.

Rais Barack Obama akiagana na Mama Salma Kikwete

Msafara wa Viongozi ukiondoka Uwanja wa Ndege.
Picha zaidi zitawajia baadae kidogo,kwa sasa tuanze na hizi kwa hisani ya TBC.

Mkasi TV Imerudi Tena Hewani, Cheki Promo with Kajala

Zikiwa Zimebakia Siku 5. Masanja, Shilole Wakotayari Kuwasha Moto Siku ya Vijimambo.

Vijimambo
Wasanii Masanja mkandamizaji na Shilole katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi wa sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa Kiswahili, Bwn. Baraka Daudi alipokwenda kuwapokea walipotinga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Vijimambo
Asha Riz mjumbe aliyewawakilisha Tano Ladies kwenye mapokezi hayo akipata picha ya pamoja na wasanii Masanja Mkandamizaji na Shilole mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Shilole
Shilole katika ukodak moment alipokua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Sterling, Virginia.
Masanja Mkandamizaji kwenye Ukondak Moment uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Washington, DC
Msanja akionyesha uwanja wa Julius Nyerere wa Marekani “UNABISHA”

Taswira Maalum Kutoka IKULU: Kuna Meremeta Karibu Obama, Tazama Picha zaidi

Maandalizi Ya Mapokezi Ya Rais Wa Marekani Barack Obama Nchini Tanzania Yakamilika Kwa Kiwango Cha Juu Kabisa,Ona Taswira Za IKULU na Rais Jakaya Kikwete Akikagua Ukamilishwaji Wa Maandalizi Mbalimbali Asubuhi Hii IKULU
IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Kibao cha Barabara wa Barack Obama.
 Barack Obama Nchini Tanzania
Jengo la Ikulu.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akisoma ratiba.
 Barack Obama Nchini Tanzania

 Barack Obama Nchini Tanzania


 Barack Obama Nchini Tanzania
 Barack Obama Nchini Tanzania
Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.Picha na IKULU

HATIMA YA ROONEY MAN UNITED ITAJULIKANA KESHO BAADA YA KIKAO CHAKE NA MOYES

Wayne Rooney KOCHA David Moyes anajiandaa kukutana na Wayne Rooney na wawakilishi wake kwa mazungumzo kesho, hilo likiwa jukumu lake la kwanza kubwa tangu aanze kazi Manchester United.

Mkataba wa miaka sita wa Mscotland huyo umeanza rasmi leo na atakwenda makao makuu ya klabu, Carrington kutatua sakata la muda mrefu la Rooney kutaka kuondoka.

Moyes anataka Rooney abaki, lakini anafahamu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 25.6 mwaka 2004 anataka kuondoka.
Tingisha: Wayne Rooney alikuwa kwenye tamasha la muziki Glastonbury mwishoni mwa wiki
Wayne Rooney
Chini ya utawala mpya: Moyes anashikilia mustakabali wa Rooney Old Trafford
Inafahamika mwanasoka huyo wa kimataifa wa England amejenga fikra zake kwamba kubadilisha klabu ni njia nzuri kufufua makali yake kuelekea Fainali za Kombe la Dunia majira yajayo ya joto.

Zaidi itategemea na mazungumzo yake na Moyes ambaye anafanya jitihada za kumbakiza.
Arsenal na Chelsea zote zinamfuatilia na zina ya kumsajili Rooney na ikiwa United itakubali kumuuza watalazimika kumuacha ajiunge na moja ya wapinzani wao katika Ligi Kuu England.