Annastazia Fredy,Mwanza
KAMPUNI ya kuuza Pikipiki kutoka china (FEKON) imetoa mkopo wa Pikipiki 240 zenye thamani ya shilingi 460.8million kwa vijana wanaofanya biashara ya Bodaboda Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Monarch Hotel Katibu wa jumuia ya vijana Mkoani hapa Abubakari Rubelwa alisema kuwa Kampuni hiyo imekuwa ya kwanza kukubali kutoa mkopo wa Pikipiki hizo ndani ya mwaka mmoja ili kuwawezesha vijana kumudu maisha yao.
“Tunaishukuru Kampuni ya Fekoni kwa sababu ni Kampuni iliyokubali kutukopesha Pikipiki ndani ya mwaka mmoja ambapo kila Pikipiki inagarimu shilingi 1.9million.”alisema Rubelwa.
Aidha Katibu huyo alisema kuwa awali Kampuni hiyo iliwai kutoa Pikipiki 15 zenye thamani ya shilingi 23million vijana wakalipa bila shinda ndiyo maana wameamua kuongeza Pikipiki 240 zitakazo wasaidia vijana wengi hasa walioko kwenye jumuia ya vijana Mkoani hapa.
Mmoja wa Wanachama wa umoja huo Salome Kasiani mkazi wa Kwimba alisema kuwa ajira ni kitu chochote ambacho kinaweza kukupatia pesa sio lazima uwajiriwe, watu wengi wamekuwa wanazitazama kazi ya kuendesha Pikipiki ni ya wanaume pakee yao lakini hata sisi wanawake tunaweza .
Aidha alisema kuwa atahamasisha wanawake wenzake huko Kwimba ili wajitokeze kwa wingi na kujiunga na chama ili wafaidike na chama kwa kujipatia mikopo ya pikipiki ili kuendesha maisha yao. “Mimi nawaomba wanawake wenzangu wasichaguwe kazi kusema hii kwamba ni ya mwanaume nah ii ni ya mwanamke mimi nitajivika jukumu hili kuhamasisha wanawake wajiunge na chama ili kufaidika” alisema Salome.