USAJILI wa timu za mikoa inayoshiriki mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu umekuwa na mwitikio mkubwa miongoni mwa vijana wa umri huo katika mikoa ya Temeke, Ilala, Kinondoni na Tanga.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti makatibu wa mikoa hiyo ambao ndiyo wanaoratibu zoezi hilo la usajili wamesema... kuwa vijana wengi wamejitokeza kiasi cha kulazimika kufanya mchujo ili kupata timu sita zinazotakiwa kushiriki Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa.
Katibu wa mkoa wa kisoka wa Temeke, Mbarouk Mohamed alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa kumekuwa na mwitikio wa ajabu ambapo zaidi ya timu mia zimejitokeza na kuwalazimu kuanza kufanya mchujo kwa kuzingatia vipaji ili kupata idadi ya timu sita zinazohitajika kushiriki. “Kwa kweli ni vijana wengi mno wanaotaka kushiriki mashindano haya ya Airtel Rising Stars na tunaamini kuwa kujitokeza kwao kwa wingi kunatupa wigo mpana wa kupata wachezaji wazuri watakao...