KUNDI la majambazi limeteka mabasi matano, mojawapo likiwa la wanajeshi wa Rwanda na kupora abiria na kisha kuwacharaza viboko.
Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi alfajiri katika Kijiji cha Kikoma kilichoko Kata ya Rusahunga, Wilaya ya Biharamulo.Mashuhuda wameeleza kuwa majambazi hao wakiwa na silaha za kivita, waliweka kizuizi na kuyasimamisha magari hayo moja baada ya jingine kisha, kuwashusha abiria na kuwapora kila kitu.
“Baada ya kuwapora abiria, waliamua kuwacharaza viboko mmoja baada ya mwingine, kisha kutokomea kusikojulikana,” alisema shuhuda mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe na kuongeza:
“Magari yaliyotekwa ni Toyota Hiace, gari moja ni la wanajeshi waliokuwa wakitokea Rwanda kwenda Dar es Salaam.”
Diwani wa Kata ya Rusahunga, Amon Mizengo alisema tukio hilo lilihusisha majambazi wanane waliokuwa na bunduki sita za kivita.
Diwani huyo alisema magari yaliyotekwa yalikuwa yakitokea...