Eneo la Kigamboni, Dar es Salaam limeondolewa katika utawala wa Manispaa ya Temeke na kuundwa muundo mpya wa Wakala wa Kusimamia Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) itakayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji. Wakala huyo ametengewa bajeti inayojumuisha fidia ya Sh trilioni 11.5, fedha zitakazotolewa na Serikali na sekta binafsi kwa miaka 20 mpaka mwaka 2032 na kwa mwaka huu, Sh bilioni 60 zimetengwa kuanzisha wakala huyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari kuhusu uendelezaji wa mji huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema utajengwa nyumba za kisasa na utakuwa na wakazi zaidi ya 400,000 wakati kwa sasa kuna wakazi 80,000 tu.
Pia wakala huyo atakuwa na wakurugenzi sita ambao watakuwa wakuu wa idara huku ikisimamiwa na Bodi na Baraza la Ushauri ambalo litakuwa na wajumbe wanaowakilisha wadau wote hususan wabunge na madiwani wa eneo litakaloendelezwa na KDA.
KDA itasimamia uendelezaji wa mji mpya Kigamboni kama Mamlaka ya Upangaji Mji katika eneo lenye ukubwa wa...