Pages

FACEBOOK YAJIPANGA KUWASAIDIA WATU MASIKINI WASIO MUDU GHARAMA ZA INTERNET

Facebook , Mark Zuckerberg. Mpango wa kuhakikisha internet inawafikia watu wengine bilioni 5 waliosalia duniani umeanzishwa na mwanzilishi wa Facebook , Mark Zuckerberg.
Mtandao huo wa kijamii umeungana na makampuni ya Ericsson, MediaTek, Nokia, Opera, Qualcomm na Samsung, na mengine kupunguza gharama za data.
Kundi hilo limesema linataka watu kwenye nchi zinazoendelea wawe sehemu ya jumuiya ya internet. Zuckerberg alisema lengo ni kuwafikishia internet watu ambao hawawezi kumudu gharama za internet.
Mpaka sasa ni watu bilioni 2.7 tu ndo wenye uwezo wa kupata internet ambayo ni sawa na theluthi ya idadi ya watu duniani.

Correspondents Wanted..!!

Job Ref: HR-CORR-08-2013
Young, Know the ‘Hood’ and Want to Write?
You could be just the person we are looking for Nairobi’s newest, newsiest and most exciting newspaper is looking for correspondents to cover their own neighbourhood.

Apart from reporting for the paper, you should be able to:
Take still pictures
Shoot short videos
Report breaking stories via SMS, Whatsapp or any other digital means
And, if you have the talent and can prove it, we’re happy to enlist you as our correspondent
Interested and itching to start?

Send your CV and application to http://careers.nationmedia.com before 2nd September, 2013 with details of your education, your career to date, why you think this is just the job for you and which neighbourhood you will be covering.

BEEMAN FT. WYRE - KIZUNGUZUNGU (OFFICIAL VIDEO)

Mwanamke Wa Miaka 64 Amevunja Rekodi Kwa Kuogelea Kutoka Cuba Mpaka Florida, Amefanikiwa Kutumia Masaa 52 Baada ya Kujaribu Mara 35

Diana Nyad
Mwogeleaji mwenye umri wa miaka 64 kutoka Marekani, Diana Nyad ameweka rekodi mpya ya dunia katika kuogelea baada ya kufanikiwa kuogelea kutoka Havanna Cuba mpaka huko Florida Marekani.
Ikiwa hii ni mara ya 35 mfululizo kufanya jaribio kama hili na kwa jumla ya hesabu, ameweza kukaa ndani ya bahari kwa masaa 52, dakika 54, na sekunde 18.6, na aliweza kutoka mwenyewe mpaka beach kabla ya kuishiwa nguvu kabisa.
Diana NyadSafari ya mwanamama huyu imekuwa na umbali wa jumla ya maili 110 sawa na kilometa 180.
Safari zote ambazo mwanamama huyu amekuwa akijaribu kuvuka bahari amekuwa akipata changamoto kama vile kushambuliwa na samaki wakali wa baharini na mambo mengi ya kufanana na hayo lakini hakukata tamaa kujaribu tena na tena na safari hii amefanikiwa bila kutumia vifaa vya kujikinga.
 Diana NyadMwanamama huyu amesema kuwa amejifunza kuwa katika safari ka kufuatilia kutimiza ndoto zako, usikate tamaa hata siku moja, na hakuna swala la kizuizi cha umri katika kufuatilia ndoto zako.
 Diana Nyad

CENTRAL ZONE ft SLIM SAL - TUKUTANE BENKI (Audio)

CENTRAL ZONE ft SLIM SAL - TUKUTANE BENKI

MSAADA KWA HUYU KIJANA

Zuberi Mgeni ZuberiKufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.
Zuberi Mgeni Zuberi alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.

Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.
Shughuli wanazo fanya ni Uvuvi na Ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwahiyo walikuwa wa kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika Mwaka 2011 Juni.

Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo.
Zuberi Mgeni Zuberi Chakusikitisha nikuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa Tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6000 za Kimarikani sawa na Shs.9,600,000/= za Tanzania.

Zikipatikana anaweza kusafirishwa na Msaidizi wake mmoja. Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia Nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492 Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui na Mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.

Msaada wa ki Fedha unaweza kutumwa kwenye Akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa Fedha za Kigeni Bank ya Exim Tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.
Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.
SHUKRAN

MELI KUBWA YA MIZIGO KULIKO ZOTE DUNIANI!!

MELI kubwa ya Mizigo Kubwa kuliko zote duniani. Inaitwa Maersk triple E.
Ina UREFU wa wastani wa zaidi ya Viwanja VINNE vya mpira (Wastani wa Mita 400). UPANA ni Mita 59. Urefu wa Kwenda Juu (KIMO) cha Mita 79.
Inaweza kubeba zaidi ya magari ELF30.
Meli hiyo iliyotengenezwa na "Mkorea" ni mali ya kampuni ya Kidenmark ya MAERSK.
Itatumika kwa kusafirisha mizigo kati ya bara la ASIA na ULAYA.
MAERSK
CNN

MTOTO WA MIAKA 14 ALIEZAA MAPACHA WATATU BABA PIA NI MTOTO ANA MIAKA 16..

Kakamega
Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye umri wa miaka 14 Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika kijiji cha Harambee katika wilaya ya Kakamega amejifungua watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana wawili kati yao
wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine akiwa na uzito wa Kilogram 1.3.
Nesi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Bugoma Bi,Mary Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini hapo. Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba Mzazi wa watoto hao watatu waliozaliwa bado ni mtoto mdogo kama alivyo Mama yao kwani Baba yao ana Umri wa Miaka 16 ambae pia bado anasoma, Zaidi aliishukuru sana Serikali kwa kuweza kuondoa garama kwa wajawazito wakiwa wanajifungua na ivyo kuweza kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo Garama zozote zile.

TIMU YA CRICKET YA WAMASAI AMBAYO IPO ZIARANI LONDON UK

CRICKET
 CRICKET
CRICKET
CRICKET
 CRICKET
Jestina-George

Dayna - Naumia (Audio)

Dayna