Pages

MATUSI NA KEJELI ZA KAGAME ZAMDUWAZA KIKWETE.

Rwanda, Rais Jakaya Kikwete
Baada ya kushambuliwa kwa kejeli na Rwanda, Rais Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kueleza kushangazwa na kauli hizo na maneno yasiyofaa yanayotolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.

Badala yake amesema Tanzania haina mgogoro wowote na nchi hiyo wala haiwezi kufanya vitendo vyovyote vibaya dhidi yake, nchi nyingine jirani au yoyote duniani, kwani migogoro haina tija wala maslahi kwa Watanzania.
Rais Kikwete alieleza mshangao huo jana katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi ya kuzungumza na taifa, na kusema kuwa yeye binafsi na serikali ya Tanzania haina ugomvi wala nia yoyote mbaya na Rwanda.
"Napenda kuwahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano na ushirikiano wetu. Mambo yapo vile vile.
Kwa upande wangu, binafsi, sijasema lo lote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu," alisema na kuongeza:
"Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha. Sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake.
Kwangu mimi sioni kama kuna mgogoro wa aina yoyote. Busara inatuelekeza kuwa tusikuze mgogoro usiokuwepo. Waingereza wanasema 'two wrongs do not make a right'.
Alikiri kuwa katika kipindi cha miezi miwili uhusiano baina ya nchi hizo umekuwa ukipita katika kipindi kigumu na kwamba kauli za viongozi wa Rwanda dhidi yake na nchi ni ushahidi wa hali hiyo.
"Napenda kuwasisitizia kuwa mimi na serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi nyingine yoyote duniani.
Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kwani mambo hayo hayana tija wala maslahi kwetu," alisema.
Rais Kikwete aliwahakikishia Watanzania na Wanyarwanda kuwa, Tanzania inapenda kuwa na uhusiano na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo uhusiano wake na nchi zingine jirani na kuongeza kuwa kama majirani kila mmoja anamhitaji mwenzake, hivyo lazima uwepo uhusiano mwema.
Kwa mujibu wa Rais, wakati Tanzania imekuwa ikijihusisha siku zote na kukuza na kujenga ujirani mwema, kufanya mambo ambayo yatasaidia kuimarisha uhusiano kwa maslahi ya nchi zote mbili na kwamba hiyo ni moja ya nguzo kuu ya Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania kabla na baada ya kutokea sintofahamu.
Alisema Rwanda na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri miaka mingi, zikishirikiana na kusaidiana katika mambo mengi kitaifa, katika kanda ya Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu, Umoja wa Afrika na hata kimataifa, hata hivyo mtikisiko huo umekuja baada ya kutoa ushauri kwa serikali ya Rwanda kufanya mazungumzo na mahasimu wao.
"Nilitoa ushauri ule kwa nia njema kabisa kwani bado naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vyema itumike. Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya Kongo (DRC) na kwa Serikali ya Uganda.
Katika mkutano ule Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli yangu. Rais wa Rwanda hakusema chochote pale mkutanoni lakini baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia na tunayoendelea kuyasikia," alisema.
Rais Kikwete alisema anastaajabu jinsi Rwanda ilivyouchukulia ushauri wake na haufanani na wanayoyafanya, huku akisisitiza kuwa alifanya vile kwa kuzingatia mila na desturi za miaka mingi katika ukanda huo.
Alisema ni kawaida kukutana katika mikutano na vikao mbalimbali kuzungumza na kushauriana kwa uwazi juu ya njia za kushughulikia matatizo na masuala mbalimbali kila yanapotokea na kwamba wakati waliyachukulia kuwa ni mambo yanayohusu wote, hivyo kupeana ushauri ni wajibu wa wote.
"Mara nyingi ushauri kwa wanaogombana kuzungumza tunautumia sana. Iweje leo mtu kutoa ushauri ule lionekane jambo baya na la ajabu. Jambo la kushutumiwa na kutukanwa!
Siyo sawa hata kidogo!! Ushauri si shuruti, ushauri si amri. Una hiyari ya kuukubali au kuukataa. Muungwana hujibu: "Siuafiki ushauri wako". Hakuna haja ya kutukana wala kusema maneno yasiyostahili wala kusema yasiyokuwepo na ya uongo," alisema.
Alisisitiza Tanzania inapenda kuendelea na uhusiano mzuri na Rwanda na kuongeza kuwa labda kama Rwanda ina jambo dhidi ya Tanzania, kwa kile alichosema kusikia mengi yanayozungumzwa na kudaiwa kupangwa kufanywa na Rwanda dhidi yake na nchi. Hata hivyo, alisema hapendi kuyaamini hayo yanayosemwa moja kwa moja lakini pia kama nchi hawatayapuuza.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete alisema kauli yake aliyoitoa katika Sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa ilitafsiriwa vibaya na kwamba hakutaja mtu wala nchi yoyote bali alizungumzia wajibu wa majeshi na raia kulinda uhuru na mipaka ya nchi.
Rais Kikwete alisema hataruhusu mtu au nchi yoyote kupokonya wala kuichezea haki ya Watanzania hiyo na kusisitiza utayari wa nchi kulinda mipaka yake, huku akitoa mfano wa mashujaa waliofariki dunia kwa kulinda nchi kuwa ni fundisho kwa mtu yeyote anayetamani kumega kipande chochote cha ardhi ya nchi ya Tanzania.
Baada ya kutoa kauli hiyo baadhi ya vyombo vya habari vilitafsiri kauli hiyo kuwa amewasema Malawi na Rwanda kutokana na kuwepo sintofahamu na viongozi wa nchi hiyo. Malawi na Tanzania wanagombea mpaka wa Ziwa Nyasa.
Alisisitiza kauli yake ya awali aliyoitoa mkoani Kagera ya kuwapa siku 14 wale wanaohusika na ujambazi, uhamiaji haramu na uingizaji haramu wa mifugo waamue kuchukua hatua muafaka sasa, badala ya kusubiri operesheni iwakute, wala wasifikirie kuwa hili ni jambo la kupita.
Pia alizungumzia ziara za viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama ambapo alisema ziara ya kiongozi huyo imeimarisha uhusiano mzuri baina ya mataifa mbalimbali pamoja na kutoa fursa na miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Alisema katika ziara hiyo, Rais Obama pia alielezea nia ya Serikali yake kutaka kuwepo mpango wa kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo ameielekeza Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kutengeneza mkakati utakaoonesha jinsi watakavyojipanga kufaidika na mpango huo.
Alitaja viongozi wengine ambao walifanya ziara hapa nchini kuwa ni Rais Mstaafu wa Marekani, George W Bush, Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair na Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, ambapo ziara za viongozi hao wote zinaonesha utayari wa dunia kuunga mkono jitihada za Tanzania kujiletea maendeleo.

Raila Odinga and Kalonzo Get 12 Security Personnel Each.!!

Former Prime Minister Raila Odinga and former Vice President Kalonzo Musyoka have been allocated 2 vehicles each and 12 security guards and the government is now demanding that they return any extra vehicles in their possession. This demand sent to the two CORD leaders was made a week ago. Ken Mijungu reports

LHRC na TLC Wamshtaki Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Pinda.

Kituo cha sheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika kimewasilisha mahakama kuu jijini Dar-es-Salaam, shauri la mashtaka dhidi ya waziri mkuu wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania ,Mheshmiwa Mizengo Pinda na mwanasheria mkuu wa serikali Mheshimiwa jaji Fredrick Werema.

16 People Arrested In ERC Gas Crackdown

Sixteen people have been arrested and 408 gas cylinders of assorted brands and sizes confiscated in a crackdown carried out by the Energy Regulatory Commission-ERC in collaboration with officers from the flying squad. According to the energy sector regulator, establishments dealing in the product pose a grave danger since they don't meet the minimum safety standards.

Mchezaji nyota wa NBA Ameendesha Clinic ya Mpira wa Kikapu ya Vijana Don Bosco -Namanga

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Stephen Curry anaecheza ligi ya NBA katika timu ya Golden State warriors ya nchini Marekani amendesha clinic ya mpira wa kikapu ya vijana karibu mia moja wa umri wa kuanza miaka 14 -18 katika kituo cha Don Bosco kilichopo Namanga.

Nay wa Mitego -Salam Zao (Audio)

Nay wa Mitego -Salam Zao

Kazi Ipo..

Shashow ft Nician - Msukule (Audio)

Shashow ft Nician - Msukule

Ipe Caption

Caption

Robert Mugabe's Party Claims Victory Over Morgan Tsvangirai..!!

Zimbabwe Poll 'A Huge Farce, Null And Void'


Zimbabwe Prime Minister Morgan Tsvangirai has dismissed the country's national elections as a "huge farce" and the results invalid because of intimidation and ballot-rigging by President Robert Mugabe's ruling party, which has claimed victory.
"In our view, that election is null and void," he said, after a senior Zanu-PF source earlier claimed a resounding victory for President Mugabe in Zimbabwe's presidential and parliamentary elections.
The unnamed senior official said the outcome was already clear and told Reuters news agency: "We've taken this election. We've buried the MDC. We never had any doubt that we were going to win."
The opposition, Mr Tsvangirai's Movement for Democratic Change (MDC), immediately claimed the elections had been "a monumental fraud" and held an emergency meeting.  Zanu-PF
A woman with a child casts her vote in Domboshava, north of Harare
"Zimbabweans have been taken for a ride by Zanu-PF and Mugabe, we do not accept it," a senior source told Reuters.
Releasing results early is illegal, and the police had warned they would arrest anybody making premature claims before the official five days the Zimbabwe Electoral Commission had said it could take to announce the result.
Riot police took up positions outside the Zanu-PF party's headquarters in central Harare and other key locations in the capital, including an MDC office.
The party later withdrew what it said was an unauthorised message on its Twitter feed claiming a landslide win, and insisted that it was awaiting the release of the official count.
The Zimbabwe Election Support Network (ZESN) - the country's leading domestic election monitoring agency - said the credibility of the vote was "seriously compromised" by irregularities on polling day.  Zimbabwe Election Support Network (ZESN
A police officer keeps watch as Zimbabweans queue to cast their votes
It said as many as one million eligible voters were not on the electoral roll, and urban voters, who mainly favour Mr Tsvangirai, had been turned away from polling stations in their thousands.
Conversely, only a small number had been prevented from voting in the countryside, where President Mugabe has most support.
It also cast doubt on the authenticity of the voters' roll, noting that 99.97% of voters in the countryside were registered, compared to 67.9% in urban areas.
"It is not sufficient for elections to be peaceful for elections to be credible," ZESN chairman Solomon Zwana said. "They must offer all citizens ... an equal opportunity to vote."
Separate reports claimed key MDC members had lost their seats, even in the capital, and that the election was looking like a "disaster" for Mr Tsvangirai. Robert Mugabe (L) and Morgan Tsvangirai
Polling rivals Robert Mugabe (L) and Morgan Tsvangirai cast their votes
To win an outright victory, one of the candidates has to secure more than 50% of the vote.
Half the country's 12.9 million population was eligible to vote at the more than 9,000 polling stations nationwide.The dispute erupted as polling stations closed and counting got under way amid fears of a repeat of the violence that marred the 2008 election.
Turnout was high, particularly in urban areas where the polling stations stayed open late into the evening to allow everyone in the queues to cast their votes.
The presidential contest pit the 89-year-old incumbent President Mugabe against his main rival Mr Tsvangirai, who his supporters believed a big turnout would favour, blunting the impact of any manipulation of the vote. Zimbabwe
A ballot paper with the images of all the presidential candidates
Zimbabweans voted in large numbers despite concerns about the credibility of the electoral process, and the vote was relatively peaceful compared to disputed and violent polls in 2008.
However, the fiercely contested election was dogged by claims of intimidation and vote rigging, despite assurances by official poll monitors of "a peaceful, orderly and free and fair vote".
It is the third time Mr Tsvangirai has tried to unseat President Mugabe, who denies vote rigging and said he would step down if he failed to extend his 33-year grip on power for another five years.

Sky Correspondent Emma Hurd, in South Africa, said: "Analysts inside Zimbabwe say it was going to be close anyway - that Robert Mugabe was not going to be wiped out in a landslide victory by the opposition.
"But what all independent observers seem to agree on is that there will have been some element of rigging in the process."The question remains how much, and whether Robert Mugabe really needed to do it in the first place to win."
Sky News report