Pages

Interpol Yamtia Mbaroni Alex Massawe Dubai

Alex Massawe DubaiDar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe ambaye alikuwa anatafutwa na Polisi wa Tanzania kwa muda mrefu, amekatwa Dubai, Falme za Kiarabu (UAE).

Mkuu wa la Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol), Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliliambia gazeti hili jana kwamba Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai akitokea Afrika Kusini.
Babile alisema hivi sasa walikuwa wanaandaa taratibu za kumrudisha nchini ambako amekuwa akisakwa kwa muda mrefu.
“Ombi la kuleta mhalifu nchini kutoka nje ya nchi (extradition request), lina hatua ndefu. Unajua kuna mlolongo wa taratibu za kutekeleza ili Massawe aletwe. Kwanza lazima Polisi wa Tanzania watoe tangazo kwa Interpol kuhusu kumsaka mtu huyo ili aletwe,” alisema Babile.
Alisema Massawe alikamatwa wakati akifanya taratibu za ukaguzi baada ya kuwasili UAE.

Habari zilizofikia gazeti hili mapema kutoka Dubai zilieleza kuwa Massawe alikamatwa na maofisa wa usalama wa UAE kutokana na alama zake za vidole na kuonyesha kuwa alikuwamo kwenye orodha ya watu waliokuwa wanasakwa na Interpol.

Massawe ambaye anamiliki majumba na biashara ya utalii katika Miji ya Arusha, Dar es Salaam na Moshi, inadaiwa kwamba alikutwa na pasi tatu bandia za kusafiria zilizokuwa na majina tofauti wakati alama zake za vidole zilionyesha anaitwa Alex Massawe.

“Maofisa wa Usalama wa uwanja wa ndege walimuuliza kuwa wewe ndiye Alex Massawe? Alikana lakini alielezwa kuwa alama za vidole vinaonyesha anaitwa hivyo,” kilidokeza chanzo cha habari hizi kwa simu kutoka Dubai. Hata hivyo, Babile alisema hakuwa na taarifa za Massawe kukutwa na pasi bandia za kusafiria.

Uvumi wa Aprili

Mapema Aprili 27, mwaka huu kulikuwa na habari kwamba Massawe amekamatwa katika mji mmojawapo ulioko katika Pwani ya Afrika Kusini.

Habari hizo za kukamatwa kwa Massawe, ambaye pia hufadhili masuala ya kisiasa na michezo, zilisambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ya Facebook, Twitter na Jamii Forum. Kulikuwa kuna mkanganyiko wa taarifa huku wengine wakidai alinaswa akiwa ndani ya boti huko Afrika Kusini, wengine wakidai alikamatwa wakati akijaribu kuingia Msumbiji akitokea Malawi.

Akizungumzia hilo Babile alisema huo ulikuwa ni uzushi na baada ya kuzisikia taarifa hizo walifuatilia katika maeneo aliyohusishwa kukamatwa na kubaini kwamba hapakuwa na ukweli wowote.

Kwa nini Massawe anatafutwa
Aprili 4 mwaka huu, mfanyabiashara huyo alitajwa mahakamani katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly ambaye aliuawa katika mazingira ya kutatanisha Novemba 6, 2011 akiwa nyumbani kwake Magomeni, Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo ambayo mshtakiwa wa kwanza ni mfanyabiashara maarufu, Abubakar Marijani ‘Papaa Msofe’ na mshtakiwa mwingine, Makongoro Joseph Nyerere alitoa malalamiko mbele ya Hakimu Mkazi, Agnes Mchome baada ya Wakili wa Serikali, Mwanaisha Kombo kudai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe mpya ya kuitaja. Mshtakiwa huyo, aliomba jalada la kesi yao lipelekwe mahakamani hapo kwa ajili ya kulifanyia kazi na kutuhumu kuwa ndugu wa marehemu Kituly hawataki maendeleo ya kesi yao hadi Massawe akamatwe.
Mwananchi

KaKobe

KaKobe

MBUNGE LEMA ASOMEWA MASHTAKA

Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA) MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), jana alisomewa maelezo ya awali kwenye kesi ya uchochezi inayomkabili, anayodaiwa kutoa kauli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alikwenda kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha kama anakwenda kwenye sherehe za kuaga mtoto wa kike ‘send off’.
Akisoma maelezo, Wakili wa Serikali, Elianenyi Njiro, mbele ya Hakimu Mkazi, Devotha Msofe, anayesikiliza shauri hilo, alidai wanatarajia kupeleka mashahidi tisa akiwamo Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), John Nanyaro na Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Arusha (OCD), Gillis Mroto.
Aliwataja mashahidi wengine kuwa ni maofisa wa Jeshi la Polisi akiwamo Mkaguzi Bernard Nyambanya na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane, PC Godfrey, Joachim Mahanyu na wengine kutoka Chuo cha Uhasibu, ambao ni Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu Hamidu.
Awali akisoma maelezo hayo, Wakili Njiro aliieleza mahakama hiyo kuwa Aprili 24, mwaka huu, Lema akiwa eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu, alitoa maneno ya uchochezi yaliyosababisha uvunjifu wa amani.
Alisema kuwa maneno hayo yanayodaiwa kutamkwa ni kinyume cha kifungu cha 390 sura ya 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu marejeo ya mwaka 2002.
“RC anakuja (Chuo cha Uhasibu), kama anakwenda kwenye sendoff, hajui chuo kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho … (RC), ameshindwa hata kuwapa (wanafunzi) pole kwa kufiwa na amesema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu,” alinukuu baadhi ya maneno aliyodai kuwa yalitamkwa na Lema siku ya tukio.
Wakili Njiro alidai mahakamani hapo kuwa kauli hizo zilipandisha hasira za wanafunzi ambao walianza kumrushia mawe na chupa Mkuu wa Mkoa, Mulongo, alipokuwa akiwahutubia kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi, Henry Koga, kilichotokea Aprili 23, mwaka huu.
Lema kupitia kwa wakili wake, Method Kimomogoro, alikanusha madai hayo huku akikubali maelezo kuhusu jina lake, anwani, makazi na wadhifa wake, ambapo shauri hilo limepangwa kuanza kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 20-22, mwaka huu.

Mgahawa wa Hassan Futari ya Kumwaga

Mgahawa wa Hassan

Wasanii Wanavyotumiwa Kwenye Madawa ya Kulevya -Orijino Komedi Video

Rapper 50 Cent has Removed His Son From His Will..!!

Rapper 50 Cent
 Marquise
Fiddy, as he is known by his fans, sent volatile text messages to his 16-year-old son Marquise in November last year, saying he planned to cut the boy and his mother off.

According to the Daily Mail, the texts came to light a day after the rapper was also shown to have sent abusive texts to his son in January this year, calling the kid a “s**t head”, “motherf***er” and “f***ing stupid”. In his January tirade, 50 Cent also demands a paternity test and tell his son to delete his number, saying “f*** you stop texting me”.

The rapper’s angry outburst allegedly stemmed from a poorly co-ordinated custody visitation. 50 Cent claims he went to see his son, but was left standing outside the house as no one answered the door. The rapper insisted that Marquise knew he was waiting outside and that he had spotted him peering at his father through the blinds.

“I don't have a son anymore,” tweeted the rapper after the incident.

This family feud, however, has been a long time in the making. In November, 2012, Fiddy wrote to his son: “If I died today would it matter to you? I’m changing my will. It’s a simple question.”

Marquise’s response highlighted the breakdown in the relationship between father and son.

“And this is coming from someone that didn't wish me a happy birthday.”

When Fiddy responded with his threat to remove Marquise and his mother from his will, the teenager replied: “I don't care about money, that's my last concern, of course we all like nice things but it's not everything.”
In his defence, 50 Cent claims that Marquise’s mother was the one texting back, and not his son.
 Marquise
Meanwhile, the rapper also has legal issues to deal with. He has been charged with one count of misdemeanour domestic violence and four counts of vandalism after he allegedly kicked a woman and destroyed $7000 worth of property at her condominium in Los Angeles last month.
According to Los Angeles City Attorney Frank Mateljan, 50 Cent kicked in a door and destroyed a piece of furniture, a chandelier and a television set.
“The altercation apparently started from an allegation of infidelity on her part,” Mateljan said.

The rapper faces a maximum penalty of five years in jail and $46 000 in fines if he is convicted.

How to Prepare For The Summer Fasts: Ramadan Kareem 2013 (Video)

Ratiba ya Ramadhani DMV

 Ratiba ya Ramadhani DMV

Ramadan Wishes from DarSlam Team

Ramadan Wishes

Ramadan Kareem

ZITTO KABWE AWATAKA WANANCHI WAGOME KUILIPA KODI YA SIMU YA SH. 1000 KWA SABABU ILIPITISHWA KINYEMELA

 kodi ya line ya simu
Sakata la kodi ya line ya simu limeendelea kuwakuna wanasiasa wetu ambao wamekuwa wakifunguka kwa nyakati mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.
Baada ya January Makamba, Zitto Kabwe naye amefunguka na kudai kuwa kodi hiyo ni batili na ilipitishwa kinyemela kwa sababu ilikuwa imeshaondolewa....
Huu ni ujumbe wake aliouweka katika account yake ya facebook:
 kodi ya line ya simu
Baada ya kauli hiyo,Zitto Kabwe aliandamwa na maswali mengi sana toka kwa wananchi wakidai kuwa "Makamba alisema tuwalaumu ninyi maana ninyi wabunge ndo mlibariki kodi hii"
Zitto naye alishindwa kulijibu swali hilo na kuwataka wananchi "wachukue simu zao, wawapigie wabunge wao wawaulize ni kwa nini walipitisha kodi hii"
 January Makamba, Zitto kabwe
"Anasema hiyo kwa sababu wabunge ndio waliopitisha.Wabunge ndio wawakilishi wa wananchi.Jambo likipita bungeni hao ndio wa kwanza kulaumiwa.Yupo sahihi kabisa.Mpigie mbunge wako simu muulize kwa nini alikubali au hakupinga kodi hii"