Pages

Matangazo Msimu wa SabaSaba. Wahi Mapema, Nafasi ni Yako Kabla Haijachukuliwa!!

Matangazo Msimu wa SabaSaba
Kwa wadau wetu walio na matangazo ya aina yoyote na ukubwa wa saiz yoyote ikiwa ni pamoja kama unakodisha au unauza Shamba, Nyumba, Gari, Duka, Saluni, Ofisi,Kiwanda, Kampuni na Kadhalika.
 Pia ni fursa kwako kua Sponsor wetu kwa matangazo ya muda mrefu. 
Kumbuka mtandao wetu ni maarufu unatembelewa na watu wote ulimwenguni kutokana na mfumo wetu wa usambazaji wa habari ktk tovuti zetu nyingine pia mitandao ya kijamii. ..Hii ni nafasi yako. Wahi sasa..!! Bei ni nafuu sana.  
Kwa maelewano usisite kutuandikia Barua pepe kupitia darslam@rocketmail.com  
Pia tunapokea habari mbalimbali buree.
         Bila kusahau Blog yako ya Taifa  ..Bongo Blogs - Blog za Bongo
Inakupa fursa husika.
Kazi ni kwako...!

Supermoon to Light Up Night Sky June 23,2013

 super moon

G.P. Mafia - Da Covenant ft. Louieville Sluggah (Official Video)

Dr ASHA-ROSE MIGIRO AFAGILIWA NA RADIO ONE KWA KUKIENZI KISWAHILI

 Asha-Rose Migiro Dr. Asha-Rose Migiro
DAR ES SALAAM, Tanzania
NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.
Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.
"Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;
   "Mmoja wa Watanzania hawa naomba nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya...

HATIMAYE JUMA KASEJA ATEMWA SIMBA RASMI

 SimbaDAR ES SALAAM, Baada ya miaka 10 ya ‘ndoa’ kati ya kipa Juma Kaseja na Simba ya Dar es Salaam, klabu hiyo ya jezi nyekundu na nyeupe kutoka Mtaa wa Msimbazi imetangaza rasmi kuachana naye.
Kaseja alisajiliwa Simba mwaka 2003 akitoka klabu ya Moro United, na tangu wakati huo alikuwa kipa tegemeo wa Simba kwa misimu tisa akiiwezesha kutwaa mataji kadhaa ya Ligi Kuu.

Katika kipindi chote cha kucheza Simba, Kaseja ambaye pia ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ni mara moja tu mwaka 2009 alijiunga na mahasimu wakubwa wa Simba, Yanga na kucheza msimu mmoja.
Uamuzi wa kuachana na Kaseja ulifikiwa na Kikao cha Kamati ya Ufundi kilichoketi juzi na jana na kuamua kutoendelea naye tena baada ya mkataba wake kumalizika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Danny Manembe alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, klabu yao ina makipa watatu wapya, hivyo hawana tena sababu ya kuendelea na Kaseja.
Makipa waliopo Simba kwa sasa ni Abel Thaira, Andrew Ntala aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar na Abuu Magube aliyepandishwa kutoka kikosi B.
“Tuna makipa watatu, hawa ni wengi sana kwetu. Hatuwezi tena kuongeza kipa mwingine, hivyo Kaseja tunaachana naye,” alisema Manembe. Akiongeza, Manembe alisema kocha mpya wa Simba, Abdallah Kibadeni katika orodha ya wachezaji anaowataka kwa ajili ya msimu ujao, hakumjumuisha Kaseja hivyo na wao wameamua kuachana naye.

Muda mfupi kabla ya Simba kutangaza uamuzi huo, Mwananchi iliwasiliana na Kaseja ambaye alisema: “Sitaki kuzungumzia habari za Simba kwa sasa, nina mambo mengi muhimu nataka kuyafanya.”
Itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kuanza msimu wa ligi bila Kaseja kwa miaka tisa, huku kipa huyo pia akiweka rekodi ya kucheza mechi nyingi za watani, ambapo mpaka anatemwa ameshasimama longoni mechi 25.

Viva Ft Burney Mc(Uganda), Willy Fololo(Kenya) - East African Metaphor (Audio)

East African Metaphor

ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL 2013


ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL

Soma Tweet ya Tusi la Mbuge wa Mbeya kwa Waziri Mkuu

Katika hali yakushangaza , mbunge wa mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, mh. SUGU ameporomosha tusi zito kwa waziri mkuu wa Tanzania
Tusi la Sugu limekuja baada ya waziri mkuu kuwaruhusu rasimi polisi kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti wananchi kwa kuwashushia kichapo ili wazitii sheria.....
Tweet ya tusi la mbuge wa mbeya kwa waziri mkuu...
Tweet ya tusi la mbuge wa mbeya kwa waziri mkuu

Sherehe za Mahafali ya Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar.

 Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar
Mkurugenzi Masoko wa Kampunin ya Simu ya ZANTEL Mohammed Baucha akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Kiislam wakati wa maadhimisho ya Mahafali ya 11 yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho huko Mazizini Zanzibar nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar
Mkuu wa Chuo cha Kiislam Zanzibar Dk. Muhidin akihutubia wakati wa mahafali hayo ya 11ya Chuo cha Kiislam Zanzibar ikiwa ni sherehe za maadhimisho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Mazizini.

ZOEZI LA UOKOAJI WAHANGA WA MAFURIKO INDIA ZINAENDELEA

Sushil Kumar Shinde
Shughuli ya kuwaokoa maelfu ya watu waliokwama kaskazini mashariki mwa India kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi inaendelea kufanyika nchini humo.Waziri wa mambo ya nje Sushil Kumar Shinde amesema kiasi ya watu 30,000 tayari wameshahamishwa kutoka maeneo mbali mbali ya jimbo la milimani la Himachal Pradesh na kwamba maelfu ya wengine bado wamekwama.Shinde aliyasema hayo baada ya kulizuru eneo hilo kwa ndege. Afisa wa kushughulikia majanga kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Dehradun amesema kuwa itachukua kipindi cha hadi wiki moja kuwaokoa watu hao takriban 30,000. Kundi la watalii 17 limehamishwa kwa ndege kutoka eneo la Dharasu huku kundi la mahujaji kiasi ya 1,000 wameonekana katika eneo kati ya Kedarnath na Gaurikund.Jumla ya miili 556 imepatikana chini ya vifusi vya majengo yaliyopromoka kutokana na maporomoko ya ardhi na inahofiwa kuwa miili zaidi imekwama chini ya vifusi hivyo.Jeshi la nchi hiyo,polisi na maafisa wa jimbo hilo wanashiriki katika shughuli hiyo ya uokozi na kutoa misaada ya dharura.Karibu helikopta 32 zinatumika katika shughuli hiyo.