Pages

HATIMAYE JUMA KASEJA ATEMWA SIMBA RASMI

 SimbaDAR ES SALAAM, Baada ya miaka 10 ya ‘ndoa’ kati ya kipa Juma Kaseja na Simba ya Dar es Salaam, klabu hiyo ya jezi nyekundu na nyeupe kutoka Mtaa wa Msimbazi imetangaza rasmi kuachana naye.
Kaseja alisajiliwa Simba mwaka 2003 akitoka klabu ya Moro United, na tangu wakati huo alikuwa kipa tegemeo wa Simba kwa misimu tisa akiiwezesha kutwaa mataji kadhaa ya Ligi Kuu.

Katika kipindi chote cha kucheza Simba, Kaseja ambaye pia ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ni mara moja tu mwaka 2009 alijiunga na mahasimu wakubwa wa Simba, Yanga na kucheza msimu mmoja.
Uamuzi wa kuachana na Kaseja ulifikiwa na Kikao cha Kamati ya Ufundi kilichoketi juzi na jana na kuamua kutoendelea naye tena baada ya mkataba wake kumalizika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Danny Manembe alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, klabu yao ina makipa watatu wapya, hivyo hawana tena sababu ya kuendelea na Kaseja.
Makipa waliopo Simba kwa sasa ni Abel Thaira, Andrew Ntala aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar na Abuu Magube aliyepandishwa kutoka kikosi B.
“Tuna makipa watatu, hawa ni wengi sana kwetu. Hatuwezi tena kuongeza kipa mwingine, hivyo Kaseja tunaachana naye,” alisema Manembe. Akiongeza, Manembe alisema kocha mpya wa Simba, Abdallah Kibadeni katika orodha ya wachezaji anaowataka kwa ajili ya msimu ujao, hakumjumuisha Kaseja hivyo na wao wameamua kuachana naye.

Muda mfupi kabla ya Simba kutangaza uamuzi huo, Mwananchi iliwasiliana na Kaseja ambaye alisema: “Sitaki kuzungumzia habari za Simba kwa sasa, nina mambo mengi muhimu nataka kuyafanya.”
Itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kuanza msimu wa ligi bila Kaseja kwa miaka tisa, huku kipa huyo pia akiweka rekodi ya kucheza mechi nyingi za watani, ambapo mpaka anatemwa ameshasimama longoni mechi 25.

Viva Ft Burney Mc(Uganda), Willy Fololo(Kenya) - East African Metaphor (Audio)

East African Metaphor

ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL 2013


ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL

Soma Tweet ya Tusi la Mbuge wa Mbeya kwa Waziri Mkuu

Katika hali yakushangaza , mbunge wa mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, mh. SUGU ameporomosha tusi zito kwa waziri mkuu wa Tanzania
Tusi la Sugu limekuja baada ya waziri mkuu kuwaruhusu rasimi polisi kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti wananchi kwa kuwashushia kichapo ili wazitii sheria.....
Tweet ya tusi la mbuge wa mbeya kwa waziri mkuu...
Tweet ya tusi la mbuge wa mbeya kwa waziri mkuu

Sherehe za Mahafali ya Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar.

 Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar
Mkurugenzi Masoko wa Kampunin ya Simu ya ZANTEL Mohammed Baucha akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Kiislam wakati wa maadhimisho ya Mahafali ya 11 yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho huko Mazizini Zanzibar nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 Chuo cha Kiislam Mazizinin Zanzibar
Mkuu wa Chuo cha Kiislam Zanzibar Dk. Muhidin akihutubia wakati wa mahafali hayo ya 11ya Chuo cha Kiislam Zanzibar ikiwa ni sherehe za maadhimisho hayo yaliofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Mazizini.

ZOEZI LA UOKOAJI WAHANGA WA MAFURIKO INDIA ZINAENDELEA

Sushil Kumar Shinde
Shughuli ya kuwaokoa maelfu ya watu waliokwama kaskazini mashariki mwa India kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi inaendelea kufanyika nchini humo.Waziri wa mambo ya nje Sushil Kumar Shinde amesema kiasi ya watu 30,000 tayari wameshahamishwa kutoka maeneo mbali mbali ya jimbo la milimani la Himachal Pradesh na kwamba maelfu ya wengine bado wamekwama.Shinde aliyasema hayo baada ya kulizuru eneo hilo kwa ndege. Afisa wa kushughulikia majanga kutoka mji mkuu wa jimbo hilo Dehradun amesema kuwa itachukua kipindi cha hadi wiki moja kuwaokoa watu hao takriban 30,000. Kundi la watalii 17 limehamishwa kwa ndege kutoka eneo la Dharasu huku kundi la mahujaji kiasi ya 1,000 wameonekana katika eneo kati ya Kedarnath na Gaurikund.Jumla ya miili 556 imepatikana chini ya vifusi vya majengo yaliyopromoka kutokana na maporomoko ya ardhi na inahofiwa kuwa miili zaidi imekwama chini ya vifusi hivyo.Jeshi la nchi hiyo,polisi na maafisa wa jimbo hilo wanashiriki katika shughuli hiyo ya uokozi na kutoa misaada ya dharura.Karibu helikopta 32 zinatumika katika shughuli hiyo.

Poetry Addiction - Link Up n' Socialize Whilst Entertained

Poetry AddictionDo you like live Soul music, Hip-Hop, Afro- Soul, Poetry or just looking for a place to network??? Well, look no further , we bring to you Poetry Addiction.

What is Poetry Addiction????
It is an event that brings together artists from different parts of world in an attempt to use the power of music and poetry for a greater cause and will involve different kinds of artists ranging from poets to live music instrumentation. Intends to bring an exceptional brand of music that is not getting the attention it deserves.

Entrance Fee: Tshs. 10,000/=
Date: 29th June 2013
Time: From 8pm to 1am
Venue: Triniti, Msasani Road, Oysterbay
For details, use the numbers below or open the attached poster.
CONTACTS: 0767211680/ 0713424851
It is about time we create a niche musical event that will allow an audience with common interests to link up and socialize whilst entertained by the live performances in a relaxed environment.
See you there..
Sponsored by Choice FM and CheusiDawa TV.

ULE MTIHANI wa WATOTO WA KISHUA SECONDARY SCHOOL, HUU HAPA. KUNA ZAWADI NONO

WATOTO WA KISHUA SECONDARY SCHOOL
S.L.P 7677, MASAKI.
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA.

MAELEKEZO.
i. Jibu maswali yote.
ii. Kila swali linabeba maksi kumi
iii. Zingatia mpangilio wa kazi.
iv. Unaruhusiwa kutumia BLOGS na MAGAZETI YA UDAKU
iv. SWALI LA TISA NI LAZIMA KUJIBU.
MUDA; Masaa matatu.

SECTION A.
1. Kwa kutumia mifano hai, elezea chanzo cha Kim Kadarshian kugombana na Kanye west.
2. Taja tofauti kuu nne kati ya MLIMANI CITY na QUALITY CENTER.
3. Kwa kutumia maeneo ya samakisamaki, Coco beach, Steers, na Kunduchi beach resort elezea maana ya neno BATA.
4. Mapenzi hujengwa kati ya msichana na mvulana. Je Vipini masikioni, Kuvaa mlegezo, mwanaume kusuka na kujipaka carolight vinachangia vipi kufanya penzi lichanue? Fafanua!! Tumia mifano hai ya maboyfriend wa watoto wa kishua
5. Kwa kutumia tamthilia za MARA CLARA na zile nyingine za PROMISE na TIMELESS elezea nafasi ya mwanamke katika jamii.

SECTION B
6. Elezea sababu kuu tano za WEMA na Diamond kugombana!! Na kisha elezea mapinduzi yaliyofanywa na Jokate Mwegelo. Na je kwa nini hawakudumu
7. Inasemekana kuwa Chipsi mayai ni mojawapo ya chakula kinachowachanganya wasichana wengi na mwisho kujikuta wametoa penzi. Kwa kutumia maeneo ya Masaki na Mikocheni elezea Baga na Pizza zinavyosababisha tatizo hili.
8. Kwa kuwatumia wasanii wa Bongofleva kama Diamond na wa mtoni kama Chriss Brown elezea maana ya neno SWAGA.
9. Watoto wengi wa kishua hukimbilia kutafuta mademu wa uswazi wakidai kuwa wasichana wa geti kali hawajui lolote. Elezea kiufasaha ukitumia mifano hai kwanini wasichana wa kishua ni bomu.
10. Kwa kutumia mifano hai ya PLAYSTATION elezea ni ipi ngumu sana kucheza kati ya PS 2 na PS 3…..
NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!!

Janet Jackson Converts To Islam, And Quits Music..!

Islam,Superstar Janet Jackson is reportedly quitting the entertainment industry and is going to leave the country to become a Muslim.
 Rob Shuter tells reporters that Jackson is moving to the Middle East and is converting to Islam.
Shuter says that since she married billionaire Wissam Al Mana, she has grown tired of the grueling entertainment industry.The pair got married last year in a very private ceremony, according to Shuter, and they want to live a private life away from the paparazzi.
Al Mana, a Qatar native, is involved in his family’s controlled Middle-East-based Al Mana Retail Group.
And since marrying Al Mana, Ms. Jackson’s net worth has certainly climbed higher as she is officially became a billionaire sometime in May, this year. However, it’s not clear if her recent billionaire status has anything to do with the fact that she recently married one.
This is Jackson’s third marriage.

Mhadhara wa Prof. Shivji wabadili Mtazamo wa Wengi Kuhusu Muungano.

Rasimu ya katiba mpya kutoeleza mipaka ya kiutawala kwa pande mbili za Tanzania bara na Zanzibar na kuruhusu kila pande kuwa na uwezo wa kuunda jeshi la polisi kunaweza kusababisha migogoro ya kiutawala na kuvuruga amani.