Pages

IDD SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KATIKA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI

KESI Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo hii imemwachiria huru Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Idd Simba pamoja na Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alikuwa Diwani wa Kata Sinza (CCM), Salum Mwaking’inda vile vile Meneja Mkuu wa shirika hilo Victor Milanzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group , Simon Kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo.
Mahakama imewaachia huru washitakiwa kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.

Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa, washitakiwa hao wapo huru.
Happiness Katabazi

Viongozi wa Chadema na Wananchi Waachiliwa Huru kwa Dhamana.. (Video)

Jeshi la polisi nchini limewaachilia kwa dhamana viongozi wa Chadema na wananchi wote waliokuwa wanashikiliwa na limemtaka mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe kuwasilisha ushahidi wa mtu aliyelipua bomu kwenye mkutano kwa Mh. Rais kama hana imani na jeshi la polisi.

Madam Rita na Water Chilambo Wakizindua Bongo Star Search 2013 (Video)

Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji muziki la Epiq Bongo Star Search, EBSS, leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya Zantel umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen a.k.a Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na mmoja wa majaji shindano hilo, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan pamoja mshindi wa shindano hilo mwaka jana, Walter Chilambo.

POETRY ADDICTION Ya FidQ Na CheusiDawaTV Ni Mwezi Huu..!

Poetry Addiction ni kitu kipya kitakachoanaza hivi karibuni chini ya uangalizi wa Fid-Q na CheusiDawaTV … Wameandaa kitu TAREHE 29 JUNE kwa ajili yako … Itahusisha wasanii na activities zingine in it … Wanna know more???? … Check hapa chini;
Poetry Addiction

Did You Know? CRACKING YOUR KNUCKLES DOES NOT ACTUALLY HURT YOUR BONES OR CAUSE ARTHRITIS.

FACTS THE SOUND YOU HEAR IS JUST GAS BUBBLES BURSTING.
Cracking your knuckles (or any of your joints) can have therapeutic benefits. When you crack one of your joints you are pulling the bones that are connected at the joint apart from each other. This process stimulates your tendons, relaxes your muscles, and loosens your joints. Chiropractors do this for spinal joints when your back is sore and stiff, but you can do this on your own for your knuckles, toes, knees, neck, etc.

Unfortunately, there can be too much of a good thing. Cracking your knuckles will never lead to arthritis (despite what your mom keeps telling you), but scientists have discovered that it can cause tissue damage in the affected joints. Knuckle-cracking pulls your finger bones apart which stretches your ligaments. Too much stretching of your ligaments will cause damage to your fingers akin to the arm injuries sustained by a baseball pitcher who throws too many pitches. In addition to making your hand really sore, this ligament damage can also result in reduced grip strength.
How does this work? Your joints, the places in your body where you can bend, are where your bones intersect and are held together by ligaments. These joints are surrounded by a liquid called synovial fluid. When you stretch your ligaments by pulling the bones apart to crack your knuckles a gas in the synovial fluid escapes and turns into a bubble. This process is called cavitation. Cavitation ends when the bubble eventually bursts, producing that popping sound we know and love. After that, your joints won't be able to crack for another 25-30 minutes while the gas gets reabsorbed into the synovial fluid.
OMG FACTS

Wachina Wameanza Kukopesha Mikopo ya Bodaboda

Bodaboda Mkoani Mwanza.
Annastazia Fredy,Mwanza
KAMPUNI ya kuuza Pikipiki kutoka china (FEKON) imetoa mkopo wa Pikipiki 240 zenye thamani ya shilingi 460.8million kwa vijana wanaofanya biashara ya Bodaboda Mkoani Mwanza.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Monarch Hotel Katibu wa jumuia ya vijana Mkoani hapa Abubakari Rubelwa alisema kuwa Kampuni hiyo imekuwa ya kwanza kukubali kutoa mkopo wa Pikipiki hizo ndani ya mwaka mmoja ili kuwawezesha vijana kumudu maisha yao.
“Tunaishukuru Kampuni ya Fekoni kwa sababu ni Kampuni iliyokubali kutukopesha Pikipiki ndani ya mwaka mmoja ambapo kila Pikipiki inagarimu shilingi 1.9million.”alisema Rubelwa.

Aidha Katibu huyo alisema kuwa awali Kampuni hiyo iliwai kutoa Pikipiki 15 zenye thamani ya shilingi 23million vijana wakalipa bila shinda ndiyo maana wameamua kuongeza Pikipiki 240 zitakazo wasaidia vijana wengi hasa walioko kwenye jumuia ya vijana Mkoani hapa.
Mmoja wa Wanachama wa umoja huo Salome Kasiani mkazi wa Kwimba alisema kuwa ajira ni kitu chochote ambacho kinaweza kukupatia pesa sio lazima uwajiriwe, watu wengi wamekuwa wanazitazama kazi ya kuendesha Pikipiki ni ya wanaume pakee yao lakini hata sisi wanawake tunaweza .

Aidha alisema kuwa atahamasisha wanawake wenzake huko Kwimba ili wajitokeze kwa wingi na kujiunga na chama ili wafaidike na chama kwa kujipatia mikopo ya pikipiki ili kuendesha maisha yao. “Mimi nawaomba wanawake wenzangu wasichaguwe kazi kusema hii kwamba ni ya mwanaume nah ii ni ya mwanamke mimi nitajivika jukumu hili kuhamasisha wanawake wajiunge na chama ili kufaidika” alisema Salome.

Prezzo - Celebration of Life (audio)

Mlipuaji wa Bomu la Arusha ni Polisi, Hatukubali Mauaji ya Aina Hii Tena -CHADEMA

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA akizungumza na Waandishi wa Habari jana tarehe 18/06/2013 Makao Makuu ya CHADEMA amesema CHADEMA inao ushahidi wa video kuwa aliyelipua bomu kwenye mkutano wa Chadema Arusha ni Polisi na Polisi wenzake wakamsaidia kutoroka

NAPE ASEMA "MBOWE NA GODBLESS LEMA WANATAKIWA WAWASILISHE USHAHIDI WA TUKIO LA BOMU LA SIVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE"

 CCM, Nape Nnauye Jeshi la Polisi limetishia kuwakamata Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na limesema litamhoji Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wanasiasa hao kudai kufahamu watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja aliwataka wanasiasa hao kuwasilisha ushahidi wa.. kile wanachofahamu kuhusu kulipuliwa kwa bomu hilo.
Juzi, Mbowe akiwa na Lema, alisema wana ushahidi wa picha za video zikiwahusisha polisi na kulipuliwa kwa bomu hilo katika Uwanja wa Soweto wakati wa mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani kwa Chadema, Jumamosi iliyopita.

Mkwara wa Chagonja
Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kupeleka ushahidi ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo.
“Tunamtaka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa askari wetu kuhusika na tukio la bomu pale Soweto. Wasipofanya hivyo tutatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo kwani yeyote mwenye ushahidi unaoweza kusaidia upelelezi wa kosa la jinai akikataa kuuwasilisha kwa vyombo husika anaweza kuchukuliwa hatua,” alisema.

Nape naye kuhojiwa
Kwa upande wake, polisi limesema litamhoji Nape ambaye alikaririwa jana akidai kuwa Chadema ndiyo waliohusika na urushaji wa bomu kwenye mkutano wao baada ya kuhisi kushindwa kwenye uchaguzi wa kata nne za Jiji la Arusha.
Kamishna Chagonja alisema watamhoji ili kusaidia kazi yao ya upelelezi. Nape aliihusisha Chadema kwa kauli alizoita za kutishia amani zilizowahi kutolewa siku za nyuma kabla ya uchaguzi wa kata za Arusha.

Watatu wakamatwa
Kamishna Chagonja alisema watu watatu wamekamatwa wakihusishwa na tukio la...

SAIDA KAROLI AKIONGEA KUHUSU KUZUSHIWA KUWA AMEKUFA, MSIKILIZE HAPA

SAIDA KAROLI