Pages

OMMY DIMPOZ AMTUSI MAREHEM MANGWAIR

 Mangwea ‘NgwairMwanamuziki chipukizi, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amedhihirisha kuwa ana kiwango cha juu sana cha dharau kwa kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele za haki.
Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Utamaduni wetu Tanzania na kama ilivyo kwa mafundisho ya dini kupitia vitabu vinne vitakatifu, Torati, Zaburi, Injili na Kuran, fundisho ni kwamba mja aliyepoteza maisha hakashifiwi, hasimangwi, hahukumiwi, isipokuwa huhifadhiwa kwa heshima kisha kuombewa salama na amani mbele ya Mungu.
Ommy Dimpoz, kijana ambaye ni mwaka jana tu alikuwa ‘anawanga’ huku na huko mikono nyuma akiomba msaada wa kimuziki, hivi sasa anajiona ameota meno ya juu kuweza kung’ata, kiburi hicho kimempa uthubutu wa kumtusi Mfalme wa Freestyle, marehemu Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’.
Thamani ya Ngwair na namna alivyozikwa kwa heshima hajaviona, badala yake akatusi kuwa Mfalme wa Freestyle alikufa maskini ndiyo maana mazishi yake yalikuwa ya kuungaunga michango ya wadau.

 Marehemu Albert Kenneth Mangwea Kifo cha Ngwair, kilivuta makundi mbalimbali kushiriki kwa hali na mali kuchangia na kumzika, taifa lilizizima mkoa kwa mkoa, mguso huo wa kitaifa aliokuwa nao mwanamuziki huyo, Ommy hakuuona, isipokuwa akanena: “Sitaki kufa maskini kama Ngwair.”

Akimweleza mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, Juni 10 (Jumatatu) na Juni 11, mwaka huu (Jumanne), Ommy alidhihaki hata ushiriki wa wanamuziki waliosimamisha shughuli zao kwa muda kisha kuungana na kushikamana kuhakikisha Ngwair anazikwa kwa heshima.
“Sitaki nikifa yatokee kama ya Ngwair, amekufa Afrika Kusini, hata kuusafirisha mwili kuuleta Tanzania imebidi mpaka watu wachangie, ile ni aibu sana,” alisema Ommy kwa dharau.
Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), mwandishi wetu alimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?
Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.

MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.
OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?
OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?
OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.
MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?
OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.
MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi’ za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.

MANENO YA KASHFA MLIMANI CITY
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: “Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa.”

Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
“Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair,” alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.
Chanzo. Le Mutuz

MTOTO WA SIKU NNE AKAA SIKU SITA SHIMONI

Bahati Upendo
Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe alipowekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa kwenye shimo...
Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipookotwa na wasamaria wema...
Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama Salimini .
Yeyote Mwenye nafasi ya kumsaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali.

GARI INAUZWA BEI POA

Daihatsu Daihatsu Daihatsu
Make:Daihatsu
Model:VS100P
Body type:Station Wagon
Colour:Silver
Year:2001
CC:659
Fuel:Petrol
Price: 7.8 Milion
Contact :+255 754 940992
Tanzania

PICHA za KWENYE MSIBA NYUMBANI KWA MAREHEMU LANGA


Hapa ndipo alipokuwa analelewa Langa kwa wazazi wake baba na mama na hizi picha ni wasanii wakifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari kutoka Star TV na EATV. Kalapina na Kala JeremiahMSIBAMSIBA
 Kalapna
 Marehemu Langa  
Ni Nyumban kwa Marehemu Langa hapa Kalapna akmuongelea Mwana hiphop Mwenzie Marehem Langa,Pina amesema ameumia sana kwani Langa alkuwa Mwanahiphop aliekuwa akifata Misingi ya Hiphop.RIP Langa

SOMA DONDOO ZA BAJETI YA TAIFA 2013/14 HAPA (Trilioni 18.2)

BAJETI YA TAIFA
1. Bajeti nzima ni Trilioni 18.2; ambapo Trilioni 11.1 sawa na 61% zitakusanywa kutoka kwenye mapato ya ndani (GBS itakuwa ni Trilioni 1.16, pia wafadhili watatoa Trilioni 2.7 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo)
2. Trilioni 5.7 zitatumika kwenye shughuli za maendeleo (ambapo Trilioni 2.7 zitatoka kwa wahisani; na Trilioni 3 zitatoka kwenye vyanzo vya ndani)
3. Matumizi ya kawaida ni Trilioni 12.5 (Trilioni 4.8 zitatumika kulipa mishahara na stahili za wafanyakazi; mfuko mkuu wa serikali umetengewa Trilioni 3.3 (kupunguza deni la Taifa) na matumizi mengineyo yatachukua Trilioni 4.5
4. Vipaumbele vya bajeti ni: Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Rasilimali-watu, Utalii na Huduma za jamii
5. Deni la Taifa lafikia Trilioni 21
6. Kodi ya sigara, soda na bia imeongezeka kwa asilimia 10
7. Nia ya serikali ni kukuza pato la Taifa kufikia 7.2% mwakani (toka 7.0% mwaka huu); pia kudhibiti mfumuko wa bei toka 8.3% sasa na kufikia 6% mwakani
8. Kodi ya mishahara(PAYE) kupungua kwa asilimia 1; toka 14% na kuwa 13%
9. Kodi ya Mafunzo (Skill Development Levy) imepungua toka asilimia 6 mpaka 5
10. Watumiaji wa simu kutozwa 14.5% (ambapo asilimia 2.5 ya pesa hizo zitagharimia elimu)
11. Kutakuwepo na tozo mpya ya mafuta ya petrol y ash 50 kwa lita kugharimia umeme vijijini
12. 10% itatozwa kama kodi kwenye commission ya kusafirisha fedha kwa njia ya simu za mikononi
13. Ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi? KIMYA
14. Waziri hakuzungumza kuhusu bajeti ya elimu itakuwa kiasi gani (alijikita zaidi kwenye maeneo yaliyofanyiwa marekebisho baada ya bajeti za wizara mbalimbali kujadiliwa-la orodha ya vipaumbele aliyoitoa..hivyo-itakuwa inafanana na kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti ya elimu cha shilingi bilioni 689.7 (bilioni 98.7 ni matumizi ya kawaida ya idara; bilioni 72.6 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo; na bilioni 518.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya taasisi (zikiwemo bilioni 306 za mikopo ya elimu ya juu).

Football Match Stopped by Armed Police Hunting Criminal Player


A fourth division fixture in Romania between Chisoda and Sannicolaul Mare was momentarily suspended after riot police carried out an armed search for a player suspected of multiple crimes.
As you can see from the above footage - taken by a spectator at the game on his mobile phone - armed police stormed the pitch during the game and forcing all of the participants and substitutes onto the ground, hands on their heads.
After checking every last footballer to see if one of them was their man - Chisoda's Sorin Udrea - the police looked set to give up and continue their manhunt elsewhere.
But it was not long before Udrea's cover was blown: the wanted footballer was hiding out in the stands among fans, and once found he was arrested on multiple counts of extortion, robbery and smuggling.

Baada Ya Malalamiko Kuhusu Tuzo Yake “Wimbo Bora Wa Hip-Hop” Ney Wa Mitego Aongea… Msikie Hapa

 Hip-Hop
Kupitia 255 segment ya kipindi cha XXL cha CloudsFM, Ney Wa Mitego alihojiwa na Dee Andy kupitia malalamiko yaliyopo baada ya msanii huyo kuchukua Tuzo ya Wimbo Bora Wa Hip-Hop.
Ney alifunguka na kuwataka wasanii waache malalamiko ya hovyo na badala yake wapige kazi … Msikilize Ney hapa …

RATIBA YA MAZISHI YA LANGA KILEO

LANGA Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

Derecho Strikes Midwest: Wall of Wind Targets East Coast Next

Torrential rains have drenched New York as a storm that flattened buildings, toppled trees and downed power lines in the MidWest promised to inflict more wild weather overnight, as it turns into a fierce nor'easter.
Meteorologists say the non-tropical storm - rare for this time of year - will batter areas from northern and coastal New Jersey to eastern Massachusetts with heavy rain, gusty winds and flooding into Friday morning.
As a result of the violent weather, there are likely to be significant travel delays and power outages in the New England region before the storm rolls off to the northeast on Friday.
Tens of thousands of families were left without power in Ohio, Illinois and northwest Indiana on Wednesday night in the storm which brought with it a series of mini tornadoes.