Pages

AMRI KIEMBA AMESAINI SIMBA MKATABA WA MIAKA 2 KWA DAU LA SH. M 50

Amri Kiemba
Kaka wa mchezaji wa Simba, Amri Kiemba (wa pili kushoto) akisaini kwa niaba ya mdogo wake kuchukua fedha za usajili kwa mkataba wa miaka miwili jumla ya Sh. Milioni 50, baada ya kiungo huyo kukubali kumwaga wino Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Klabu hiyo ya Simba SC wakati wa zoezi hilo lililofanyika leo mchana. Wa pili (kulia) ni Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang'are 'Kinesi' na Damian Manembe (kulia) na Salum Pamba, Wajumbe wa Kamati ya Utendaji. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry
Amri KiembaAmri Kiemba Pichani, ambaye alikuwa gumzo kila kukicha hukua akielezewa kuwa tayari alikuwa ameshamwaga wino kwa mahasimu wa Simba Yanga na kupewa mkataba wa miaka miwili na kitita cha Sh. milioni 38, huku akiahidiwa kulipwa mshahara wa Sh. 90,000 kwa mwezi ambao ulikuwa umezidi ule anaopokea kwa wekundu hao.
Kwa zoezi hilo la kumsainisha Kiungo huyo sasa Klabu ya Simba imekata mzizi wa fitina na kuzima maneno yote yaliyokuwa yameenea mtaani kuwa Kiemba alikuwa katika harakati za kusajiliwa na Yanga.
Lakini pia Inawezekana Wekundu hao wameshtukia dili baada ya kusikia mchezaji huyo amekuwa 'LULU' huko nchini Morocco na kuonekana kuvivutia baadhi ya Vilabu vilivyoonyesha nia ya kumhitaji kiungo huo, hivyo inawezekana Simba wamecheza Karata ya Dume ili kuwahi kitita cha kumuuza Kiungo huyo iwapo waarabu hao watafika bei. ''Kila la kheri Kiemba na huu ndiyo msimu wa mavuno''.....

Kimbembe

Kimbembe

Vodacom Yawekeza Trilioni 1.3 Nchini Tanzania

Kiasi cha shilingi bilioni 190 zimekusanywa kama makato ya kodi toka kwa wateja na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania mwaka jana na kulipwa serikalini huku pia vodacom yenyewe ambayo tayari imewekeza shilingi trilioni 1.3 hapa nchini ikilipa kodi ya shilingi bilioni 36.5 kwa kipindi hicho

In The Congo - Rhyme Like A Girl Ft Nasambu (Video)

"In The Congo", is the first major musical collaborative effort of its kind to raise awareness on what some are calling the third World War. Calling for a new wave of Green Technology and Fair Trade Electronics. This music video highlights the main cause of rape and genocide in the Eastern Congo region as a desperate scramble for the minerals that power every cell phone and laptop. Produced and directed by Tanzanian Hip Hop guru, Zavara Mponjika, the video features US Hip Hop Ambassador Toni Blackman's collective, Rhyme Like a Girl, alongside California based Kenyan Afro-Soul artist and founder of Activate Afrika, Nasambu. In times when the mainstream media rarely highlights issues of consequence, leaving many people in a state of ignorance, these artists have joined together across time, space, and geographical borders to express their views on this global war and human rights catastrophe that is urgently.

LWAKATARE WA CHADEMA AMEPATA DHAMANA

LWAKATARE WA CHADEMA
Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akiingia katika chumba cha ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kupata dhamana katika kesi yake inayomkabili ya kula njama ya kutaka kumzuru kwa sumu Mhariri wa gazeti la wananchi.Wilfred Lwakatare
Wilfred Lwakatare akiwa na furaha pamoja na wakili wake baada kupata dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mshtakiwa wa pili katika kesi inayomkali akiwa amerudi rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
Wilfred Lwakatare
Wakili wa Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara akiwa katika picha ya pamoja na mteja wake Wilfred Lwakatare pamoja na wadhamini wake muda mfupi baada ya.....

CCM Yaipeleka Rasimu ya Katiba Mpya kwa Wanachama Wake.

 Katiba Mpya
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauy akizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika kikao cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya. Kamati Kuu imeipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa:
Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.
Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.
CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.
Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.

"UJIO WA OBAMA NCHINI SI KWAAJILI YA RASILIMALI ZA WATANZANIA" Balozi wa Marekani nchini Tanzania

Alfonso Lenhard
Akiongea na waandishi wa habari jana, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Alfonso Lenhard amesema ziara ya mwezi ujao ya Rais wa Taifa la Marekani, Barack Obama nchini Tanzania haina ajenda ya siri: "kuna maswali mengi naulizwa kwa nini Rais Obama amechagua kuzuru Tanzania? Ni kweli Rais wetu anakuja malengo ya ziara yake yatajikita katika mambo ambayo ni... malengo ya Marekani kwa Afrika, ambayo ni uhusiano wa kiuchumi, kuimarisha demokrasia na kuwekeza katika kujenga kizazi kijacho cha uongozi."

Akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari kuhusu uhusiano wa ujio wa Rais Obama na rasilimali za Tanzania, Balozi Lenhardt alisema: "Ni kweli Obama atakuja Tanzania. Lakini .....

The Team Sehemu ya Kumi na Tatu ( Episode 13 )


Ben Pol - JIKUBALI (Official Music Video)