Pages

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BESTA (ENGLISH MEDIUM) WAONDOLEWA SHULENI BAADA YA SHULE KUUZWA KWA AMRI YA MAHAKAMA MBEYA

Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya
Hii ndiyo Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya.
Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya
Vibarua waliopewa jukumu la kuhamisha mizigo shuleni hapo
Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya
Viti vikiwa vimetolewa eneo la shule ya Msingi Besta
ENGLISH MEDIUM
Gari la mizigo likichukua mizigo kuelekea...

SHIT HAPPENS! The Jacuzzi Scandal

Hatimaye Awamu ya Kwanza ya Rasimu ya Katiba Imezinduliwa Jijini DSM (Video)

Awamu ya kwanza ya rasimu ya katiba imezinduliwa jijini Dar es Salaam ambapo imetoa ufafanuzi wa mambo kadhaa wa kadhaa ikiwemo madaraka ya rais, muundo wa muungano huku ikibainisha wazi kuwa kuwepo na mgombea huru wa nafasi ya urais.

TAARIFA KUTOKA JWTZ KUHUSU UKWELI WA MESEJI KWENYE SIMU


 JWTZ 

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA03 Juni, 2013
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limepata ujumbe kupitia simu za mkononi ambao umesambazwa kwa wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa unatolewa na JWTZ. Ujumbe huo wa simu ya mkononi unasema ‘Habari zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una shaka nacho, kunabomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’ Piga namba 0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.
JWTZ linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo haujatolewa na JWTZ. JWTZ haliwezi likatumia mfumo huo wa SMS kuwapa wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ hutangaza kupitia vyombo rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.

Pili, bomu la tani 100 ni zito mno, halijawahi kutengenezwa duniani. Na kama lipo, haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia ndege au Mzinga?. Lakini pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani kote na wala hakuna ndege yenye uwezo huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama hilo(Chupa ya Chai).

Tatu, habari hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia au fikra za kawaida. Tunawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za hatari,lazima lingewajulisha wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa simu za mkononi.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Klabu ya Simba Yajiondoa Mashindano ya CECAFA

Nicholas Musonye
Klabu ya Simba kutoka Tanzania, imetangaza kuwa haitashiriki katika michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA, ikiwa itaandaliwa katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mjadala ulioibuka katika bunge la Tanzania baada ya waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benard Membe kuhoji hali ya Usalama katika eneo hilo. Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Adne Rage, amesema uongozi wa CECAFA ni sharti ubadilishe mahala pa fainali hizo la sivyo wao hawatashiriki. ''Hatuwezi kwenda Darfu kuvalia mavazi yasiyopenya risasi'' Alisema Bwana Rage. ''Ni wazi kuwa hali ya usalama katika eneo hilo sio nzuri kama ilivyothibitishwa na serikali'' Aliongeza mwenyekiti huyo wa Simba.
Membe aliliambia bunge la Tanzania kuwa alishangazwa sana na uamuzi wa kuandaa fainali hizo katika eneo la Darfur ambalo limekubwa na mapigano ya mara kwa mara.
Membe amesema serikali ya Tanzania, inachunguza hali ilivyo na kuwa watachukua uamuzi muafaka kuhusiana na suala hilo. ''Hatuwezi kuwatuma vijana wetu katika eneo ambalo hatuna hakikisho la Usalama'' Alisema Membe.
Mabingwa watetezi Yanga, vile vile kutoka Tanzania ambao walikuwa wameonyesha nia ya kushiriki katika fainali hizo za Darfur, pia nao wanasema watafuata ushauri kutoka kwa serikali.
Katibu mkuu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Tanzania TFF, Generali Anfetile Osiah, amesema wao wamehakikishiwa usalama na eneo watakalopiga kambi wakati wa mashindano hayo.
Endapo timu hizo mbili kutoka Tanzania zitajiondoa kutoka kwa fainali hizo, itakuwa pigo kubwa kwa waandalizi wa mashindano hayo. Timu mbili kubwa nchini Sudan Al Hilal na Al Merreikh tayari zimethibitisha kuwa hazitashiriki kutokana na hofu sa kiusalama.
Katibu mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amekariri kuwa eneo hilo la Darfur ni salama kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
BBC

Kilio Cha Mama Nziula Aliyepigania Uhuru (Video)

Huku Kenya ikiadhimisha miaka hamsini ya Madaraka, baadhi ya waliojitolea kupigania uhuru wa nchi hii wanaishi kwa machungu kama mwanamke mmoja katika Kaunti ya Machakos ambaye katika uzee wake anataka kulipwa fidia kwa yale aliyoyapitia.

WATANZANIA WA SOUTH AFRICA WAKIAGA MWILI WA ALBERT MANGWEA


 ALBERT MANGWEA
Muda huu wa saa kumi na Mbili kwa saa za Afrika mashariki kwa saa za South Africa ni saa kumi na Moja jioni.....tukiwa bado tupo kwenye majonzi makubwa yakupotelewa na ndugu yetu Albert Mangweha.....Baada ya ratiba kupangika watanzania waishio nchini South Africa wamepata nafasi ya kuaga mwili wa Albert Mangweha kuelekea katika safari ya mwisho...wakiongozwa na Msanii Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru, Kinjeketile wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini South Africa
 South Africa
 ALBERT MANGWEA

3rd Anniversary of Vijimambo Blog


Anniversary of Vijimambo Blog

Langa - Rafiki wa kweli (Official Video)

Video ya Meli Mv. Arafat Ikiteketea kwa Moto Bandarini Tanga

Meli ya mizigo ''Mv Arafat'' inayofanya safari zake kupeleka shehena ya mizigo katika nchi jirani ya Kenya , Zanzibar na Mtwara Imeteketea kwa moto katika bandari ya Tanga kwa kile kinachodaiwa kuwa hitilafu ya umeme.