Pages

Linex Ft Wyre - Riziki Yangu (Audio)

Linex Ft wyre - Riziki Yangu

MABAKI YA MWANAMKE YAMEKUTWA JIRANI NA MAGEREZA

Magereza,  Miyomboni Kitanzini MABAKI ya mwili wa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina lake halikufahamika, yamekutwa eneo la Magereza, Kata ya Miyomboni Kitanzini, Manispaa ya Iringa.
Mabaki hayo yalikutwa majira ya saa 6:00 mchana, juzikati yakiwa yamesambaratika kutokana na kuoza.
Walioyakuta ni maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa wakikata miti kwa ajili ya kuni.
Wakizungumza na Amani, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo inaonekana siku ya kifo chake alikuwa amevaa suruali nyeusi, kilemba cha kitenge chenye madoa mekundu, njano, meusi na meupe pamoja na skafu ya rangi nyeupe na nyeusi.
Mashuhuda hao walidai kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha kwa zaidi ya wiki mbili nyuma kutokana na mabaki hayo kuharibika kupita kiasi na kukauka

Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo yalionesha utata kwa kuwa hata polisi waliofika eneo la tukio, walikiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote ya mtu kupotea na kwamba inawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake au alikuwa akitoka hospitali ambayo ipo jirani na eneo hilo.
Mabaki ya mwili huo yalichukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika Chumba cha Maiti cha Nina Marwaha cha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa.
GPL

Best of 2000s Bongo Flava by Dj KayCee (Audio)

Best Bongo Flava by Dj KayCee

Usalama wa Waandishi wa Habari Shakani

Waandishi wa habari Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwa waangalifu na kuchukua hatua kwa kujilinda dhidi ya watu wasiowatakia mema ambao wanaweza kuwashambulia kutokana na kazi zao za kila siku wanazozifanya ndani ya jamii. Kadhalika, imeelezwa kuwa idadi kubwa ya waandishi wa habari ni waadilifu, ingawa wapo wachache wasio na uadilifu ambao wanatumiwa na watu kuwaangamiza wenzao. Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nchini (MOAT), Dk. Reginald Mengi, alipofungua mkutano wa siku moja uliowashirikisha watetezi wa haki za binadamu, walimiki wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari nchini.
Dk. Mengi alisema waandishi wa habari wanakumbana na matatizo mengi kupitia kazi wanazozifanya kila siku katika jamii na kuongeza kuwa wanatakiwa kujilinda wao wenyewe na kuachana na tabia zinazoweza kuwatumbukiza kwenye hatari.
Alitaja baadhi ya maeneo ambayo yanaweza kumtumbukiza katika hatari mwaandishi kuwa ni...

Wanafunzi 15 Mbaroni kwa Kuchoma Moto Bweni

Moto Bweni
WANAFUNZI 15 wa Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe, mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchoma moto bweni wakipinga hatua ya wanafunzi wenzao kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea Mei 14, mwaka huu saa 2.00 usiku.
Kamanda Athuman alisema kuwa wanafunzi hao baada ya  kuona wenzao watatu wamesimamishwa masomo walianza kufanya vurugu usiku na kuanza kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Kamanda Athuman aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu shuleni hapo kuwa ni, Joseph Robert (18), Mwita Chacha na Daniel David (18).
“Hawa wanafunzi watatu waliosimamishwa masomo walihamasisha wenzao kuunga mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kuchoma bweni hilo,”alisema Kamanda Athuman.

Alisema bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi ambao hawakuwa tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani shuleni hapo. Aidha Kamanda Athuman alisema wanafunzi 15 wanashikiliwa na polisi wakiwemo vinara wa fujo hizo.
Kuhusu mali zilizoharibiwa, Kamanda huyo alisema thamani halisi ya uharibifu uliotokea bado haijajulikana. Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake watatue matatizo kwa njia ya mazungumzo kwa kufuata mamlaka husika.  
MAJIRA

Unga wa Ngano Zaidi ya Tani 700 Umekwama Bandarini Zanzibar (Video)

Unga wa ngano tani zaidi ya 700 umekwama bandarini Zanzibar baada ya kuharibika na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hadi sasa kushindwa kupata mahali pa kuangamiza hali hiyo imesababisha kuomba msaada wa kitalaamu kutoka serikali ya muungano.

Usiogope Family - Habari ya mjini {Official HD Video}

SIMBA SPORTS CLUB YAANDAA MPANGO MKAKATI

Simba Sports Club Simba Sports Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafahamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (Strategic Plan).
Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-
1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.

Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013 Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-
1. Joseph Itang’are
2. Swedy Mkwabi
3. Francis Waya
4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Ngahyoma
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mutahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga

Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.

Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.

Mpango mkakati huo utakuwa tayari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.
Imetolewa na
Evodius Mtawala
Katibu Mkuu,
Simba Sports Club.

Father's Advice To His Young Daughter (Video)