Pages

Wanafunzi 15 Mbaroni kwa Kuchoma Moto Bweni

Moto Bweni
WANAFUNZI 15 wa Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe, mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kosa la kuchoma moto bweni wakipinga hatua ya wanafunzi wenzao kusimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea Mei 14, mwaka huu saa 2.00 usiku.
Kamanda Athuman alisema kuwa wanafunzi hao baada ya  kuona wenzao watatu wamesimamishwa masomo walianza kufanya vurugu usiku na kuanza kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Kamanda Athuman aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu shuleni hapo kuwa ni, Joseph Robert (18), Mwita Chacha na Daniel David (18).
“Hawa wanafunzi watatu waliosimamishwa masomo walihamasisha wenzao kuunga mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kuchoma bweni hilo,”alisema Kamanda Athuman.

Alisema bweni lililochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi ambao hawakuwa tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani shuleni hapo. Aidha Kamanda Athuman alisema wanafunzi 15 wanashikiliwa na polisi wakiwemo vinara wa fujo hizo.
Kuhusu mali zilizoharibiwa, Kamanda huyo alisema thamani halisi ya uharibifu uliotokea bado haijajulikana. Kamanda Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake watatue matatizo kwa njia ya mazungumzo kwa kufuata mamlaka husika.  
MAJIRA

Unga wa Ngano Zaidi ya Tani 700 Umekwama Bandarini Zanzibar (Video)

Unga wa ngano tani zaidi ya 700 umekwama bandarini Zanzibar baada ya kuharibika na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hadi sasa kushindwa kupata mahali pa kuangamiza hali hiyo imesababisha kuomba msaada wa kitalaamu kutoka serikali ya muungano.

Usiogope Family - Habari ya mjini {Official HD Video}

SIMBA SPORTS CLUB YAANDAA MPANGO MKAKATI

Simba Sports Club Simba Sports Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafahamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (Strategic Plan).
Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-
1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.

Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013 Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-
1. Joseph Itang’are
2. Swedy Mkwabi
3. Francis Waya
4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Ngahyoma
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mutahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga

Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.

Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.

Mpango mkakati huo utakuwa tayari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.
Imetolewa na
Evodius Mtawala
Katibu Mkuu,
Simba Sports Club.

Father's Advice To His Young Daughter (Video)

SIKILIZA KWA UMAKINI WARAKA WA WEUSI KUHUSU TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KANISA OLASITY ARUSHA

WARAKA WA WEUSI

Was Rapper Eminem Stabbed 4 Times In NYC??

Eminem Stabbed Don't click on links to purporting to offer surveillance video of Eminem being stabbed four times by a crazed fan. The story is false, the video doesn't exist, and the links actually redirect users to scam websites promising "free prizes" (which don't exist either) for completing an online survey.
Worse yet, users who comply with instructions to share said links via social media will suck their Facebook friends and Twitter followers into the scam as well. Don't do it!
An identical scam claiming Justin Bieber was the victim of a stabbing attack made the rounds in 2011. Even the photo was the same.
Tips & tricks:
How to Spot a Facebook Survey Scam

Watch Everything Wrong With Jurassic Park In 3 Minutes Or Less

VODACOM NA SAMSUNG WAZINDUA Samsung Galaxy S4.

Samsung Tanzania Meneja wa kampuni ya simu za Samsung nchini Kishor Kumar akiwaonyesha simu aina ya Samsung Galaxy S4 iliyosheheni teknolojia mbalimbali za kisasa ,Meneja uendeshaji wa maduka ya Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi (kulia) Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung Sylvester Manyar na Meneja Masoko wa Vodacom Ibrahim Kingozi (kushoto) wakati wa uzinduzi wa simu hizo mpya ambapo wateja watakaonunua aina ya simu hizo watapata huduma ya bure ya Intaneti ya (5GB) kwa muda wa siku 30 ikiwa sambamba na waranti ya mwaka mmoja wa matengezo uzinduzi huo.ulifanyika katika duka la Vodacom lililopo eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Samsung Tanzania Country Manager, Kishor Kumar, illustrates the features of the new Samsung Galaxy S4 to Vodacom Tanzania Manager for Franchise and Operations, Elihuruma Ngowi (right), Samsung Tanzania Manager for Sales and Distribution, Sylvester Manyar and Vodacom Tanzania Post Paid and Enterprise Acquisition Manager, Ibrahim Kiongozi (left) during the launch of the device in Oysterbay, Dar es Salaam. Upon purchase of the Samsung Galaxy S4, customers will get free 5GB internet for 30 days when activated with Vodacom SIM card. The device also comes with 24 months of warranty that will cover any device feature malfunctions.
Ibrahim KingoziMeneja Uendeshaji wa Maduka ya Vodacom Tanzania,Bw.Elihuruma Ngowi,akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu za mkononi za Samsung Galax S4 ambazo zitapatikana kwenye maduka ya Vodacom,wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa kampuni ya simu za Samsung nchini Kishor Kumar na kushoto ni Afisa Masoko wa Vodacom Ibrahim Kingozi. wateja watakaonunua aina ya simu hizo watapata huduma ya bure ya Intaneti ya (5GB) kwa muda wa siku 30 ikiwa sambamba na waranti ya mwaka mmoja wa matengezo uzinduzi huo.ulifanyika katika duka la Vodacom lililopo eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam.

BABA JONII KUTAMBULISHA BOONGE LA MIXTAPE KESHO KWA BIRTHDAY YAKE 16TH MAY

Adam Mchomvu a.k.a baba jonii Radio presenter clouds fm mwenye crown ya best presenter, anatarajia kutoa mixtape yenye ngoma kumi na nane alioshirikiana na wasanii mbali mbali kama Jose Mtambo, Banana Zorro, Illimatix, Cliff mitindo, G.nako, Niki wa 2, Babuu wa kitaa, TID, na wasanii wengine wengi kama zawadi kwa mashabiki wake ibaki kama kumbukumbu kwa kile anachokifanya hewani (on air) ... mixtape itaingia kitaani soon baada kupreview ngoma hizo ndani ya double XL (XXL) kuanzia saa tisa alasiri kwa hot 3 @ 3 ..... big up baba la baba!
BABAJONII MIXTAPE VOL 1