Tweets za Mchezaji wa Chelsea Adam Nditi Akiiponda Show ya Diamond Uingereza
Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwa wiki kadhaa sasa amekuwa nchini Uingereza akifanya maonyesho yake ya kimuziki, usiku wa jana jijini London alikuwa akifanya show na mmoja ya wahudhuriaji alikuwa mchezaji wa kikosi cha pili cha Chelsea Adam Nditi ambaye ni mzaliwa wa Tanzania Visiwani. Kwa mujibu wa tweets za Adam Nditi amesema hakupenda hata kidogo kitendo alichofanya Diamond katika show yake kwa kufanya show mbovu ambayo ilichelewa kuanza baada ya msanii kuingia ukumbini asubuhi badala muda halisi uliopangwa.
Dramatic footage: Vintage Stunt Plane Crashes Outside Madrid at Aerobatics Show
An air show featuring aerial acrobatics and vintage aircraft has ended
in tragedy near Madrid as a stunt plane crashed into buildings. A pilot
sustained severe injuries and reportedly died in hospital
Pigo Jingine kwa Babu Seya na Papii Kocha!!
MAMA mzazi wa mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ aitwaye Bernadeta, amefariki dunia ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni pigo lingine kwa mwanamuziki huyo na mwanaye, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wanaotumikia kifungo cha maisha jela.
Kifo hicho kimetokea wakati Babu Seya na Papii Kocha wakiendelea kutumikia kifungo hicho katika Gereza la Ukonga, Dar.
Kwa mujibu wa mtoto wa Babu Seya, Nguza Mbangu, mama huyo alifariki ghafla akiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kusumbuliwa na presha.
Kwa mujibu wa Mbangu, mama wa Babu Seya ambaye ni bibi yake alianza kusumbuliwa na presha baada ya mwanaye na wajukuu zake kutiwa hatiani kwa ubakaji wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza, Dar hadi ugonjwa huo ulipomuondoa ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbangu alisema kuwa wameumizwa na kifo hicho kwa kuwa marehemu alikuwa tegemeo kubwa kwa ushauri na kifo chake kimezidisha uchungu kwa familia yao.
Mbangu aliongeza kuwa baba yake, Babu Seya na ndugu yake, Papii Kocha waliposikia taarifa hizo walilia kwa uchungu wakiwa gerezani.
Taarifa zaidi zinasema kuwa wanandugu waishio Dar walikutana Kimara, kwa ajili ya kumchagua mwakilishi wa kwenda Kongo kuwahi mazishi.
JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MTU MMOJA KUHUSIKA KATIKA MLIPUKO WA BOMU LEO ASUBUHI JIJINI ARUSHA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo.
JESHI la Polisi Mkoani Polisi Mkoa wa Arushalinamshikilia mtu mmoja ambaye anahusishwa na kutokea kwa mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki la St Joseph Olasiti Arusha leo asubuhi.
Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Papa kutoka Vatican akizindua Parokia hiyo mpya ya St Joseph Olasiti ya Jijini Arusha.Kama unavyoona katika picha ni kanisa katoliki, parokia mpya ya Olasisi jijini Arusha ilivyo baada ya kulipuliwa na bomu mapema leo.Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi huku msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine unaendelea.
JESHI la Polisi Mkoani Polisi Mkoa wa Arushalinamshikilia mtu mmoja ambaye anahusishwa na kutokea kwa mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki la St Joseph Olasiti Arusha leo asubuhi.
Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Papa kutoka Vatican akizindua Parokia hiyo mpya ya St Joseph Olasiti ya Jijini Arusha.Kama unavyoona katika picha ni kanisa katoliki, parokia mpya ya Olasisi jijini Arusha ilivyo baada ya kulipuliwa na bomu mapema leo.Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi huku msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine unaendelea.
Waasi wa Kongo M23 Wametoa Vitisho Vikali kwa Tanzania Kupitia Twitter!!
Kuptia Tovuti ya kijamii ya Twitter Jeshi la waasi wa nchini DRC kimetuma ujumbe wa vitisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, kufuatia kauli aliyoitoa Bungeni leo kuhusu Tanzania kupeleka jeshi lake DRC kukabiliana na waasi hao.Ni hii ndio tweet yao
M23 Congo RDC @m23congordc 16h @ Bernard Membe tunasubiri majeshi yako Congo. Usidaganye bunge lako eti Tanzania inakuja zima moto,bali munakuja kuweka mafuta kwenye moto
MAJIBISHANO KATI YA BERNARD MEMBE NA ZITTO KABWE KUHUSIANA NA VITISHO HIVYO:
Subscribe to:
Posts (Atom)



