Pages

Baadhi ya Wagombea wa Tawi la CCM DMV Wajitoa Kwenye Uchaguzi

CCM DMV
Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika baadhi ya wagombea wamelazimika kujitoa majina yao kwenye uchaguzi huo uliotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi Machi 16, 2013 saa tisa kamili jioni katika anuani hii: 500 Sligo Avenue, Silver Spring MD 20910.

Wagombea waliojitoa ni..
Ndugu Mrisho Mzese – Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa tawi
Ndugu Al Amin Hassan Chande Othman – Mgombea - Mwenyekiti wa vijana
Ndugu Steven Ngosha – Mgombea nafasi ya katibu mwenezi na itikadi
Ndugu Warashi Khamisi - Mgombea nafasi ya halmashauri ya kuu ya tawi
Ndugu Fadhil Londa - Mgombea nafasi ya katibu wa vijana
Ndugu Ismail Abubakar Mwilima - Mgombea nafasi ya halmashauri ya kuu ya tawi

Watoto Wawili Morogoro Wafanyiwa Ukatili na Baba Yao...

Watoto wawili wa darasa la tatu na darasa la kwanza katika shule ya msingi Msamvu B ya mjini Morogoro wamefanyiwa ukatili kwa kupigwa kisha kuchomwa midomo kwa mkaa wa moto na baba yao mzazi baada ya kuwatuhumu kula Karanga.

Lady Jay Dee ft Proffesor Jay- Joto Hasira (Video)

Punguzo Maalum Msimu wa Pasaka na Sabasaba

Punguzo maalum kwa wateja walio na matangazo ya aina yoyote na ukubwa wa saiz yoyote ikiwa ni pamoja kama unakodisha au unauza Shamba,Nyumba,Gari,Duka,Saluni,Ofisi,Kiwanda,Kampuni na Kadhalika.
    darslam@rocketmail.com
  •      Pia ni fursa kwako kua Sponsor wetu kwa matangazo ya muda mrefu. Kumbuka mtandao wetu ni maarufu unatembelewa na watu wote ulimwenguni kutokana na mfumo wetu wa usambazaji wa habari ktk tovuti zetu nyingine pia mitandao ya kijamii
 ..Hii ni nafasi yako. Wahi sasa..!! 
 Bei ni nafuu sana kwa maelewano usisite kutuandikia Barua pepe kupitia darslam@rocketmail.com
Pia tunapokea habari mbalimbali.

Dozens of Drug Users Rush to Dealer's Car 'Like Children to an IceCream Van' Caught on CCTV Camera

This is the terrifying moment a drug dealer parked a car just yards from a children's playground and attracted a running crowd of 30 drug users who surrounded it like children on an ice cream van.
The footage released by West Midlands Police today shows the addicts racing after a drug dealer's car to get their fix seconds after he pulls into a street at 8:30am in Bordesley Green, Birmingham.
Police released the footage taken from a nearby CCTV camera - which will be shown on BBC1 series Caught Red Handed at 11am tomorrow - after jailing 29 men as part of their Operation No Deal.DCI Nick Walton said: 'You'd imagine drug transactions are carried out in a discrete manner, but the footage we obtained shows around 30 people rush towards the dealer's car in broad daylight.

Six-year-old Treasure Hunter Looking for Old Coins Finds First World War BOMB in his Grandpa’s Back Garden!

When six-year-old Oliver Hudd set out on his first outing with his new metal detector, he could never have imagined what he’d find. First World War BOMB
Oliver Hudd at the spot where he discovered the bomb which led to a police operation
For with just a few sweeps of the ground, the youngster had found an 8lb First World War bomb, sparking a police operation that saw a road cordoned off and a bomb disposal squad rushing to the scene.

Oliver was looking for Roman coins in his grandmother’s garden in Darenth Road, Dartford, with his father Jason when the drama began.
His mother Jenny Smith said: “Jason was using it for a bit without any luck, but as soon as Oliver touched it, it started beeping.“Jason dug down and felt the spade hit metal. He kept digging and hit it a good few times with the spade before seeing the pointed end and realising it looked like a bomb.”

The father-and-son treasure hunters raced into the house to tell the family.
“I thought Jason was just mucking about at first and I didn’t really believe it,” the mother-of-two added.
“I assumed it was probably some old baked bean tin, but Jason was adamant, so we phoned the police and when they arrived they rang for bomb disposal and closed the road.
“Oliver was so excited, running around the house shouting ‘we found a bomb’, but my three-year-old daughter Josie was scared and clinging to me.”

Bomb disposal units arrived from Dover at 5pm on Sunday and checked the bomb.
They quickly established it was a First World War bomb shell, but did not contain any explosives.
Miss Smith, 36, said: “We couldn’t believe it. The first time he goes out with his metal detector and finds that
“I think he reckons he’s always going to be finding exciting things now, a bomb in every field.”

Ile Picha ya Mbwa Mtu!

Mbwa Mtu

Wakamatwa kwa Kujihusisha na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu

Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan Jumla ya watu 12, 864, wakiwemo Watanzania na raia wa nje, wamekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwa kosa la kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Burhan, alisema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na kuimarishwa kwa mfumo wa usimamizi wa mipaka na udhibiti.

Alisema raia wa nje wanaofanyabiashara hiyo wanashirikiana na wenyeji, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi, hivyo ni vyema wakaacha tabia hiyo kwa kuweka uzalendo mbele.
Aidha, aliiomba serikali kuongeza vifaa vya kisasa kutokana na kuwepo kwa mbinu mpya na matumizi ya silaha na kuingizwa kwa silaha za kivita ambazo hutumika kuleta madhara kwa jamii.

Idara hiyo nchi nzima ina askari wasiozidi 3,000 huku mahitaji yakiwa ni 8,000, ambapo mpaka wa Tanzania ukiwa mkubwa unaopakana na nchi nyingi na..

Waganga Wajitokeza Kupambana na Jini Mahaba Linalo Mtesa Lady J'dee

Lady J'dee
WAGANGA wanaodai kuwa ni wataalam na wana uzoefu wa kupambana na jini mahaba linalomsumbua Mwanamuziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, wamejitokeza huku kila mmoja akiomba apewe nafasi ya kumtibu bure.

Mmoja wa wataalam hao aliyejitambulisha kwa jina la Jumaa wa Magomeni, Dar alisema: “Nimesoma habari kuhusu Jide, mimi naweza kumtibu tena bure, mpe namba yangu na mwambie anipigie.”

Mwingine ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema: “Nimesikitika sana kusoma hii habari ya huyu msanii Lady Jaydee, kwa kifupi naweza kumtibia free of charge.”

Kufuatia maombi ya wataalam hao, mwandishi wetu alijitahidi kumtafuta Jide bila mafanikio lakini juzikati kupitia kipindi chake cha Diary ya Lady Jaydee alionekana akipewa matibabu na ustaadhi mmoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda mambo yametulia.
CREDIT : GPL

Askari Aliyemwua kwa Risasi Mwalimu NMB Afukuzwa Kazi, Njombe

JESHI la Polisi mkoani Njombe, limemfukuza kazi askari wake PC Gelvas Joseph, mwenye namba 9790, kwa kosa la kufanya mauaji ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo, wilayani Makete.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Focus Malengo, alisema askari huyo alifanya kosa hilo Februari 27 mwaka huu kwa kumpiga risasi kifuani mwalimu Castory Sote (31), na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema askari huyo amefukuzwa kazi baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na kubaini alikiuka kanuni za utumishi ambapo hivi sasa anakabiliwa na mashtaka.

Aliongeza kuwa, kosa hilo alilifanya akiwa lindoni kwenye Benki ya NMB, tawi la Makete, ambapo marehemu alikuwa akichukua fedha katika mashine za benki hiyo.

Ilidaiwa kuwa, siku ya tukio hilo kulitokea malumbano kati ya mwalimu huyo na askari ambaye alimtuhumu marehemu kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu (helmet) kichwani. Hali hiyo ilizua mzozo kati yao baada ya marehemu kudai kuwa, polisi huyo si askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Imeandikwa na Mercy James, Njombe (via Majira)