
Kura zikihesabiwa kwenye kituo kilichopo Viwanja vya Kibera Social, jijini Nairobi baada ya wananchi wa Kenya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo jana. Picha na AFP
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Hadi majira haya ya saa 6.45 usiku wa kuamkia leo, Uhuru ambaye ni mgombea wa TNA alikuwa amepata kura 744,648 sawa na asilimia 56.1 wakati Raila ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 527, 780 sawa na asilimia 39.7.
Matokeo hayo ni kutoka katika vituo zaidi ya 5000 kati ya...
