Pages

Mwigizaji Lulu Kuachiwa kwa Dhamana Kesho Endapo Milioni 20 Itapatikana

mwigizaji Lulu
Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho january 25 2013.
Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano january 23 lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.
Chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.
Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba, endelea kuipitia millardayo.com kwa stori zaidi.

Kiwanda cha Mchina Chaua Wanne

Watu wanne wamefariki dunia katika mlipuko unaodaiwa kuwa ni wa bomu ambao umetokea kwenye kiwanda cha Hong Yu Steel cha kuyeyusha vyuma chakavu kilichopo Zogoani, katika mji wa Kibaha. Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema tukio hilo lilitokea juzi na kwamba ni mlipuko uliosababishwa na ajali ya kawaida. Alisema tayari mabaki ya vyuma vilivyolipuka yamepelekwa kwa wataalam wa milipuko kwa uchunguzi zaidi na kwamba taarifa zitatolewa baadaye.
Matei alisema mlipuko huo ulitokea wakati uyeyushaji wa vyuma ukiendelea na kwamba hiyo ni ajali ya kawaida.
“Hatuwezi kusema sasa kwamba ni bomu kwa sababu kwanza madhara yametokea tu kwa binadamu, bomu lingeweza kuvunja kuta na paa. Tunasubiri majibu ya wataalam ambao wanachunguza tukio hili,” alisema.
Alisema jana Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ilifanya ziara kiwandani hapo kujionea hali halisi na kujiridhisha kwamba kiwanda kisitishe shughuli zake kwa muda. Alisema tangu ajali hiyo ilipotokea juzi, menejimenti ya kiwanda ilitangaza kusimamisha shughuli zake kwa muda wa siku tatu na kwamba jana imekubaliwa kwamba kisimamishe uzalishaji kwa muda mrefu zaidi. Kamanda Matei alisema katika ajali hiyo, watu wanne walifariki ambao ni Watanzania watatu na raia mmoja kutoka China.

Kamanda Matei aliwataja waliofariki kuwa ni Kassim Mtulia (26), George Manumbu (25), Mwinjuma Hussein (25) wote Watanzania pamoja na Yu Huafing (28) raia wa China.
Alisema katika mlipuko huo watu kadhaa walijeruhiwa na kutibiwa Hospitali ya Tumbi.
Kati ya waliojeruhiwa, mmoja kati yao bado yuko hospitali na hali yake inaendelea vizuri huku wengine wakiwa wameruhusiwa.

Hili ni tukio la pili kutokea baada ya lile la Oktoba mwaka jana wakati mlipuko kama huo ulipotokea Mikocheni, jijini Dar es Salaam eneo la kwa Warioba karibu na Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha baada ya vijana waliokuwa wakiuza nyaya aina ya kopa kama vyuma chakavu kulipuka na kusababisha majeruhi kwa msichana mmoja na wengine kunusurika.
Habari na RESTUTA JAMES
SOURCE: THE GUARDIAN

DMX ft. Machine Gun Kelly - I Dont Dance

Check out the official video of 'I Don't Dance,' which features Machine Gun Kelly

Brooklyn Beckham Has Chelsea Football Trial

The 13-year-old son of David and Victoria Beckham has played in a match at the south-west London club's training ground in Surrey.
Brooklyn Beckham is as big a football fan as his father
David Beckham's eldest son Brooklyn has had a trial with Chelsea football club.
The 13-year-old played in a game at the Premier League side's training ground in Surrey on Tuesday.
It is understood it was a low-key academy training match aimed at giving him a taste of English junior football.
Sky sources said: "Brooklyn was there as part of a big try-out, with talented kids coming from around the world. "It was not just one day, there are several days as part of it so no decision has been made."Brooklyn Beckham and his brothers were keen on football when in the US
The sources added: "All three of the boys absolutely love football and they are glad to be back and living in London."
Former England captain David, 37, is currently without a club after leaving Los Angeles Galaxy at the end of the Major League Soccer season.
He and his family are understood to be living in south-west London in a £20m house.

Beckham was pictured on Twitter with a young team player at Chelsea's Cobham training base prompting speculation he..

Eden Hazard Pega una Patada a un Recogepelotas del Swansea // Chelsea // Capital One Cup

Wananchi wa Ngara Waendesha Operesheni ya Kuwaondoa Wahamiaji

Wananchi wa kijiji cha Kasuro mpakani mwa Tanzania na nchi ya Rwanda wameendesha operesheni ya kuwaondoa nchini wahamiaji haramu wenye makundi makubwa ya mifugo waliomilikishwa ardhi kinyume cha sheria baada ya serikali kushindwakutekeleza ahadi zake za kuwaondoa takribani miaka kumi iliyopita na kuchochea migogoro ya ardhi na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Siri ya Mtungi - Sehemu ya 1 (Tamthilia)

"Siri ya Mtungi" ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu

NI MARUFUKU WALIMU KUWAREJESHA WANAFUNZI NYUMBANI KWA KISINGIZIO CHA ADA

 
Na Kibada Kibada wa Fullshangwe-Katavi
Serikali imepiga marufuku Wakuu wa shule za Sekondari wote nchini kuwarudisha nyumbani wanafunzi kwa kisingizio cha kukosa Ada na michango ya aina yeyote ya aina mbalimbaliwatoto wanaoshindwa kuchangia na kulipa Ada kutokana na ama wazazi kutokawa na uwezo wa kulipia kwa wakati michango hiyo.
Agizo hilo limetolwa jana na Naibu waziri wa Tamisemi Aggrey Mwanri wakati wa ziara yake mkoani katavi mara baada ya kutembelea shule ya sekondari ya Nsimbo Mkoani Katavi na kusomewa taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi wanashinwa kuendelea na masomo kutokana na kukosa ada na michango mbalimbali inayotolewa mashuleni kutokana na wazazi waokuokuwa na uwezo.
“Ni marufuku kwa mkuu yeyote wa shule kuwrudisha nyumbani watoto kwa sababu ya kukosa ada ikiwamo michango ya madawati kwani kumrudisha nyumbani mtoto ni kumuonea michango hiyo adaiwe mzazi wakati mwanafunzi akiendelea na masomo”alisema Naibu waziri.

Alieleza kuwa michango yote inayotakiwa kukubaliwa shule ni lazima Katibu Tawala wa mkoa husika aione na kuridhia kwenye barua na siyo wakuu wa shule kujiamulia kienyeji hali inayoonesha kuwarudisha nyumbani wato ambao ..

Trapee ft Size 8 - City life

Trapee brings you yet another infectious banger featuring Linet aka Size 8 about the hustle of the big city

Video ya Ofisa wa TRA Akichukua Rushwa Waziwazi!!

Video hii imerekodiwa kutoka kwenye simu ya mkononi na inamuonyesha Ofisa wa TRA Arusha akipokea rushwa toka kwa mteja ili aweze kumhudumia.
Ofisa huyu yupo mapokezi (reception) na inadaiwa ni kawaida yake kupokea Rushwa na kuwa usipompa anadai kwa nguvu.
Wafanyakazi wa TRA na wakubwa zake inadaiwa wanajua kinachoendelea lakini hawachukui hatua.
Kuna utendaji mbovu, lugha chafu kwa wateja na za majivuno na mambo mengi yanayofanana na hayo.
Mamlaka husika zinaombwa kuingilia kati TRA Mapato, (karibu na Benki Kuu tawi la Arusha) ili raia wapate huduma bila vikwazo vya rushwa toka kwa maofisa kama huyu.