Pages

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAONGEZA MUDA WA MAOMBI YA MKOPO

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU   KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2013/2014

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kuwa muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja hadi Julai 31, 2013.

Pamoja na nyongeza hii ya muda, Bodi inasisitiza waombaji kujaza fomu za maombi ya kwa njia ya mtandao (OLAS) kwa usahihi na kuzingatia muda wa maombi uliowekwa ili kuepuka usumbufu usio wa lazima. Waombaji wa mara ya kwanza wahakikishe wanajaza kwa ufasaha na kuweka viambatanisho vyote muhimu ili kufanikisha mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo.

Kundi la kwanza la wanafunzi waliopangwa kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambao wamemaliza mafunzo hayo mwezi Juni, 2013 wanapaswa kutumia fursa hii kujaza fomu za maombi ya mikopo bila kukosa. Aidha, kundi la pili la wanafunzi wanaotegemea kuanza mafunzo hayo mwezi Julai, 2013 walitakiwa wawe wameshaomba mikopo kati ya tarehe 1 Mei, 2013 na 30 Juni, 2013 lakini endapo kuna wachache ambao hawakuweza kufanya hivyo basi nao watumie muda huu wa nyongeza kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao wakiwa huko huko JKT.

Endapo mwombaji yeyote atakabiliana na matatizo wakati wa kujaza fomu yake anashauriwa kupiga simu kwenye dawati la huduma kwa wateja kwa namba 022 550 7910 kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 2.00 usiku siku za Jumatatu hadi Ijumaa, na kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 10.00 jioni siku za Jumamosi.

Ikumbukwe kwamba Bodi haitaongeza muda wa ziada baada ya Julai 31, 2013 ili kutoa nafasi kwa Bodi kuendelea na mchakato wa uchambuzi na upangaji mikopo.
IMETOLEWA NA:
BODI YA WAKURUGENZI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

A Frustrated Kenyan Responds to Obama Skipping Kenya (Video)

Hasan Salaam - Miss America (prod. by Snowgoons f/ DJ GI Joe) Video

Jaco Beats -Kilaza Official HD Video

SPIKA WA BUNGE LA OMAN NA UJUMBE WAKE WAWASILI DODOMA, ASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO BAINA YA BUNGE LA TANZANIA NA BUNGE LA OMAN

OMAN
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
Abdulkarim Shah
Kaminisha wa Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Abdulkarim Shah akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Dodoma jana.
 Job Ndugai
Naibu Spika Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Katibu wa Bunge. Dkt. Thomas Kashililah kwa Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali alipowasili Dodoma jana.
Anne Makinda
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Dodoma ambapo anafanya ziara ya kibunge ikiwa ni pamoja na kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
Anne Makinda
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali wakisaini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano baina ya mabunge haya mawili.
 Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali
Wakibadilishana mikataba ya Makubaliano.
 Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali

Picha ya Pamoja Ujumbe wa Spika wa Bunge la Oman na Wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania.
Spika wa Bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Bin Nasir Al Maawali akiwa na ujumbe wa Wabunge toka Oman yupo hapa nchini kwa ziara ya kikazi ya siku sita ambapo pamoja na mambo mengine amesaini mkataba wa uanzishwaji wa ushirikiano wa Bunge la Tanzania na Bunge la Oman katika Maswala mbalimbali. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

MAOFISA WA MAREKANI WADAI KUWA WAO NDO WATAPANGA MAWAZIRI WA TANZANIA WATAKAORUHUSIWA KUSHIKANA MKONO NA OBAMA AKIJA DAR

 Barack Obama
Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI.

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Moses Malaki aliliambia gazeti hili jana kuwa matayarisho ya ujio wa Rais huyo ni kabambe na hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Pia alisema shughuli za kumpokea Rais Obama, anayetarajiwa kutua Jumatatu saa 8:40 mchana, zitaanza asubuhi kwa maofisa wa Marekani kushika majukumu yote katika uwanja huo, ikiwemo kuongoza ndege, ukaguzi wa abiria na mizigo, kwa maana wafanyakazi wa uwanja huo kuwa likizo kwa siku mbili.
“Wamesema kuwa wao watasimamia kila kitu kuanzia wageni watakaoingia na kutoka na wataamua nani aingie na kutoka,” alisema Malaki.
Aliongeza kuwa japokuwa Mamlaka ya Anga Tanzania (TAA) inaendelea kufanya kazi zake kama kawaida, lakini Jumatatu, Wamarekani watasimamia kila kitu hadi ukaguzi wa wageni.
“Siku hiyo mwongoza ndege wa TAA, atafanya shughuli kidogo, mambo mengine yatafanywa na wao,” alisema.

Idadi ya maofisa wa Tanzania
Imebainika kuwa hata idadi ya maofisa wa Tanzania wakiwemo viongozi watakaompokea pia itapangwa na Wamarekani wenyewe.

“Wenyewe wana orodha yao na wanajua nani atakuwepo au hatakiwi kuwepo katika kundi la wageni watakaompokea Rais Obama,” alisema na kuongeza:

“Nilimuuliza Ofisa Usalama wa Marekani iwapo nitaweza kumwona Rais Obama, akaniambia: Utamwona ukibahatika kuwepo kwenye orodha.”

Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe naye alikiri kuwa mawaziri wanaotakiwa kuwepo katika msafara wa kumpokea Rais Obama ni wachache watakaochaguliwa tu na Wamarekani, baada ya kuyapitia na kuyachunguza majina hayo kwanza kabla ya kuyakubali.

“Hii sijawahi kuiona, hata sisi wenyewe tunateuliwa na wakishayapitia wataamua, nani aende au asiende,” alisema Chikawe.
Mwananchi

Ibra Da Hustler ft Ude Ude – Sababu Ya Wewe (Audio)

Ibra Da Hustler

WATANZANIA WANAHITAJI MAJIBU YA UJIO WA RAIS OBAMA, SOMA MASWALI


1) Wamarekani kuingiza majeshi na makachero zaidi ya 1500 ndani ya nchi huru na kusimamia ziara ya Rais wao, hii si aina ingine ya kuitawala Tanzania kwa muda?

2) maafisa wa Serikali na mawaziri kufanyiwa mchujo, ili wale tu kupata mawaziri na maafisa wenye hadhi ya kuwa kwenye msafara wa Obama , hii si inazidi kuthibitisha kuwa Obama sio tu anakuja kama Mgeni, ila anakuja kama mwenye mamlaka ya juu nchi huru?

3)je hii fedheha kwa wale mawaziri ambao utawala wa Obama utaona haufurahishwi nao, hivyo wao kutotakiwa kwenye kumpokea Rais Obama, je hii si kudhalilisha Itifaki na Protokali za Tanzania?

4) je, hii ya kuwatangazia wananchi wasije Dar es salaam kwa kuwa Obama annakuja, nayo haizidi kuthibitisha haya kuwa pengine ni maelekezo toka kwenye mamlaka kuu "marekani" ?

5) Akiwa ziarani Senegal Rais Obama aliendelea kusisitiza Africa kubadilika na kukubali ndoa za jinsia moja, je Tanzania iko Tayari kusema HAPANA kwa ndoa za jinsia moja, au itachekea hizo dola milioni 800 zenye masharti?

6) hii miradi ya Simbion/dowans/richmond atakayotembelea Obama,

DOKII - OBAMA WELCOME TANZANIA (Video)

Kipanya Leo

Kipanya