Pages

Picha Kali za Leo

Picha
Picha

Cheki Kiji-Camera Hiki Kilichogunduliwa Huko Sweeden Kinavyoweza Kufanya Kazi

Technolojia Imekuwa Kwa Kasi Kubwa Sana, Tazama Kiji-Camera Hiki Kilichogunduliwa Huko Sweeden Kinavyoweza Kufanya Kazi
Memoto Katika jitihada za kuhakikisha kuwa inawezekana kuweka kumbukumbu ya kila kitu kinachoendelea katika maisha ya binadamu masaa yote bila kupumzika kwa kutumia njia ya picha, Kampuni ya Memoto ya nchini Sweeden chini ya Martin Kaellstroem, wamefanikisha kutengeneza ki-camera kidogo ambacho huweza kuvaliwa na mtu katika mavazi yake ya kawaida na kuendelea kurekodi kila kitu katika mishe zake bila kusimama.

Kicamera hiki ambacho kinatambulika kwa jina Memoto Camera, Ambacho kipo katika mfumo wa ipod ndogo, hukusanya picha za matukio yote kwa kutegemea location ya GPS ambayo mtumiaji yupo kwa wakati huo, muda na kiasi cha mwanga pia na kuzistream moja kwa moja katika mtandao.
Memoto Camera, Njia hii imetajwa kama teknolojia mpya ambayo itasaidia sana kuweka kumbukumbu ya mambo na matukio na kupunguza kazi ya kuweka rekodi hizi katika diary.
Memoto Camera,Kizuri zaidi kuhusiana na camera hizi ni kuwa, unaweza kuunganisha mfumo wa kumbukumbu za matukio haya na picha hizi zikawa zinaenda moja kwa moja katika mitandao kama twitter na facebook.

Mh. Sugu Ajisalimisha. NI BAADA YA POLISI KUMSAKA USIKU, MCHANA

Joseph MbilinyiBAADA ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kumsaka kwa siku mbili bila mafanikio mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu (CHADEMA), akidaiwa kumpiga na kumjeruhi mmoja wa askari wa Bunge, hatimaye alijisalimisha mwenyewe jana jioni.
Taarifa zilizotufikia wakati tunakwenda mitamboni, Sugu alikwenda polisi akiongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wabunge Tundu Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Ubungo) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki).
Akizungumza na gazeti hili, Mnyika alisema kuwa Sugu hakukamatwa bali alijipeleka mwenyewe polisi kwa hiari yake na kwamba jioni hiyo majira ya saa 1:10 alikuwa akiandikisha maelezo yake.
Wakati Sugu akijisalimisha, wanasheria wa Bunge nao walikuwa wamejifungia kuangalia namna ya kumkabidhi mbunge huyo mikononi mwa sheria.
Juzi na jana viwanja vya Bunge vilitawaliwa na idadi kubwa ya polisi waliotumwa kumkamata Sugu lakini mpaka Bunge linaahirishwa jioni haikujulikana ni wapi alikokuwa mbunge huyo.
Mbunge huyo juzi baada ya kubebwa mzobemzobe na askari wa Bunge na kisha kutolewa nje ya ukumbi, inadaiwa kuwa alimpiga ngumi mmoja wa askari aliyemtuhumu kuwa alikuwa amempia ngumi wakati wakimtoka nje.
Askari hao juzi jioni walikuwa kwenye vikundi vikundi nje ya ukumbi wa Pius Msekwa ambako kulikuwa kukifanyika mkutano wa wabunge wa upinzani ambapo Sugu pia alikuwa miongoni mwao.
Kutokamatwa kwa Sugu kumewashangaza wengi waliokuwa karibu na askari hao kwa kuwa alikuwa amekaa jirani nao akizungumza na wenzake kabla ya kuanza kwa kikao chao.
Tanzania Daima lilidokezwa kuwa askari hao walishindwa kumkamata Sugu kwa kuwa hapakuwepo na amri ya kukamatwa kwake na hata ilipotolewa alikuwa ameshaondoka katika viwanja vya Bunge.
Mpaka Bunge linaahirishwa juzi jioni, idadi kubwa ya askari walikuwa nje ya milango na korido zilipo ofisi za kambi ya upinzani wakimsubiri Sugu bila mafanikio.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa mambo yaliyochangia askari kusuasua kukamatwa kwa Sugu ni kutokana na kinga ya kibunge aliyonayo na pia kosa analotuhumiwa kulifanya alilifanya akiwa kwenye viwanja vya Bunge.
“Tulipata mtanziko wa kumkamata haraka haraka, ilibidi lazima tuwasiliane na ofisi ya Spika kujua taratibu za kumkamata kiongozi huyo hasa kwa kuwa alifanya kosa hilo akiwa bungeni,” kilisema chanzo kimoja.
Wakati askari wakihaha kumtafuta Sugu, mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), jana aliomba mwongozo wa Spika kuhusu tukio la vurugu zilizotokea juzi bungeni hasa tukio la Sugu kumpiga askari.
Sendeka alisema tukio hilo limelidhalilisha Bunge na askari wanaowalinda, hivyo akataka liweke wazi ni hatua gani zitakazochukuliwa dhidi ya mbunge huyo ili kulinda heshima ya chombo hicho.
“Nataka nijue ibara ya 100 ambayo humpa kinga mbunge na uhuru wa mawazo akiwa ndani ya Bunge inatumikaje katika tukio hili?
“Je, Bunge litalindaje heshima yake dhidi ya tukio hili lililofanywa na mbunge mwenzetu?” alihoji.
Akijibu mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama, alisema tukio hilo ni geni hivyo Bunge limeshindwa kutoa jibu la mara moja.
“Jambo hili halijawahi kutokea katika historia ya Bunge, sasa nami nitalifikisha kwa wanasheria wa Bunge wanishauri namna ya kulishughulikia na baada ya hapo nitatoa mwongozo,” alisema.
Akitoa mwongozo huo muda mfupi kabla ya Bunge kuahirishwa jana jioni, Naibu Spika, Job Ndugai, alisema kuwa bado wanashauriana na wanasheria kuona kanuni zinawaelekezaje.
Alisema kuwa licha ya tukio hilo kutokea katika eneo la Bunge bado kitendo hicho ni cha jinai na hivyo, mtuhumiwa atashughulikiwa kisheria.
“Ni sawa na jaji yuko mahakamani ambapo kuna kinga kama za Bunge halafu jaji mwenzake ampige ngumi. Huyo lazima achukuliwe hatua hawezi kuachwa. Kinga zetu ziko kwenye uhuru wa mawazo tu,” alisema.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, juzi lilitangaza kumsaka Sugu kwa tuhuma za kufanya vurugu na kumjeruhi askari wa Bunge.
“Lakini tuna mashaka sana na hatua yake aliyoifanya nje ya ukumbi ambapo alimvamia na kumpiga ngumi nzito Koplo Nikwisa Nkisu ambaye alijeruhiwa jicho,” alisema mmoja wa askari ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Ofisa Upelelezi wa Wilaya ya Dodoma ASP Jumanne Kim, juzi jioni alithibitisha kusakwa kwa mbunge huyo aliyeondoka maeneo ya Bunge mchana akiwa ndani ya gari la kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe.
Chadema blog

Nyota wa Airtel Rising Stars Kwenda Nigeria

Airtel Rising StarsTimu za wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka 17 ambazo zitaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars zinaingia kambini jijini Dar es Salaam kesho (Alhamisi September 5) kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kukwea pipa kwenda nchini Nigeria kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Jumatano Sept 4), Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wachezaji hao chipukizi watashughulikia na kukamilisha hati zao za kusafiria kati ya kesho, Alhamisi na Ijumaa. “Kwa upende wetu kila kitu kimekamilika kwa ajili ya safari kuelekea kwenye mashindano hayo ya kimataifa ambayo yatashirikisha timu kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika,” alisema.

Jumla ya wavulana na wasichana 32 walifuzu kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu wakati wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zilizofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Juni. Mashindano haya ya kimataifa yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu yakiwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa wachezaji chipukizi kuendeleza vipaji vyao.

Kwa mara ya kwanza mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yalifanyika jijini Nairobi mwaka jana ambapo Tanzania iliwakilishwa na timu ya wavulana pekee ambayo hata hivyo ilitolewa hatua za awali huku timu ya Nigeria ikitawazwa kuwa mabingwa.

“Kulingana na kiwango cha kuridhisha cha wachezaji waliochaguliwa mwaka huu nina imani kwamba timu zetu za Tanzania – wasichana na wavulana – wana nafasi nzuri ya kufanya vizuri,” anasema Matinde ambaye ni mmoja wa maofisa wa Airtel Tanzania waliongoza na timu kwenye mashindano hayo.

Airtel imeanzisha mashindano haya ya vijana barani Afrika kwa nia ya kusaidia upatikanaji wa vijana wenye vipaji vya soka kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ngazi ya Taifa. Airtel Rising Stars inatoa fursa kwa vijana kudhihirisha uwezo wao kwa makocha wa Taifa na kimataifa na kuweza kujiendeleza zaidi kisoka.

Hivi sasa Airtel Rising Stars ni moja ya matukio muhimu ya kisoka kwenye kalenda ya Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF). Huanzia katika hatua ya usajili ikifuatiwa na mechi za mtoano ili kupata wachezaji nyota wa kuunda timu za mikoa ambazo huchuana katika ngazi ya Taifa.

Airtel inaendesha muchuano hii kwa kushirikiana na klabu maarufu duniani ya Manchester United ambayo hutoa ushauri wa kiufundi na michuano hii imekuwa na hamasa kubwa katika nchi zote zinazoshiriki.

CHEKI MH.SUGU ALIVYOCHEZEA KICHAPO BUNGENI

Joseph Mbilinyi
Askari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimdhibiti Mbunge wa Chadema kutoka jimbo la Mbeya Mjini Mh. Joseph Mbilinyi 'Sugu' wakati akitolewa ndani ya Ukumbi wa Bunge,baada ya kupishana kauli na waheshimiwa wenzake.

JWTZ Yatoa Sababu 200 Zilizoifanya Tanzania Ipambane na Waasi wa M23

JWTZ
Ushiriki wa Tanzania katika Operesheni ya Ulinzi wa Amani nchini DRC, unatokana na mgogoro kati ya Serikali DRC na waasi hususan kikundi cha waasi cha M23. Mgogoro huo ulianza mwezi Aprili 2012 ambapo kikundi cha M23 kilijitoa katika Jeshji la serikali ya DRC na kuanzisha mapigano hali iliyopelekea hali ya usalama nchini DRC kuwa mbaya.

Kufuatia hali hiyo mbaya ya usalama, wakati wa kikao cha International Conference on the Great Lakes Region kilichofanyika tarehe 12 Julai 2012 mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mhe. Rais Joseph Kabila aliwasilisha ombi kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambazo Rwanda, Uganda, Tanzania, na DRC akaomba nchi wanachama wa Maziwa Makuu zisaidie kuwapokonya silaha waasi wa M23.
Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikubaliana na ombi hilo na kutoa maelekezo kwa Mawaziri wa Ulinzi ambao walikutana tarehe 01 hadi 2 Agosti 2012 na kujadili maelekezo ya Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu. Mawaziri wa Ulinzi walikubaliana kuwa ni muhimu kwa vikundi vyote vya Waasi (ADF, FDLR na M23) kushughulikiwa na wakawasilisha mapendekezo yao kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu.

Tarehe 7 Agosti 2012, Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu walikutana tena mjini Kampala, Uganda na kupanga mkakati wa kuanzishwa kwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na nchi wanachama wa Nchi za Maziwa Makuu zikaombwa kuchangia askari watakaounda ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ambapo Tanzania iliombwa na ikahadi kuchangia kikosi kimoja. Kikao hiki kilitoa maelekezo ya hatua inayofuata kwa Mawaziri wa Ulinzi wa Maziwa Makuu.

Tarehe 7 hadi 8 Sep 2012, Mawaziri wa Ulinzi wa maziwa Makuu, walikutana na kujadili utekelezaji wa uanzishwaji wa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Wakaunda ‘Military Assessment Team (MAT)’ kufanya tathmini ya tishio. Timu hiyo ililifanya tathmini na kuwasilisha taarifa yake kwenye kikao cha Mawaziri wa Ulinzi kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2012 mjini Goma, DRC na baadaye taarifa hiyo iliwasilishwa kwa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu ambao waliagiza kushirikishwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Afrika(AU) na Umja wa Mataifa(UN) ili kufanikisha mkakati huo.

Nchi wanachamma wa SADC na Nchi za Maziwa Mkuu kwa pamoja walikubaliana na kupendekeza SADC Standby Brigade ipelekwe DRC kama ‘Neutral Intervention Force (NIF)’. Kufuatia ridhaa hiyo nchi wanachama wa SADC ziliombwa kuchangia ambapo nchi mbalimbali wanachama zilikubali kuchangia, lakini Umoja wa Mataifa(UN) ilizipitisha nchi za Tanzania, Afrika Kusini na Malawi kuchangia askari nguvu ya Brigedi moja kuunda NIF ya MONUSCO.

Aidha, Umoja wa Mataifa mwezi Januari 2013 uliridhia mapendekezo ya Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu na Nchi wanachama wa SADC ya kuundwa ‘Neutral Intervention Force (NIF)’ na kupelekwa DRC. Kufuatia idhini hiyo tarehe 28 Machi 2013, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio (Resolution) namba 2098 (2013) na kutoa jukumu maalumu la ulinzi wa amani nchini DRC, likijumuisha ushiriki wa Neutral Intervention Force (NIF) kama sehemu ya MONUSCO, na ikaitwa ‘Force Intervention Brigade (FIB)’ ambayo kikosi cha Tanzania ni sehemu ya Brigade hiyo.

Kwa mantiki hiyo ieleweke kwamba, Kikosi cha Tanzania kilichopo DRC ni sehemu ya SADC standby brigade iliyotoa mchango wake katika Jeshi la Umoja wa Mataifa (MONUSCO). Kinafanya kazi chini ya Force Commander, MONUSCO na majukumu yake ni:
Kuzuia waasi kujitanua (Prevention of Expansion)
Kuvunja nguvu za waasi (Neutralization)
Kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.

Kwa kuzingatia kuwa kikosi chetu kiko chini ya majeshi ya Umoja wa Mataifa ya MONUSCO, inamanisha kuwa Operesheni hiyo ni ya Umoja wa Mataifa, Tanzania haipigani na M-23 na haina tatizo na Rwanda kuhusiana na Operesheni hiyo na ridhaa ya kikosi chetu kwenda DRC ilikubaliwa pia na Rwanda, nchi ambayo ni mwanachama wa nchi za Maziwa Makuu. Aidha, Rwanda imesaidia sana kwa kuruhusu kikosi cha Tanzania kupitisha watu, vifaa na zana katika nchi yake kupeleka DRC.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
6/9/2013
Dar es Salaam.