Pages

Tindikali Yaendelea Kuuzwa Kama Njugu Mitaani Dar

Tindikali
Dar es Salaam. Siku chache baada ya wasichana wawili raia wa Uingereza kumwagiwa tindikali mjini Zanzibar, imebainika kuwa, tindikali za aina mbalimbali zinauzwa kiholela kama njugu jijini Dar es Salaam.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa jijini Dar es Salaam yapo maduka mengi yanayouza tindikali ya kila aina na bidhaa hiyo inauzwa bila ya udhibiti wowote kuanzia Kariakoo hadi Vingunguti.

Wiki iliyopita, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alitoa miezi mitatu kwa wafanyabiashara wa tindikali kujisajili ili kuzuia kuongezeka kwa matukio ya uhalifu kwa kemikali hiyo nchini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika mitaa ya Dar es Salaam, umebaini kuwa tindikali za aina mbalimbali zinapatikana kwa wingi katika maduka ya rejareja na jumla, huku wauzaji wa bidhaa hizo wakishindwa kutoa tahadhari yoyote kwa wateja wao.
SOMA ZAIDI

Google Blackout Sees Global Web Traffic Plunge by 40% -Internet apocalypse

Worldwide internet traffic plunged by about 40 per cent as Google services suffered an ‘unprecedented’ black-out, web experts have revealed.
Google Blackout
The Google data center in Douglas Country, Georgia. The company is refusing to reveal what caused the ‘unprecedented’ blackout

The tech company said all of its services from Google Search to Gmail to YouTube to Google Drive went down for between one and five minutes last night but it refused to elaborate on the reasons why.
According to web analytics firm GoSquared, global internet traffic fell by around 40% during the black-out, reflecting Google’s massive grip on the web.
‘That’s huge,’ GoSquared developer Simon Tabor told Sky News. ‘As internet users, our reliance on Google.com being up is huge.
‘It’s also of note that pageviews spiked shortly afterwards, as users managed to get to their destination.’

A message on the Google Apps Dashboard showed all of its services were hit.
‘We’re aware of a problem with Gmail affecting a significant subset of users. The affected users are able to access Gmail, but are seeing error messages and/or other unexpected behaviour,’ it said.

A later message said: ‘Between 15:51 and 15:52 PDT, 50% to 70% of requests to Google received errors; service was mostly restored one minute later, and entirely restored after four minutes.’
Experts said the outage had cost the company about £330,000 and that the event was unheard of. They are baffled by the cause.
Computer website writer Neil McAllister added said technical experts would be ‘nervous’ as they sought to find out what happened.
‘Exactly how an operation like Google’s can even go dark like that, all at once, is anybody’s guess,’ he said.
By In2EastAfrica Reporter

NashMc/sightMo/Viva/Salmin Swaggz/Nyigu/Gentriez - Asante (Audio)

NashMc/sightMo/Viva/Salmin Swaggz/Nyigu/Gentriez - Asante

Mengi Wanaongea -Docta D One & Eazy One Feat Jeff Legend (Video)

Tanzanian Blog Awards, Shindano la Mwaka Huu 2013

Tanzanian Blog Awards
Vipengele vya Kushiriki na Sheria Tafadhali soma vizuri. Mwaka huu tumebadilisha,vipengele vya shindano letu na sheria ya shindano letu. Kwa blog yako au blog unayotaka ipendekezwe tafadhali wataarifu bloggers hao, hatutaki kushirikisha bloggers ambao hawataki kuhusishwa katika shindano hili. Sasa ili tujue kuwa blogger huyo unayempendekeza amekubali au anajua kushirikishwa kwake katika shindano hili mwambie alink blog yake katika shindano letu.

Jinsi ya kulink
1. Aandike post kuhusu shindano hili na kuwataarifu wasomaje wake katika post hiyo alinki kwetu...Tanzanian blog awards link.

2. Kama blog unayoipendekaza hatafanya hivyo blog yake haitashirikishwa

3. Unaweza kupendekeza blog katika vipengele vingi upedavyo lakini katika kila email unayotuma ni blog moja tu utaruhusiwa kuipendekeza kwa wakati mmoja
mfano: Kwenye subject unaandika jina la blog unayotaka kuipendekeza
tanzanianblogawards.blogspot.com
Kwenye body ya email unaandika vipengele unayotaka blog hiyo ishirikishwe
Best Agriculture
Best Beauty/Fashion Blog
etc etc

4. Email iwe ni ya ukweli kama tukiwa tunataka kuwasiliana na wewe kuhusu link ya blog uliyopendekeza tuweze kufanya hivyo na tuma mapendekezo yako kwa hii hapa Email

nomination@bloggersassociationoftanzania.com au tanzanianblogawards@gmail.com

5. Mwanzo wa kupokea mapendekezo hayo ni
Tarehe 17/8/ 2013 saa 12:01am mpaka tarehe 30/8/2013 saa 11:59pm saa za Africa mashariki

Vipengele
Best Agriculture
Best Beauty/Fashion Blog
Best Business Blog
Best Creative Writing Blog
Best Design/Graphic Design Blog
Best Educational Blog
Best Entertainments
Best Food Blog
Best General Blog
Best Inspiration Blog
Best Newcomer Blog
Best News Blog
Best Photography Blog
Best Political Blog
Best Religion Blog
Best Sports Blog
Best Technology Blog
Best Tots Blog (17 yr old and below)
Best Travel Blogs

TAARIFA YA HARAKATI YA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KWA VYOMBO VYA KHABARI

Bismillar Rahmanir Rahiim JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)
Jana asubuhi majira ya saa nne na nusu askari wa jeshi la Polisi na watu wanaoaminika kuwa usalama wa taifa walikwenda hospitali ya Muhimbili (MOI) na kumchukua Sheikh Ponda Issa Ponda. Juhudi za Sheikh Mwenyewe, mkewe na waislam waliokuwepo pale hospitali kutaka abaki hospitalini kuendelea na matibabu hazikuzaa matunda. Mpaka Sasa bado tunafuatilia kujua mahali Kiongozi huyo wa Kiislam alikopelekwa.
Tumepokea kwa masikitiko makubwa sana habari hizi na tunashindwa kuamini kama mambo haya yanaweza kufanywa na Serikali inayodai kutawala kwa kufuata utawala bora unaojali sheria, uadilifu, utu na uhuru wa kujieleza.
Kitendo cha kumpiga risasi Sheikh Ponda na kisha kumchukua toka hospitalini na kumpeleka Gerezani kwa kukiuka taratibu ni kinyume cha haki za binadamu, utawala bora na uhuru wa maisha ya mtu. Matibabu ni haki mojawapo kwa binadamu yoyote hata kama kuna wanaomtuhumu. Tuhuma juu ya mtu si sababu ya kukiuka taratibu, kuvunja sheria na hata kumtisha unayemtuhumu kwani njia hiyo haiwezi kutatua tatizo bali inalifanya kuwa kubwa zaidi.
Jumuiya na Taasisi za Kiislam tunalaani kwa mara nyingine kitendo cha Polisi na Usalama wa Taifa kutenda vitendo vinavyoashiria uonevu kwa viongozi wa dini ya Kiislam na tunaitaka Serikali kutenda uadilifu kwa raia wake hata pale inapokuwa inaamini kuwa raia hao wanamakosa.
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu zinapinga kwa kauli moja tume iliyoundwa na jeshi la polisi kuchunguza unyama aliofanyiwa Sheikh Ponda na waislamu hawatatoa ushirikiano kwa tume hiyo ya jeshi la polisi.
Jumuiya na Taasisi za Kiislam zinaitaka serikali kuunda tume huru itakayohusisha viongozi wa kiislamu wanaoaminika kwa ummah kuchunguza tukio la kupigwa risasi Sheikh Ponda Issa Ponda ili kujenga mustakbali mzuri wa amani ya Taifa letu.
Jumuiya na Taasisi za Kiislam hapa nchini zinaamini kuwa ufumbuzi wa suala la amani ya kweli na ya kudumu ya nchi yetu, upo katika kushughulikia madai ya msingi ya waislam dhidi ya Serikali ambayo ndio chanzo cha kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda kwa kuyasema waziwazi, na si kwa kuwatesa, kuwadhalilisha na kuwaauwa Viongozi wa kiislam.
Kutokana na tukio hili Jumuiya na Taasisi za Kiislam zimeitisha mkutano wa dharura utaofanyika katika viwanja vya Nurul yakin siku ya Jumapili saa 9 alasili kutafakari kwa pamoja na hatimae kuchukua hatua za msingi zitazoleta tija ya kweli ili Viongozi wa Kiislam wasiendelee kudhalilishwa.
SHEIKH JUMA SAID ALLY
MWENYEKIT JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM
16/08/2013

Lady Jaydee - Yahaya Official Video

Sakaktaa la Madawa ya Kulevya. Waliochelewesha Mbwa wa Ukaguzi Uwanja wa Ndege Kufukuzwa kazi

Kufuatia matukio ya kukamatwa kwa dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, serikali imewafukuza kazi na itawafikisha mahakamani watumishi wake wa tano na askari polisi mmoja wa uwanjani,ambapo maofisa wa usalama wa taifa waliochelewesha kuwapeleka mbwa uwanjani hapo siku ya tarehe 05 July 2013 na Kupitisha kiasi kibubwa cha dawa za kulevya wanachunguzwa.

MKUTANO WA MAREKEBISHO YA KATIBA KWA WATANZANIA MAREKANI

Marekani na Canada
Tume ya Mapendekezo ya katiba kwa watanzabia wanaoishi Marekani imeundwa ili kukusanyamaoni na mapendekezo kutoka kwa watanzania wore waishio nchini Marekani na Canada.
website www.katibatanzania.org

Baadhi ya Waumini wa Msikiti wa Mtambani Dar Wamemkamata Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi na Kumshikilia kwa Muda Kabla ya Kumwachia kwa Masharti

Askari wa Jeshi la Polisi  Askari Polisi wakizunguka doria eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam Jana kuhakikisha kuna amani.
Askari wa Jeshi la Polisi
Askari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakizunguka kufanya doria maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam jana kuhakikisha kuna amani.
Msikiti wa Mtambani
Baadhi ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani wakiwa wamemzunguka askari Polisi, Jonathan Tossi (katikati aliyeshika kamera) wakimuhoji baada ya kumshikilia kwa muda, hata hivyo walimuachia kwa masharti ya kumtaka afute picha zote alizopiga eneo hilo.Picha kwa hisani ya Gazeti la Jambo LEO
  BAADHI ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani Jijini Dar es Salaam jana wamemkamata mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi na kumshikilia kwa muda kabla ya kumwachia kwa masharti kadhaa. Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kimebainisha askari aliyekamatwa ni Jonathan Tossi ambaye anafanya kazi kitengo cha habari na uhusiano wa Jeshi la Polisi.

Askari huyo alijikuta akiingia kwenye mikono ya waumini hao alipokuwa akitekeleza majukumu yake (kazini) akipiga picha mtaani maeneo ya Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema baada ya waumini hao kumkamata askari huyo walimuhoji kwa muda kisha kutaka kitambulisho chake na kumuamuru afute picha zote alizokuwa akipiga eneo hilo ili wamuachilie kwa usalama wake.
“Kutokana na kuhofia usalama wake alikubaliana nao na kisha kufta picha zote alizopiga. Walimtaka pia aoneshe kitambulisho na kuhoji ni kwanini anapiga picha wakati yeye ni askari…baada ya kukubaliana na masharti hayo walimuachia,” kilisema chanzo chetu.
“Sisi wenyewe tunashangaa wapiga picha walikuwa wengi wa vyombo mbalimbali vya habari hatujui hawa walijuaje kwamba yule jamaa alikuwa askari na wakati alikuwa amevaa kiraia,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo la tukio.

Leo mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ulinzi na doria iliim*rishwa na Jeshi la Polisi ambapo magari na pikipiki za Polisi zikiwa na askari waliojiandaa kutuliza ghasia yalikuwa yakizunguka ikiwa ni kujiandaa kwa kukabiliana na vurugu zozote.

Mitaa kadhaa mwandishi wa mtandao huu alishuhudia askari walio na mabomu ya machozi, huku wakiwa wamevalia vifaa maalumu vya kujikinga na risasi wakizunguka kwenye magari yao maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Da rs Salaam. Hata hivyo hakuna taarifa za kutokea vurugu zozote.

Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zinasema doria ya polisi ililazimika kufanywa baada za kuwepo na taarifa kuwa huenda wafuasi wa Shekhe Issa Ponda wangelifanya fujo kutokana na kutoridhishwa na hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo kwa tuhuma kadhaa zinazomkabili.

Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuzungumzia kwa kina taarifa hizi hazikuzaa matuna. Hata hivyo Thehabari inaendelea kumtafuta kwa ufafanuzi zaidi wa tukio la kukamatwa kwa askari wao na kuachiwa.