Pages

PICHA za KATE, PRINCE WILLIAM WAKIWA NA MTOTO WAO

Kate Middleton, Prince William,  
Juu na chini ni Kate Middleton, Prince William, katika picha ya pamoja na mtoto wao nje ya ngazi za hospitali ya Mt. Mary hospitali ambayo Kate amejifungulia mtoto wao wa kwanza siku ya Jumatatu mchana July 22, 2013 Prince William aliwaambia wanahabari bado hawajampa jina huku Kate akiongezea kwamba Mumewe ameweza kumbadilisha mtoto wao diaper ya kwanza naona ameanza kupata uzoefu. Kate Middleton, Prince William, Kate Middleton, Prince William, Kate Middleton, Prince William,
Vijimambo

Rage Auzika Rasmi Uwanja wa Simba

Hati bado hawajapewa na watapewa siku yoyote. Kiwanja kipo Bunju plot no. 226 block 1 Extension.
 Simba, Ismail Aden RageMwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameifuta ndoto ya klabu hiyo kuwa na uwanja wake, baada ya kusema haiwezekani uongozi wake kujenga uwanja katika miaka miwili wakati Serikali imejenga Uwanja wa Taifa kwa miaka 50.

Rage alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay huku ukitawaliwa na vurugu zilizosababisha ajenda za muhimu za mkutano kushindwa kujadiliwa kwa kina.

‘’ Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi CCM imewachukua miaka 50 kujenga uwanja wa kisasa ule wa Taifa, sasa mimi Rage na Kamati yangu tutajenga uwanja wa kisasa kwa miaka miwili uwezo huo tunatolea wapi? “alihoji “Vitu vingine vinahitaji kufikiria kwa kawaida tu jamani. Tunaomba muwe wavumilivu tunaenda polepole, lakini kwa uhakika tumeshalipia eneo la ujenzi tunasubiri hati yetu.

Kauli hiyo ilizua majadiliano kutoka kwa wajumbe, lakini Rage aliendelea kusema ‘’nipo kwenye agenda ya saba nyie pigeni kelele tu mimi naendelea (huku akicheka).

Hapa kuna watu wanataka kwenda kuangalia mpira, tena mtaingia bure na vitambulisho vyenu, vya mkutano, Simba oyeeee’’.
Licha ya Rage kutoa kauli hiyo, mwenyekiti huyo amekuwa akitoa...

Akamatwa Akitengeneza Silaha Kienyeji

Jeshi la PolisiKaimu Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ally Mlenge,akizungumza na waandishi wa habari jana.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata majambazi wanane akiwamo mmoja ambaye amebainika kumiliki kiwanda cha kienyeji kinachotengeneza silaha.

Jeshi hilo limemtaja mtuhumiwa anayemiliki kiwanda hicho kuwa ni Charles Masunzu (30), ambaye ni Msukuma na mkazi wa Kawe Mzimuni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamishna wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ally Mlenge, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa na silaha mbalimbali ambazo ni rifle tatu, risasi 36, pingu, mitutu mitano iliyotengenezwa kienyeji, Shortgun, mfuko wa kuhifadhia silaha na maganda 17.

Vitu vingine alivyokutwa navyo ni Pistol KJW works, cocking handle za silaha, ‘house’ ya silaha aina ya Greenel, Magazine iliyounganishwa na tiger guard ya silaha ya aina ya riffle, shortgun moja namba 2539 double bore na vikato vitatu vya silaha.

Aidha vifaa vingine ni meza moja yenye vice clamp kwa ajiri ya kutengenezea silaha kienyeji, mikasi minne ya aina tofauti, mipini mitatu ya silaha aina ya riffle, funguo mbalimbali, nyundo, makufuli, misumeno ya kutengeneza vyuma na vielelezo vingine vinavyohusiana na uhalifu.

Mtuhumiwa alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya unyang’anyi na kusababisha mauaji mengi sehemu mbalimbali. Jambazi huyo ameshikiliwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha, Jeshi la Polisi linawashikilia majambazi wanne waliokutwa na bunduki aina ya SMG iliyosajiliwa kwa namba 02704 ikiwa na risasi 20 ndani ya magazine yake na ikiwa imekatwa kitako.

Baada ya mahojiano na jeshi la polisi, majambazi hao walikiri kujihusisha na matukio ya uporaji na kwamba bunduki hiyo walimpora askari polisi Wilaya ya Rufiji akiwa anasindikiza magari kutoka Ikwiriri Mkoani Pwani mnamo mwaka 2007.

Kadhalika, jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata tapeli aliyejulikana kwa jina la Mfaume Omari (29) mkazi wa Magomeni Kagera, aliyekuwa akitumia majina ya viongozi wa serikali, viongozi wa dini na watu maarufu kujipatia fedha kwa kuvaa uhusika wa majina hayo.

Mlenge alisema, baada ya kufuatilia nyendo za mtuhumiwa, jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa Mchungaji Getrude Rwakatare kuwa jina lake lilikuwa likitumiwa vibaya na mtuhumiwa huyo. Aidha jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa anamiliki simu yenye namba 0659 736 454 ikiwa imesajiliwa kwa jina la Mfaume Saidi Omari na 0659 164 744 ikiwa imesajiliwa kwa jina la Alex Mtenga.
NIPASHE

AdSense Celebrating 10 Years of Shared Success

 AdSense Ten years ago we launched AdSense to help publishers earn money by placing relevant ads on their websites. I can still remember the excitement and anticipation as AdSense went live that first day.
Our small team huddled together in a cramped conference room, and right away we saw that publishers were as excited about AdSense as we were.
Fast-forward 10 years, and AdSense has become a core part of Google’s advertising business. The AdSense community has grown to include more than 2 million publishers, and last year alone, publishers earned more than $7 billion from AdSense. AdSense is a community that thrives because of all the content creators we are so fortunate to partner with. Their stories inspire us to do our part to make AdSense great.

On this occasion, it’s especially inspiring to hear the stories of partners who have been with us since the very beginning—like a retiree in New Zealand who was able to pursue her dream of writing about her garden, a tech support expert in Colorado who can spend more time with his kids, and a theme park reviewer who now sends employees around the world to test and review rides—all thanks to money earned from AdSense.

I look forward to joining several of our partners to share stories from the early days of AdSense, talk about how we’ve all grown since then, and discuss the future for publishers and online advertising. And if you want even more 10th anniversary celebration, just visit our AdSense 10th anniversary page at any time.
by Susan Wojcicki

KILICHOJIRI MAHAKAMANI TABORA KESI YA MUME WA JOYCE KIRIA

 Chadema Tabora Kamanda Mbaruk,
Juzi nikiwa mahakamani Tabora kulia kwangu ni M/Kiti wa Chadema Tabora Kamanda Mbaruk, kushoto ni shemeji yangu Kamanda Bella.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia MAHAKAMA KUU ambapo nilishuhudia jaji akifanya kazi yake kwa busara iliyopitiliza (kwa maoni ya Wakili msomi Peter Kibatala)
Chadema Tabora
Kamanda wangu Mume wangu (kombati nyeusi) na shemeji zangu wakiingia mahakamani jana mjini Tabota.
Masuala ya Mahakamani yanaitaji subira ya hali ya juu hivyo bado naendelea kumfariji Mpenzi wangu Kilewo ya kwamba mambo haya yatapita tu. zaidi ya hapo namwombea sana.
Chadema TaboraKushoto kwangu ni kamanda wa Chadema Tabora (huyu mama) na kulia ni mke mwenzangu (mumewe yupo kesi moja na mume wangu)

Kwa maoni ya Wakili Msomi PK ni kwamba Jaji alichukulia kesi hiyo kwa uzito wake na pia akaheshimu na kuzingatia hali halisi ya Wakili, kwamba anatoka mbali Dar es salaam na hivyo akaamuru Hoja za pande zote mbili zipelekwe kimaandishi kuwaondolea usumbufu hasa wapeleka maombi ambao ni sisi tunaosafiri kila siku. Na kwa sababu hizo basi tar 30july Jaji atataja tar ya uamuzi.
Asanteni sana sana najua mpo pamoja na familia yetu

KAULI YA RAISI MH.KIKWETE KUHUSU KODI YA KADI ZA SIMU

KODI YA KADI ZA SIMU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.
Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
23 Julai, 2013

MAREKANI YAIONYA RWANDA KUACHA MARA MOJA KUWASAIDIA M23

 RWANDA
(Reuters) - The United States on Tuesday called on Rwanda to end support for M23 rebels in neighboring Democratic Republic of Congo, saying there was evidence Rwandan military officials were involved. "We call upon Rwanda to immediately end any support for the M23 (and) withdraw military personnel from eastern DRC," State Department spokeswoman Jen Psaki said.
She declined to say whether Rwandan President Paul Kagame was implicated. "I wasn't speaking to Kagame himself," she added.

The call comes two days before U.S. Secretary of State John Kerry leads a special session of the United Nations Security Council on Africa's Great Lakes region
Psaki said the concerns followed a "credible body of evidence" in a recent report by Human Rights Watch that said M23 rebels in Congo were to blame for executions, rapes and forcible recruitment of men and boys while receiving support from Rwanda.  RWANDA RWANDA
M23 began taking parts of eastern Congo early last year, accusing the government of failing to honor a 2009 peace deal.
(Reporting by Lesley Wroughton; Editing by Doina Chiacu)

ASKARI POLISI WATIMULIWA CHUONI HUKO MOSHI

ASKARI POLISI Wanafunzi 117 wa Polisi, wamefukuzwa katika Chuo cha Taaluma na Mafunzo ya Polisi (MPA), kilichopo Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waliotupiwa virago na kufutwa kwenye kozi hiyo ni wale waliopoteza sifa za kuendelea na mafunzo ya kijeshi baada ya kukutwa na makosa ya utovu wa nidhamu, utoro na matatizo ya kiafya.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matanga Mbushi, ambaye ni mkuu wa chuo hicho aliliambia NIPASHE katika mahojiano maalumu kwamba, waliotimuliwa chuoni ni kati ya askari wanafunzi 3,189 waliokuwa wamesajiliwa kuanza mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho, Oktoba 25 mwaka jana.

Kati yao askari 115 ni wale wa Polisi na askari wawili wanatoka katika Idara ya Uhamiaji iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kufukuzwa kwa wanafunzi hao , kuna akisi moja kwa moja jinsi menejimenti ya chuo hicho ilivyojipanga upya kupunguza wimbi la baadhi ya askari walioko kazini na ambao wanalipaka matope jeshi hilo kutokana na kupotoka kimaadili kwa kutaka kujinufaisha kimaslahi.

Askari hao walikuwa waungane na wenzao ambao wanatarajiwa kuhitimu mafunzo ya awali ya polisi na uhamiaji, Julai 26 mwaka huu baada ya kupatiwa mafunzo ya medani za kivita. Mgeni wa heshima atakayeshuhudia kuagwa kwa askari 3,092 ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Kamishna Mbushi alisema askari hao pamoja na mambo mengine wamepatiwa mafunzo maalumu ya utunzaji wa amani ya nchi iliyopo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Haki za Binadamu, Masuala ya mtambuka (Cross cutting issues), Usimamizi wa majanga na Usimamizi wa kazi za Polisi.

Mafunzo mengine ni pamoja na Polisi Jamii, Sheria ya ushahidi, Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, Upelelezi wa makosa ya jinai, Usalama barabarani na stadi za kazi.

Taarifa za awali kutoka ndani ya chuo hicho, zinaeleza kuwa mahafali hayo ya Polisi yatatanguliwa na medani za kivita yatakayofanyika Julai 25 huko katika Kijiji cha Kilele-Pori, Wilaya ya Siha.
HABARI LEO