Pages

Mhariri Mtendaji wa “Jamhuri” Atiwa Mbaroni, Ahojiwa, Kushitakiwa

Safari ya kupambana na ufisadi katika nchi hii ni ngumu sana.
Leo kuanzia saa 5 hadi saa 8:30 mchana, Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Deo Balile, amehojiwa Makao Makuu ya Polisi kuhusu habari iliyochapishwa kwenye Jamhuri inayohusu “Ufisadi ujio wa marais 11”

Kwa bahati nzuri, habari nzima wanaikubali kwamba ni ya kweli! Kasoro pekee eti ni matumizi ya barua ya Ikulu iliyokuwa na neno “Secret” ambayo ilikuwa na majina tu.

Anashitakiwa kwa kosa la "Kuchapisha Nyaraka za Siri", jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Usalama, kifungu 5(1). Nimemwekea dhamana hadi Ijumaa saa 4 asubuhi.

Angalizo:
Huu ni mwendelezo wa Serikali kukwepa kuwashughulikia wezi na wafujaji wa fedha za umma zaidi ya Sh bilioni 8 kwenye Mkutano wa Smart Partnership, badala yake wameamua kuhangaika na neno moja tu “Secret”. Hivi kweli neno “secret” ni kero na hatari zaidi kuliko hoja yenyewe ya kile kilichoandikwa?
Nawasilisha.
Manyerere Jackton

The Running Man - Arsenal Asia Tour 2013 - Vietnam

When Arsenal FC had their Asia Tour 2013 in Vietnam, there was a beautiful moment captured in the capital city of Vietnam, Hanoi. After their trip to one of the most famous pagoda in Vietnam "Chùa Một Cột", this young Vietnamese guy was running for about 5 miles, chasing the Arsenal bus in Hanoi, he got hit by a tree, the team decided to stop the bus to let him in, signed his Arsenal red and white jersey and took pictures with him as they were chanting to Arsene Wenger "SIGN HIM UP!"
Dreams do come true.

Kocha wa Yanga Kuendelea Kutathmini Viwango vya Wachezaji Wapya.

Kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Ernie Brandts atapata wakati mzuri wa kuendelea kutathmini viwango vya wachezaji wapya wakati kikosi chake kitakapoikabili timu ya three pillars ya Nigeria katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa keshokutwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

After Eating Poisoned Free School Meal, 21 Children Die in India..!

Bihar
Grief ... a dad holds his daughter's lifeless body after she died on way to hospital

Cops are investigating how a lethal dose of insecticide got into the food at a school in the impoverished eastern state of Bihar. One official said the ingredients may not have been properly washed before the meal was cooked.

The children, between the ages of 8 and 11, fell ill on Tuesday soon after having lunch in Gandamal, 50 miles north of the state capital of Patna.
School authorities immediately stopped serving the meal of rice, lentils, soya beans and potatoes when the children began vomiting.

The lunch, part of a popular national campaign to give at least one daily hot meal to children from poor families, was cooked in the school kitchen.
The school cook was also reported to be seriously ill.
Bihar
Victims ... survivors of the poisoning are treated in hospital in Patna
One girl called Savita, 11, told how she got a stomach ache and was sick soon after eating.
“I don’t know what happened after that,” she said at Patna Medical College Hospital, where she and 25 other children are being treated for poisoning.

Ten children are in a serious condition, officials said.
Authorities suspended an official in charge of the free meal scheme in the school and registered a case of criminal negligence against the school headmaster, who fled as soon as the children fell ill.

Angry villagers took the streets in protest, pelting a local police station with stones and setting cars and buses ablaze.

India’s Mid-Day Meal scheme is the world’s largest school feeding programme involving 120 million children across the country.

Dash ... a family takes a sick boy to hospital after a free school meal made him ill
The sun.

Lil Wayne - God Bless Amerika (Official Music Video)


Lunduno The Inc -Baraka za Neema (Video)


Hatimaye Absalom Kibanda Azungumzia Mkasa Wake

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania (TEF), "Absalom Kibanda" amesema zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye, lakini ukweli utabaki kuwa kweli na tukio alilofanyiwa ni la kihalifu, linalotokana na misimamo ya kazi yake.

Aidha amesema kabla ya kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya alikuwa muoga sana na kwamba hakupata kujua kama yeye ni jasiri kwa kiwango hicho.

Kibanda alisema hayo jana wakati akizungumza Dar es Salaam katika kipindi cha Jenerali On Monday na kuongeza kuwa kalamu yake ndiyo iliyomfikisha hapo na kwamba bado atajisemea mwenyewe huku akisema kweli daima.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa New Habari Limited (2006), alijeruhiwa vibaya katika mkasa uliotokea Machi 6, mwaka huu na kumwacha na ulemavu wa jicho, kidole na mifupa kadhaa mwilini kuvunjika.

“Nilikuwa muoga sana kabla ya kupatwa madhala haya, nilikuwa nikiwaza jambo mara mbilimbili na sikupata kujua kama mimi ni jasiri kiwango hiki…kwani hata maneno ya madaktari waliokuwa wakinihudumia yalinifariji kuwa hata shinikizo la damu na sukari viko katika hali nzuri,” alisema Kibanda na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.

Alisema zipo taarifa mbalimbali za kutaka kupotosha ukweli kuhusu yeye lakini ukweli utabaki kuwa kweli na kwamba yapo mambo ambayo atayafanya tofauti na ilivyokuwa awali.

“Katika miezi mitatu niliyokuwa nikipatiwa matibabu nchini Afrika Kusini zipo lugha nyingi za kishabiki ziliandikwa…ni wakati wa kuchunguza kwa kina na kusema ukweli,” alisema Kibanda na kuongeza kuwa leo (jana) ni siku 100 tangu alipofanyiwa tukio hilo, lakini hakuna aliyekamatwa wala kufikishwa mahakamani. Kuhusu kupata ushirikiano katika shauri lake, alisema amekuwa akipata mawasiliano kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo pia viongozi wa ulinzi na usalama wa Taifa ambao wanachunguza suala hilo.

“Maofisa wa polisi wamekuwa wakiwasiliana nami na hata nilipokuwa Afrika Kusini Jeshi la Polisi lilimtuma ofisa wake na alifanya mahojiano nami kuhusu tukio hili,” alisema Kibanda na kusisitiza kuwa ifikie wakati serikali iwe inajali pindi yanapotokea matukio ya aina hiyo.

Aidha alisema tukio alilofanyiwa ni la kihalifu na anaamini kuwa aliumizwa kwa misimamo yake ya kazi, lakini bado anatoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuchunguza tukio hilo.

Kibanda alisema yapo mambo ambayo yalipindishwa kuhusu tukio hilo na kwamba atajisemea mwenyewe.

Akihitimisha kipindi hicho, Muandaaji, Jenerali Ulimwengu alisema matukio kama hayo yanapotokea yana tabia ya kukua, kusambaa na mwishowe kuota meno marefu na kuyaondoa huwa hayawezekaniki tena, hivyo matukio kama hayo yazuiwe yasijirudie.

VOTE FOR SPORAH SHOW

The Sporah Show
The Sporah Show is proud to have been nominated by the British Young Business Awards in the Best Social Enterprise category which will take place on the 12th August 2013.
Please vote for Sporah at
http://www.invinciblebusiness.com/british-young-business-awards/voting/
or you can vote via http://www.sporah.com/

DK. BILAL AKUTANA NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UKIMWI LA KIMATAIFA ABUJA NIGERIA

ABUJA NIGERIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, baada ya mazungumzo yao walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
ABUJA NIGERIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, wakati walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan na baadhi ya Marais wengine baada ya kufunguliwa mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais