Pages

Doctor Who Theme - Doctor Who Prom - BBC Proms 2013 - Video

Murray Gold's version of Ron Grainer's original Doctor Who Theme performed by the BBC National Orchestra of Wales and London Philharmonic Choir conducted by Ben Foster, at the BBC Proms' 50th anniversary celebration of the Doctor Who series.

Kanye West Paparazzi Tantrum REMIX -- D-D-Don't Talk to Me!!! (Video)

DARAJA LA KIGAMBONI LIPO ktk HATUA za MWISHO!

DARAJA LA KIGAMBONI

Victor Wanyama. MKENYA WA KWANZA KUSAJILIWA LIGI KUU YA UINGEREZA

Victor Wanyama Southampton imemsajili mcheza kiungo wa Celtic Victor Wanyama kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili na nusu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye alijiunga na Celtic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, amesaini mkataba wa miaka minne na Southampton.
Wanyama, kutoka Kenya, aliteuliwa kuwa mchezaji bora mchanga katika ligi ya Scottland mwaka uliopita na alifunga bao wakati wa mechi yao ya kuwania kombe la klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona ambayo Celtic iliibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.
Kiasi hicho ndicho cha juu zaidi kwa mchezaji yeyote kuuzwa nchini Scottland.
Wanyama vile vile amevunja rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Kenya kushiriki katika ligi kuu ya Premier ya England.
Kwingineko Swansea imekamilisha usajili wa Wilfreid Bonny kutoka kwa klabu ya Vitesse arnhem ya Uholanzi kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili kiwango ambacho ndicho kubwa zaidi kwa klabu hiyo kumnunua mchezaji yeyote.
Hata hivyo usajili huo utategemea ikiwa mchezaji huyo atapewa kibali cha kufanya kazi nchini England.
Bonny ambaye alikuwa amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya uholansi, alifunga magoli 21 baada ya kucheza mechi 30 msimu uliopita pekee.
Klabu ya Westham vile vile ilikuwa imewasilisha ombi la kutaka kumsajili mchezaji huyo kutoka Ivory Coast lakini Swansea ikafanikiwa kwa kutoa kiasi cha juu.

TAMKO LA AMIRI JESHI MKUU KIKWETE KUHUSU TUKIO LA DAFUR

 Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa sana na tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa vijana saba hodari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokuwa wanalinda amani katika eneo la Darfur, Sudan.
Kwa hakika, Rais amesikitishwa sana na kitendo hicho ambako wanajeshi wengine 14 wa Tanzania wamejeruhiwa na waasi wa Sudan na ametuma salamu za rambirambi za moyoni mwake kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kwa familia za wafiwa wote.
Aidha, Rais Kikwete anaungana na Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Rais pia anaungana na Watanzania wote kuwaombea wale walioumia katika tukio hilo waweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yao ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Katika salamu zake za rambirambi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Adolf Mwamunynge na familia za wafiwa, Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu amesema:
“Sina maneno ya kutosha ya kuelezea mshtuko, huzuni na masikitiko yangu makubwa kufuatia vifo vya vijana wetu hao ambao wamepoteza maisha yao katika shughuli muhimu sana ya utekelezaji wa majukumu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda na kuleta amani katika eneo la dunia ambako maelfu kwa maelfu ya watu wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na waassi.”
Rais Kikwete ameongeza kumwambia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na familia za wafiwa ”Napenda kwa niaba ya Watanzania wenzangu niwahakikishieni kwamba hakuna shaka kuwa vijana wetu hao tokea walipokwenda Darfur Februari mwaka huu, na kwa hakika tokea Tanzania ilipoanza kuchangia walinzi katika eneo hilo mwaka 2007, wamefanya kazi nzuri sana, kazi iliyoongozwa na weledi wa hali ya juu na kazi ambayo imeiletea nchi yetu heshima kubwa. Tutaendelea kuwaenzi kwa kujivunia kazi yao.”
Amesisitiza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza vijana wetu hawa. Kupitia kwao, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa wakuu na maofisa wadogo pamoja na wapigaji wote wa Jeshi letu kwa kupotelewa na wenzao. “
“Aidha, kupitia kwako, nawatuma salamu zangu kwa wanafamilia za waliopotelewa na wapenzi wao na ndugu zao katika tukio hilo. Wajulishe kuwa naungana nao katika kuomboleza. Wajue kuwa uchungu wao ni uchungu wangu pia na wa Watanzania wote na kuwa kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu. Vile vile kwa pamoja tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze peponi roho za marehemu. Amina.’
Kwa walioumia, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Naungana pia na Watanzania wenzangu katika kuwapa pole nyingi walioumia katika tukio hilo tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka na kuendelea na shughuli zao za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.”
Vijana hao waliopoteza maisha yao na walioumia, walikuwa sehemu ya askari 37 na ofisa mmoja ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa waangalizi wa kijeshi katika Darfur kutoka eneo la Khorabeche kwenda Nyara waliposhambuliwa na waasi kiasi cha kilomita 20 kutoka Khorabeche saa tatu asubuhi jana, Jumamosi, Julai 13, 2013

CHADEMA Waibuka Kidede Arusha

CHADEMA ,ArushaChama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo kimeweka historia baada ya kufanikiwa kushinda kata zote nne katika uchaguzi wa madiwani uliofanyika mjini Arusha,uchaguzi huo ulizihusisha kata za Elerai, Themi, Kaloleni na Kimandolu . Habari kutoka kwa watu walio eneo la tukio wameweza kutujulisha kuwa hadi sasa CHADEMA wamefanikiwa kutwaa ushindi kwenye kata zote nne kama inavyoonekana hapo chini.....
 
ELERAI
CHADEMA - 1,715
CCM - 1,239
CUF - 213

THEMI
CHADEMA - 678
CCM - 326
CUF - 313

KALOLENI
CHADEMA - 1,019
CCM - 389
CUF - 169

KIMANDOLU
CHADEMA - 2,665
CCM - 1,169
CUF - 0

Le Profeseri - Utafiti Kwenye Mwili wa Mtu (Orijino Komedi)

Talk Show Celebrity Oprah Winfrey in Serengeti National Park

Television talk show celebrity Oprah Winfrey
One of the world’s recognised Television talk show celebrity Oprah Winfrey is touring Serengeti National Park for what is described as private excursion.
The woman behind the popular ‘Oprah Winfrey’ shows, Oprah, who is also a famous film actress and currently playing the role of Gloria Gaines in the 2013 movie ‘The Butler,’ is reportedly, going to be in or around the Serengeti National Park for the whole week starting this weekend.
“It is going to be Oprah’s private tour,” admitted Mr Paschal Shelutete the Public Relations Manager for Tanzania National Parks (TANAPA) which manages Serengeti, the country’s second largest National Park, but which is also the most known.

Her private excursion in the Serengeti, however, won’t prevent Oprah from meeting and hold talks with the Deputy Minister for Natural Resources and Tourism, Mr Lazaro Nyalandu who is also flying to Serengeti to welcome the pop-culture doyenne and founder of television talk shows media genre.

Ever since she debuted in the 1985 film, ‘Colour Purple’ Oprah has starred in 28 other movies in addition to producing several Television Documentaries and publishing three books.

Whether we should expect her next film or TV documentary to be filmed in Serengeti is yet to be seen but the country’s popular Park, home to the legendary migration of over 2 million wildebeests and Zebras, the queen may be interested to capture a bit of the spectacular show.

Winfrey has remained the only African American to rank among America’s 400 richest people nearly every year since 1995. With a net worth of US $800 million, Winfrey is believed to be the richest African American of the 20th century.

She has also won, and nominated for, various outstanding awards including the ‘Academy Awards,’ ‘Emmy awards,’ ‘Golden Globe Award,’ ‘PGA Awards’ and got named as best talk show presenter and host several times.

Winfrey has remained the only African American to rank among America’s 400 richest people nearly every year since 1995 and is believed to be the richest African American of the 20th century.

She is also generous because in 2004, Winfrey became the first black person to rank among the 50 most generous Americans and she remained among the top 50 until 2010. By 2012 she had given away about US $400 million to educational causes.
Tanzania Daily News/ Bizu/WENN

Uchaguzi Mdogo wa Madiwani Arusha Wageuka Vurugu Tupu

Uchaguzi mdogo katika kata nne za Jiji la Arusha unafanyika leo, huku Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ikiwapiga marufuku Mkuu wa Mkoa, Magessa Mulongo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella kuingia kwenye vituo vya kupigia kura, wala kujihusisha kwa namna yoyote na zoezi la upigaji kura ikisema siyo jukumu lao kisheria.

Mbali ya NEC kupiga marufuku viongozi hao wa kisiasa kukaribia vituo hivyo, uchaguzi huo umekumbwa na matukio kadhaa likiwamo la Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa Chadema(Bavicha), John Heche, kunusurika kuswekwa rumande jana.

“RC na DC hawana haki wala mamlaka ya kujihusisha kwenye zoezi na shughuli za upigaji kura. Mwenye dhamana, wajibu na haki ya shughuli zote za upigaji kura ni Mkurugenzi wa Jiji ambaye ni mwakilishi wa NEC pamoja na maofisa wengine wanaotambuliwa kisheria,” alisema Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva jana.

Lema na Heche walinusurika kuswekwa rumande baada ya kufika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha, wakishinikiza jeshi hilo, kukamata magari matatu waliyodai kuwa ni ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na kubadilishwa namba yakihofiwa kwamba huenda yakatumika kuvuruga uchaguzi wa leo.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea jana asubuhi baada ya viongozi hao, kufika polisi na kutoa taarifa hiyo, wakieleza kuwa lakini waliambiwa waondoke kwa kuwa gari kubadili namba siyo kosa ambapo pia walitakiwa kumtaja aliyewaeleza kama magari hayo yatatumika kufanya uhalifu.

Aidha, viongozi wa vyama vyote vya siasa ambao sio mawakala wala wagombea, wamepigwa marufuku kuingia kwenye vituo vya kupigia kura, wala kujihusisha kwa namna yoyote na zoezi la upigaji kura badala yake wakiwa ni wakazi wa kata husika kupiga kura na kuondoka maeneo hayo.

Mwenyekiti wa NEC, alitoa tamko la kuzuia viongozi hao jana alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea mipango na mikakati ya tume yake katika kufanikisha zoezi hilo linalofanyika baada ya kuahirishwa mara mbili.

Mbele ya makamu wake Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Jaji Hamid Mohamoud Hamid, Jaji Lubuva alitaja orodha ya watu 12 wenye haki kisheria kuingia kwenye vituo vya kupigia kura na kujihusisha na zoezi la upigaji, kuhesabu, kujumlisha kura kuwa ni msimamizi wa kituo, msimamizi msaidizi wa kituo, mawakala wa vyama na wapiga kura.

Wengine ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, mgombea, mjumbe wa NEC, Ofisa wa NEC, Mratibu wa NEC mkoa, askari polisi au mtu yeyote anayehusika na usalama katika kituo cha kupiga kura, mtu anayemsaidia mpigakura asiyejiweza na mwangalizi wa uchaguzi aliyeidhinishwa na NEC kimaandishi na katika utaratibu uliowekwa.

Uchaguzi huo unafanyika leo baada ya kuahirishwa Juni 16, mwaka huu, baada ya bomu la kutupa kwa mkono kulipuka kwenye mkutano wa Chadema wa kufunga kampeni kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.

Agizo la kupiga marufuku kujihusisha na Uchaguzi Mkuu wa Mkoa(Mulongo) na Mkuu wa Wilaya(Mongella) ambao ni makada na wajumbe wa Kamati za Siasa na Halmashauri za Mkoa na Wilaya za CCM, limekuja wakati kukiwa na tuhuma kutoka kwa vyama vya upinzani, hasa Chadema kuwa wanatumia nyadhifa zao kukibeba chama tawala.

Akizungumzia kunusurika kuwekwa rumande, Heche alisema kutokana na majibu ya polisi wao wakiomba wapewe hata fursa ya kuandika maelezo kuhusu tukio hilo au wapewe polisi kwenda kuzikamata gari hizo, lakini waligomewa, ndipo likatolewa agizo la kukamatwa kuwekwa rumande kwa Lema.

“Mimi niligoma nikasema kwa nini akamatwe wakati tunaleta wote taarifa hapa basi watukamate wote, jukumu la polisi ni kuchunguza kwa kuwa sisi tuna taarifa magari hayo yatatumika kuteka vijana wetu na kuvuruga uchaguzi,”alisema Heche.

Alitaja magari hayo (namba tunazo) kuwa moja ni la CCM Wilaya ya Arusha na magari mengine mawili.

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa alisema kuwa wanashangazwa na polisi kukataa kukamata magari hayo na kwamba katika uchunguzi wao wamebaini moja ya namba mpya za magari hayo ni za moja ya kampuni ya nje ya Arusha.
“Tumeshangaa, badala ya polisi kuchunguza wanataka kukamata viongozi wetu, kweli hii ni halali?”alihoji Golugwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo, baada ya simu yake kupigwa bila majibu huku ikielezwa kuwa alikuwa wilayani Monduli katika sherehe za kutoa kamisheni wanajeshi wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi Monduli(TMA), ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwapo na viongozi wengine.

NEC ‘yahamishia’ ofisi Arusha
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), ‘imehamishia’ kwa muda ofisi zake jijini Arusha kuhakikisha zoezi la kura katika Kata za Themi, Kimandolu, Elerai na Kaloleni linafanyika kwa ufanisi.

Pamoja na Mwenyekiti wa wa NEC, Makamu wake, makamishna wanne na Mkurugenzi wa NEC, Julius Mallaba pia wapo Arusha kusimamia zoezi hilo.

Makamishna wa NEC waliopo Arusha ni Jaji wastaafu John Mkwawa, Mary Longway, Profesa Amon Chariga na Mchaka Mchanga, walioambatana na watendaji kadhaa wa tume hiyo kutoka Dar es Salaam.

Akijibu swali la kwa nini wote wako jijini Arusha, Jaji Lubuva alisema wingi na uwepo wao umetokana na hali na mazingira halisi ya siasa za Jiji la Arusha kwa kuzingatia sababu za uchaguzi huo kuahirishwa mara mbili Juni 16 na 30, mwaka huu.

“Pamoja na ukweli kwamba Mkurugenzi wa Jiji ndiye msimamizi wa uchaguzi akisaidiana na watendaji wengine, mimi na makamishna wengine wa NEC tuko hapa kwa ajili ya kusimamia utendaji, kutoa ushauri na ufafanuzi kwa karibu zaidi pale jambo lolote linapojitokeza,” alisema Jaji Lubuva.

Wapiga kura kutoruhusiwa kukaa karibu na vituo vya kura
Akizungumzia maandalizi na taratibu zitakazotumika leo, Jaji Lubuva alisema wapiga kura wanashauriwa kurejea nyumbani kusubiri matokeo mara baada ya kupiga kura, badala ya kukaa karibu na vituo ili kuepuka mikusanyiko kutokana na Jiji la Arusha kukumbwa na milipuko ya mabomu.

Hata hivyo, wakati Jaji Lubuva akiwataka wananchi kuepuka mikusanyiko kwa hofu ya mabomu, mkutano mkubwa wa Injili unaohubiriwa na Askofu Emanuel Lazaro unaendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Karatasi za kura na fomu za matokea zabadilishwa rangi
Kutokana na zoezi la kupiga kura Arusha kuahirishwa Juni 16, mwaka huu baada ya karatasi za kura na fomu za matokeo kusambazwa, Jaji Lubuva alisema NEC imebadilisha rangi za karatasi hizo na fomu za matokeo kuepuka udanganyifu na hujuma yoyote.

Taarifa zinasema NEC imelazimika kubadilisha karatasi za kura na fomu za matokeo baada ya baadhi ya karatasi za kura za awali kudaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hazipatikana hadi leo.

Kauli ya Chadema kuhusu wapigakura kurejea majumbani
Chadema kimekataa ushauri wa NEC wa kutaka wananchi kurejea nyumbani baada ya kupiga kura, badala yake kimesisitiza kuwa wafuasi wa chama hicho watakaa umbali wa zaidi ya mita 100 kutoka vituo vya kupigia kura kama sheria inavyoelekeza.
Mwananchi

Sheikh wa Wilaya Arushiwa Tindikali

ArushaArusha. Wakati vumbi la matukio ya kigaidi ya milipuko ya bomu kanisani na kwenye mkutano wa kampeni za Chadema halijatulia, tukio lingine linalohusishwa na ugaidi limetokea wilayani Arumeru kwa Sheikh wa wilaya hiyo, Said Juma Makamba aliyejeruhiwa kwa kumwagiwa usoni kimiminika kinachoaminika kuwa tindikali.

Sheikh Makamba anayekaimu nafasi hiyo alikutwa na hayo kati ya Saa 4:00 hadi 5:00 usiku wa kuamkia juzi akitoka kusali Tarawei na alilazwa wodi namba nne katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu.

Jicho la kushoto la Sheikh huyo limeathirika, huku akiwa amebabuka na kuvimba usoni, kifuani, mkono wa kushoto na mgongoni.

Akizungumza kwa taabu kitandani kwake alikolazwa, Sheikh Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei wilayani Arumeru alisema alimwagiwa tindikali muda mfupi baada ya kurejea nyumbani kwake akitoka kuswali.

“Nilipotoka Msikitini, nilisindikizwa hadi nyumbani na vijana wawili nilioongozana nao kutoka msikitini ambao walihakikisha nimeingia ndani salama. Lakini kabla ya kulala nilitoka nje kwa ajili ya kujisaidia kwenye choo cha nje ndipo nilimwona mtu amesimama pembeni ya nyumba nikiwa najitahidi kumwangalia ili nimtambue, ghafla alinimwagia kitu cha majimaji usoni,” alisema Sheikh Makamba.

Ingawa hataki kuingia kwa undani kuhusu anaowatuhumu na sababu za kumwagiwa tindikali, Sheikh Makamba alisema anadhani jambo hilo linatoakana na ugomvi wa madaraka msikitini hapo.

Katibu wa Bakwata Wilaya ya Arumeru, Sheikh Yahaya Husein Mwangela aliwaomba polisi kuchunguza tukio hilo ili kuondoa hofu miongoni mwa viongozi wa Bakwata.

Hili ni tukio la pili kwa viongozi wa Bakwata Arusha kumwagiwa tindikali baada ya Oktoba mwaka jana, Katibu wa Baraza hilo Mkoa wa Arusha, Abdukarim Njonjo kulipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu. Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa hadi juzi kulikuwa hakuna mtu aliyekamatwa.

ri imeanza upelelezi na uchunguzi wa kina wa tukio hilo kubaini wahusika.
Hadi jana jioni, hakuna mtu aliyekuwa akishikiliwa polisi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
Mwananchi