Pages

Uhuru Kenyatta on Churchill Live

Mama Ntilie Jijini Dar Wanatumika Kuuza Dawa za Kulevya

Mama Ntilie Dar es Salaam. Biashara ya dawa za kulevya nchini inazidi kuchukua sura mpya ambapo sasa wanawake wanaouza vyakula, maarufu mama ntilie, hutumika kusambaza dawa hizo kwa wateja.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa muda mrefu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam unaonyesha kuwa biashara hiyo inafanyika katika maeneo ya Tandika, Manzese, Vingunguti, Temeke, Tandale, Mtongani na Keko.
Wanawake hao wamekuwa wakitumia mwanya wa kuuza chakula kama kinga yao, huku biashara yao kubwa ikiwa ni kuuza dawa za kulevya aina ya heroin, bangi na aina nyingine.

Mbinu hii mpya ya usambazaji wa dawa za kulevya kwa kutumia wanawake wanaouza vyakula imeelezwa kuwa inawasaidia wahusika wakuu, kuendesha biashara yao kwa ufanisi zaidi.

Uchunguzi umeonyesha kuwa wafanyabiashara wa dawa hizo wameamua kuwatumia mamalishe kutokana na kuwa waaminifu na kuhudumia wateja wengi, hivyo ni vigumu watu kuwashtukia wakiwamo askari polisi.

Imebainika kuwa dawa hizo huuzwa kulingana na maeneo, wakati maeneo ya watu wasiokuwa wa uwezo hupimwa kwa kutumia kipimo kidogo zaidi kwa bei ya chini ambayo watumiaji husika huweza kuimudu.

Aidha dawa hizo hufungwa katika mitindo miwili tofauti, ukiwa katika unga wa vidonge na wa kawaida ingawa bei zake hazitofautiani sana.

Uchunguzi unaonyesha kuwa vidoge huuzwa vikiwa vizima au vipande, huku unga wa kawaida ukiuzwa kwa kipimo maalumu.

Kwa kawaida ‘unga’ huo huuzwa kwa Sh1,000 kwa pointi huku kete moja ikiuzwa kwa Sh2,000, wakati vidonge, kizima huuzwa kwa Sh2,000, huku kipande huuzwa kwa Sh1,000 zikitofautiana kulingana na maeneo.

Gazeti hili lilifanikiwa kuongea na baadhi ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Asha (28) ambaye siyo jina lake halisi ni muuzaji mkubwa wa dawa hizo. Awali alikuwa akifanya shughuli zake hizo za uuzaji katika maeneo ya Yombo Kilakala, ingawaje hivi sasa amehamia Temeke.

“Unajua siku zote dhumuni la kufanya biashara ni kupata faida, hivyo naweza kusema niliingia kwenye biashara hii kwa sababu tu ina faida zaidi kuliko biashara nyingine,” anasema.

Awali alikuwa akiuza vyakula huku akifanya biashara hiyo ya kuuza dawa, baadaye akaacha kuuza vyakula akabaki na biashara ya dawa za kulevya.

Akielezea namna anavyofanya biashara yake hiyo, Asha anasema kwa kawaida huwa ananunua mkanda ambao unakuwa umefungwa vidoge vidogovidogo kumi hadi ishirini. Mara nyingi huuza kulingana na mahitaji ya mteja.
“Halafu baada ya kununua hivyo huwa nauza kidogokidogo vidonge hivyo.

Kwa kawaida kidoge kimoja huwa nauza kati ya sh1,000 hadi Sh2,000. Bei yake hutegemea na mahali unapouzia. Kama unauzia watu waliochoka sana inabidi upaki kidogokidogo ili kuweza kuliteka soko lao,” anasema.
“Nimefanya biashara hii kwa muda wa miaka mitatu, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa nimefanikiwa kwa kiasi fulani. Nimeweza kujenga nyumba ya kwangu mwenyewe, pia kuhudumia familia yangu. Licha ya kuwa na madhara kwa watu, lakini ukweli ni kuwa biashara ya unga inalipa,” anasisitiza.

Abubakari Ismail (33) aliyewahi kutumia dawa za kulevya, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa kupambana na dawa hizo kinachofahamika kama Use Ant -Drugs, kilichopo Yombo, wilayani Temeke, anasema kuwa tatizo la wanawake kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya linachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha mapambano dhidi ya dawa hizo hususan kwa vijana.

‘Joseph (17)’, siyo jina lake halisi ni kijana aliyekuwa katika matibabu kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Hivi sasa kijana huyu amelazimika kuhama nyumbani kwao kutokana na kumkimbia mama yake mzazi ambaye anajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Kituo cha Makangarawe Youth Information Center cha jijini Dar es Salaam, kinachojishughulisha na miradi kadhaa ya vijana ikiwamo mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa vijana, Ismail Mnikite, amesema kitendo cha wanawake kushiriki katika uuzaji wa dawa za kulevya ni tatizo jipya linalochangia kukwamisha juhudi za mapambano hayo.
Mwananchi

Mashine ya Kupima Ujinga

Ujinga

Video Pritenda ya Wiki Hii (Censored)

MAREKANI KUTOA NDEGE ZA KIVITA MISRI

Ndege ya kivita F-16 Marekani inaendelea na mpango wake wa kutoa ndege za kivita kwa jeshi la Misri licha ya msukosuko wa kisiasa unaokumba nchi hiyo. Hatua hii inajiri wakati Marekani ikiendelea kutathmini matukio ya wiki jana ambapo jeshi lilimuondoa madarakani Rais Mohammed Morsi.

Msaada wa kijeshi kwa Misri ungesitishwa endapo Marekani ingelitaja matukio ya wiki jana kama mapinduzi ya kijeshi. Kundi la Muslim Brotherhood linalomuunga mkono Morsi linasisitiza arejeshwe madarakani.

Wafuasi wake wamekua wakiandamana karibu na kambi kuu ya jeshi ambapo anaaminika kuuzuiliwa. Hapo Jumatatu,wafuasi wa Brotherhood 51 waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi wakati wanakabiliano.

Utawala wa mpito umesema kwamba Bw. Morsi anazuiliwa eneo salama na kwamba haki zake zinazingatiwa. Maafisa wa Marekani wamesema ndege mpya za kivita aina ya F-16 zitawasilishwa katika wiki chache zijazo.

Mpango wa kufadhili jeshi ulianza kutekelezwa mapema mwaka huu na jeshi linatarajia kupokea ndege 20 za kivita. Msemaji wa ikulu ya Rais amesema Marekani haitabadilisha mpango wa kufadhili jeshi la Misri, japo inaendelea kutathmini kuhusu matukio ya kisiasa. Msaada wa kijeshi nchini Misri ambao hutolewa na Marekani hufikia dola bilioni 1.3 kila mwaka.

Hapo Jumanne, kibali cha kumkamata kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohamed Badie kilitolewa pamoja na wakuu wengine tisa wa kundi hilo. Viongiozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia mjini Cairo ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa na mamia kujeruhiwa.
BBC Swahili

FUTARI YA PAMOJA KWA MWEZI WA RAMADHANI - DMV

 
Uongozi wa Tanzanian Muslim Community in Washington DC Metro(TAMCO) unawakaribisha na kuwajulisha kuwa tutaanza kufuturu pamoja jumamosi na jumapili hii pamoja na weekend zote za mwezi wa ramadhani.
Tunaombwa tuudhurie na tuwajulishe wengine wote:
Saturday, July 13, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Sunday, July 14, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Saturday, July 20, 2013
Sligo-Dennis Avenue Local Park
Sunday, July 21, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Saturday, July 27, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Sunday, July 28, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Saturday, August 03, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park
Sunday, August 04, 2013
Indian Springs-Terrace Local Park

Address ni:
Indian Spring- Terrace Local Park
9717 Lawndale, Silver Spring, MD 20901
Sligo – Dennis Avenue Local Park
10200 Sligo Creek Pkwy, Silver Spring, MD 20902
Karibuni
Uongozi
TAMCO
http://www.tamcousa.org/

LIL TWIST ARRESTED IN CALIFORNIA FOR DUI !!

JUSTIN BIERBER
 YOUNG MONEY RAPPER LIL TWIST WITH JUSTIN BIERBER

 HE WAS ARRESTED EARLIER THIS YEAR FOR CAUSING ACCIDENT WHILE DRIVING THE SAME JUSTIN BIERBER FERRARI
LIL TWIST
Lil' Twist Arrested For DUI in California Early This Morning While Driving Justin Beiber Ferrari!! When officers approached the car, they believe Twist appeared to be under the influence of a substance ... but we're told he DID NOT appear to be drunk.

NEW UPDATE:
Lil Twist was driving Justin Bieber's car while under the influence of marijuana ... and he even had a LIT BLUNT in the car at the time of his DUI arrest, law enforcement sources said. We broke the story ... 20-year-old Twist was busted in Calabasas around 3:30 AM Thursday morning on his way to Bieber's house.
Twist was hauled to a nearby station, where he was booked ... and was later released after roughly 8 hours in custody.
As he left the Sheriff's station, Twist didn't have much to say to us. We're guessing he'll be more talkative when he explains himself to JB.

SERIKALI IMETANGAZA KIMA CHA CHINI MISHAHARA YA KISEKTA.

KIMA CHA CHINI Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo wakifuatilia mawasilisho ya bajeti yao Bungeni mjini Dodoma

DAR ES SALAAM.
SERIKALI imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyum
bani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao.

Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha.

Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000.

“Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo.
Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi.

Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000.
Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000.

Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000.

Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000.

Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000.
Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000.
MWANANCHI

Tanzania Kufaidika na Trilioni 1.4 Kutoka Sweden

Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es salaam
Lennarth Hjelmaker
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es salaam. (Picha na Ikulu)
------------------------------------------
TANZANIA itafaidika na mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaogharamiwa na Serikali ya Sweden utakao gharimu kiasi cha T.Shs trilioni 1.4 kupitia kitengo chake cha Swedish International Cooperation Agency (SIDA).

Balozi wa Sweden hapa nchini, Lennarth Hjelmaker amemueleza Rais Jakaya Kikwete leo Ikulu ambapo amefika kumkabidhi Rais barua kutoka kwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Sweden Mheshimiwa Gunilla Carlsson, ambaye amemuandikia Rais Kikwete barua maalum kumjulisha kuhusu mpango huo ambao serikali ya Sweden utaugharamia.

Mpango huo wa maendeleo wa 2013-2019 unalenga katika maeneo makuu matatu:-
Kuongeza ajira, kuendeleza sekta ya nishati na masoko kwa mazao ya kilimo; Elimu ambapo kipaumbele kitakuwa katika kuwapa elimu ya awali watot wengi zaidi na pia katika vyuo vya ufundi; Kukuza demokrasia, uwajibikaji na uwazi pamoja na kuongeza uelewa wa haki za binadamu nchini.

Katika barua yake kwa Rais Kikwete, Waziri Carlsson amemueleza Rais Kikwete kuwa Tanzania itaendelea kuwa mwenza muhimu kwa nchi ya Sweden.

“Huu si ushahidi wa ushirika wetu wa kihistoria, bali pia ni kwa ajili ya sera za Tanzania na ukuaji wa taasisi za kidemokrasia nchini Tanzania” amesema waziri Carlsson na kuongeza kuwa “Wakati uhusiano baina ya nchi hizi mbili ni muhimu, mahusiano yetu ya baadaye yataimarika zaidi sio kwenye misaada bali katika uwekezaji” ameongeza.

Rais Kikwete ameishukuru Sweden kwa msaada huo na kueleza kuwa nchi zinazoendelea kwa hakika zinahitaji misaada ya maendeleo ili kujijengea uwezo na hatimaye kufikia kwenye uwekezaji ambao utaharakisha maendeleo ya nchi hizi.

KWELI NIMEKAMATWA SAUZ: MASOGANGE

Agnes Gerald ‘Masogange’
.Na Mwandishi Wetu
HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi, Ijumaa linakupasha.

AWALI YA YOTE
Mwishoni mwa wiki iliyopita, habari ya mjini ilikuwa Masogange kanaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Habari zilisambaa kwamba sanjari na Masogange, mwingine aliyenaswa naye ni mdogo wake (mtoto wa mama yake mdogo Agnes) aitwaye Melisa Edward.

Kwa mujibu wa habari hiyo ya mjini, wawili hao walinaswa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oriver Tambo uliopo Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania wakiwa na ‘mzigo’ wa kilo nyingi aina ya ‘crystal methamphetamine’ wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 6.8!
Melisa Edward Melisa Edward aliyekamatwa na Agnes.

IJUMAA LAANZA KUSAKA UKWELI
Baada ya kunasa habari hiyo, Ijumaa liliingia mzigoni kuusaka ukweli ambapo hata hivyo, madai hayo yalikuwa yakijifungafunga sana.
Mtu mmoja wa karibu na Masogange alipoulizwa kuhusu ukweli au uongo wa habari hiyo alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli Agnes amekamatwa akiwa na madawa ya kulevya kule Sauzi. Lakini si yenye thamani hiyo ya bilioni sita bali ni milioni arobaini tu. Hata hivyo, ameachiwa kwa dhamana ila paspoti yake imezuiliwa.
“Nadhani kuna mambo yanawekwa sawa ikiwezekana atarudi nyumbani.”

JIJINI DAR, KAMANDA WA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ANENA
Jumatatu iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliviambia vyombo vya habari kuwa, Watanzania wawili walikamatwa nchini Afrika Kusini na mamlaka ya mapato wakiwa na madawa ya kulevya kutoka Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.

Kamanda Nzowa aliwataja Watanzania hao kuwa ni Agnes Gerald ambaye ana miaka 25 na Melisa Edward mwenye miaka 24. Alisema wawili hao baada ya kukamatwa na chombo hicho walikabidhiwa kwa polisi ambapo mahojiano yanaendelea.

IJUMAA LAMWIBUKIA KAMANDA NZOWA
Baada ya Kamanda Nzowa kuwataja kwa majina wawili hao Jumatatu iliyopita, siku iliyofuata, Ijumaa lilipiga hodi kwenye ofisi za kamanda huyo kwa lengo la kutaka kujua kama Agnes Gerald aliyemtaja jana yake ni Masogage au majina yanafanana tu.
Kamanda huyo hakuwepo ofisini kwake asubuhi hiyo na kwa mujibu wa wasaidizi wake, alikuwa kwenye kikao cha dharura kwenye Ofisi za Polisi wa Kimataifa ‘Interpol’.

APIGIWA SIMU
Ilibidi Ijumaa limsake kwa njia ya simu ya kiganjani kwa mara kadhaa. Alipopokea akaulizwa kuhusu Agnes Gerald aliyemtaja kama ni Masogange yule staa.
Kamanda Nzowa: “Eee, mimi siwezi kusema ni huyo, ninachojua ni Agnes Gerald tu basi. Sasa kama ni Masogange mimi sifahamu lolote.”

JUMANNE USIKU SIMU KUTOKA SAUZI
Mpaka hapo, timu nzima iliyokuwa ikifuatilia habari hiyo haikuona ukweli wa Agnes Gerald kuwa ni Masogange na kwa vile siku zote Global Publishers inasimamia utafiti kabla ya kuandika habari iliamua kuiweka pembeni kwanza ili kuendelea kuichimba.
Saa 2:14 usiku wa siku hiyo, Ijumaa lilipokea simu yenye kuashiria wito (code number) ni ya nje na kabla haijapokelewa, ilibainika ni ya Afrika Kusini.
Ijumaa: Haloo.

Sauti: Haloo, mimi Masogange.
Ijumaa: Mambo Agnes, pole sana na mkasa uliokupata bwana, pole sana.
Agnes: Kwanza naumizwa sana na maneno ambayo watu wanazidi kuyaeneza sehemu mbalimbali bila kuwa na uhakika wowote, mimi sikukamatwa kwa sababu ya madawa ya kulevya.

“Mkasa nilioupata siyo ambao watu wanaueneza kwenye mitandao mbalimbali na katika vyombo ya habari.”
Ijumaa: Kwa hiyo madai ya kukutwa na madawa ya kulevya si ya kweli?
Agnes: Kweli nilikamatwa huku kwa matatizo f’lan ila siyo ishu ya madawa kama watu wanavyosambaza.
Ijumaa: Ni tatizo gani sasa?

Agnes: Unajua sipendi tena kuwapa watu faida ila lilikuwa ni tatizo la kawaida, nilikamatwa na baada ya hapo nilitoka na niko huru. Nasubiri tu kwenda mahakamani Ijumaa (leo) mara moja kisha n’tarudi Bongo.
Ijumaa: Mh! Sasa Egg, mbona huku mpaka viongozi wa polisi wamesema ni madawa?
Agnes: Hapana, siyo, ipo ishu ndogo tu.
Ijumaa: Haya pole sana kwa misukosuko.
Agnes: Asante sana, nitakuja huko siku si nyingi.
GPL