Pages

PICHA ZA MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGA VIWANJA VYA MSASANI CLUB DAR ZIKO HAPA

Afande Sele Afande Sele akiimb kwa hisia kali
 Oooi. usiogope jamaa hapigwiiii ila ni mizuka ya battle man 2 man
Kundi la Kiokosi cha Mizinga limefanya show ya kutimiza miaka 13 tangu lianzishwe
Show hiyo iliyo hudhuliwa na mashabiki kibao wa hip hop wa Jijini Dar es salaam.
Onyesho hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudhuliwa na wasanii wa muda mrefu sana waliopotea katika mziki huo wakiwemo Member wa Kundi la Wateule,Mark 2 Be aka Simba wa kundi la Big Dogg Poz, Chidi Benz... Man 2 Man Battle Hakupigwa mtu, sema ooi...
KalapinaKalapina akifanya mambo kwenye stegi
Chidi BenzChidi Benz ndani ya nyumba
Kalapina Mashabiki wakiwa mzukaa mbaya
Kalapina
Man 2 Man Battle
MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGAKumbukumbu Muhimu Mwana

SongaSonga akiwa kwa steji akifanya yake
MIAKA 13 YA KIKOSI CHA MIZINGA Mashuati Mashuati kwenye stage wakionyesha ujuzi wa karate raha kwelii Man 2 Man Battle Haya sasa Man 2 Man Battle nichane nikupasue Man 2 Man Battle

Na Huu Ndio Ukweli Kuhusu Wimbo “YAHAYA” Wa Lady Jaydee

YAHYA: A New TAPELI In ARUSHA
Katika kusikiliza wimbo mpya ya mwanadada LADY JAYDEE uliotoka hivi karibuni ukitambulika kwa jina YAHYA, nikaona kama ina ukweli fulani ndani yake na ndipo nilipoamua kumuuliza muhusika na kunijibu kuwa Yahya ni wimbo alioutunga kutokana na tabia za baadhi ya watu tunaoishi nao katika maisha yetu ya kila siku na maisha yao ni uongo wa kusabisha utapeli kwa watu na mali zao akiwemo huyo YAHYA.
Katika pitapita na uchunguzi, GongaMx TEAM imegundua kuwa YAHYA yupo na anaendelea na mambo yake ya utapeli na uongo baada ya kufuma taarifa kwenye mtandao wa jamii wa Facebook iliyoandikwa na Mr. JOHN wa huko Arusha kuwa YAHYA aka HISBERT akimtambulisha kama “A New TAPELI IN ARUSHA” kuwa amefanikiwa kukutana na YAHYA na ameweza kuhadithia aliyokutana nayo baada ya kukutana nae.
JOHN: I met this guy last night in the Heineken UEFA final @ Mango Tree,,, He just came and show up to us and introducing himself as a Immigration Officer from dar es salaam and he is in Arusha for special Task, especially for us MUZUNGU who lives here since most of us are illegal here. He told us not to tell anyone that we met him and he wanted to meet us next day >TODAY> for lunch because he had our files and we were the target by Immigration of Tanzania.
He left us the business card with his contact. I really wanted to meet him today since i was so curious to hear the story behind us.
Luckily,,, When i woke up this morning i just decided to Google him, since i had his name on business card. What i find on Google was all off his criminal record from PCCB (Prevention and Combating of Corruption Bureau), I was really shocked and i decided to share this with my fellow Arusha People. Be aware of this guy he is known as HISBERT KIJJAH.
HISBERT KIJJAH.Tip: He speak very broken English,, am not sure if this guy has finished Primary School, He is Muscled, And he is told me that he is a trainer in a GYM @ NJIRO COMLEX,, am not sure if he was true.
I attach the link and some photos of him so you will not be the next victim.
You can even find him on Facebook known as Hisbert Khijjah or you can Google him by the name of Hisbert Kijjah.
Best regards.
JOHN.
Please share this to keep Arusha the best place.
Last night @ Mango tree,,u can even see my friends behind him
 Prevention and Combating of Corruption Bureau . As The trainer at the GYM in Njiro Complex.
Businessman Hisbert Mbega Kijjah is charged on false pretence to be an officer of the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), contrary to section 36(a) of PCCA No. 11 of 2007. The charge was read over to the accused on June 7th, 2010 at Kisutu Magistrate Court. The case will come for Mention on January 5th, 2011at Kisutu Magistrate Court.
GongaMx

CUF Kuandamana Jumamosi Kwenda Ikulu

Na Romana Mallya
23rd June 2013
Chama cha Wananchi (CUF), kimeandaa maandamano ya amani Jumamosi ijayo kuelekea Ikulu kwa lengo la kumfikishia malalamiko Rais Jakaya Kikwete, kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanywa na jeshi la polisi na JWTZ huko Mtwara.

Pia maandamano hayo yamelenga kumtaka Rais kuhakikisha kuwa ripoti ya uchunguzi ya maafa ya mlipuko wa bomu kule Arusha inawekwa wazi na wahusika wote wanachukuliwa hatua stahiki.
Naibu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Siasa wa chama hicho, Shaweji Mketo, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa, maandamano hayo hata kama ikitokea jeshi la polisi ikayazuia, yatafanyika kama yalivyopangwa.

Akielezea kuhusu maandamano hayo, Mketo alisema kuwa, tayari wameshamwandikia barua Rais na jeshi la polisi kuhusu azma hiyo na kwamba Ikulu wanatarajia kupokelewa na Kikwete au mwakilishi wake. Alisema Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova, amempigia simu muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari na kumtaka aende Polisi Kati kwa ajili ya kuandaa njia za kupita siku hiyo.
Alisema maandamano hayo yataanza saa 4:00 asubuhi eneo la Buguruni kituo cha mafuta kuelekea Barabara ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Bibi Titi, Posta Mpya, Ardhi na hatimaye Ikulu.

Kuhusu Mtwara, Mketo alisema wanataka kumfikishia Rais malalamiko ya wananchi wa Mtwara kutokana na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na polisi na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). Pia alisema maandamano hayo yamelenga kuishinikiza serikali kukomesha vitendo vya kinyama, kijangili vinavyofanywa na majeshi hayo kwa kuwakamata, kuwatesa na kuwabaka wananchi wasio na hatia mkoani humo.
NIPASHE JUMAPILI

VIGOGO 200 WAHOJIWA MABILIONI YA USWISI, VIGOGO WENYEWE NI HAWA HAPA ..

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.SUALA la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatar
ajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Jaji Werema alipoulizwa na Mwananchi Jumpili maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea. “Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.
“Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.”

Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa. Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea.

Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.
Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini.
Werema anaripotiwa akiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta.
Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.
MWANANCHI.

Mwana FA. AJUTA KUANZISHA BIFU NA JIDE, HANA RAHA AMEAMUA KUFUNGUKA..SOMA ALICHOKIANDIKA HAPA

MwanaFAKutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.
Mwanamuziki Hamis Mwinjuma, maarufu Mwana FA, amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee, baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake kuna jina la Jay Dee.
Tofauti na ilivyozooeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee ‘Anaconda’, hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.

Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kurudia wimbo huo na alipofika katika kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi huo ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka; “Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapatana,” alisema Mwana FA.

Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa kama 250 tu.

Tanzania's Got Talent (Video)

Amazing soccer talent/skills from a Tanzanian girl

Matangazo Msimu wa SabaSaba. Wahi Mapema, Nafasi ni Yako Kabla Haijachukuliwa!!

Matangazo Msimu wa SabaSaba
Kwa wadau wetu walio na matangazo ya aina yoyote na ukubwa wa saiz yoyote ikiwa ni pamoja kama unakodisha au unauza Shamba, Nyumba, Gari, Duka, Saluni, Ofisi,Kiwanda, Kampuni na Kadhalika.
 Pia ni fursa kwako kua Sponsor wetu kwa matangazo ya muda mrefu. 
Kumbuka mtandao wetu ni maarufu unatembelewa na watu wote ulimwenguni kutokana na mfumo wetu wa usambazaji wa habari ktk tovuti zetu nyingine pia mitandao ya kijamii. ..Hii ni nafasi yako. Wahi sasa..!! Bei ni nafuu sana.  
Kwa maelewano usisite kutuandikia Barua pepe kupitia darslam@rocketmail.com  
Pia tunapokea habari mbalimbali buree.
         Bila kusahau Blog yako ya Taifa  ..Bongo Blogs - Blog za Bongo
Inakupa fursa husika.
Kazi ni kwako...!

Supermoon to Light Up Night Sky June 23,2013

 super moon

G.P. Mafia - Da Covenant ft. Louieville Sluggah (Official Video)

Dr ASHA-ROSE MIGIRO AFAGILIWA NA RADIO ONE KWA KUKIENZI KISWAHILI

 Asha-Rose Migiro Dr. Asha-Rose Migiro
DAR ES SALAAM, Tanzania
NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.
Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.
"Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;
   "Mmoja wa Watanzania hawa naomba nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya...