
Hatimae Mbowe, Lema Wajisalimisha Polisi

Mwenyekiti wa Chadema Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema hivi sasa bado wanahojiwa na Polisi baada ya Kujisalimisha kutokana na Maagizo ya Polisi ya kutaka kuwahoji kuhusiana na Tukio la Mlipuko wa Bomu Arusha. Baada ya Mohojiano hayo wanatarajia kushiriki kuaga mwili wa Marehemu Judith Moshi aliyekuwa Mwenyekiti wa Bawacha Arusha, anayeagwa leo na kutarajia kuzikwa mjini Arusha leo.
Chadema blog
Maandalizi ya Sherehe za Miaka Mitatu ya Vijimambo

Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, wanamitindo ya mavazi mbalimbali kuwakilisha, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani Shilole na Masanja wakishirikiana na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili
HOTEL KWA WAGENI
Tumeongeza vyumba 35 Hotel ya Country Inn & Suites
Na unapopiga simu uliza SWAHILI CULTURE IN USA kusudi upate unafuu wa bei nambari ya simu ni 301 350 8088 na Addrees ni
8850 Hampton Malls Drive North
Capitol Heights, MD 20843
Hotel za jirani na hapa ni
Hampton Inn
9421 Largo Dr West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 499 4600
Extended Stay American
9401 Largo Drive West,
Largo, MD 20774
simu ni 301 3339139
Confort Inn
56 Hampton Park Blvd
Capitol Heghts, MD20743
Simu ni 301 336 8900
MAONYESHO YA 37 YA SABA SABA 2013, TAN TRADE YATOA SEMINA KWA WASHIRIKI MBALI MBALI
Washiriki mbali mbali kutoka katika mashirika na vyama mbali mbali vya
ujasiriamali kutoka nje na ndani ya Tanznia leo wamepatiwa semina
yenye mafunzo mbali mbali katika maandalizi ya maonyesho ya 37 ya saba
saba yatakayoanza hivi karibuani katika viwanya vya Mwalimu nyerere
vilivyopo kilwa road jijini Dar es salaam.
Akifungua semina hiyo iliyofanyika leo mkurugenzi wa Tan Trade bi Anna F.Bulando ameelezea maonyesha haya ya 37 kuwa yatakuwa maonyesho makubwa ya kimataifa na ya kipekee kufanyika jijini Dar es salaam ukilinganisha na maonyesho ya miaka mingine kwani maonyesho haya yatashirikisha nchi nyingi zaidi kuliko miaka yote.
Nchi zitakazoshirkia katika maonyesho ya mwaka huu zimeongezeka kutoka nchi 11 zilizoshiriki mwaka jana na kuongezeka hadi kufikia nchi 32 ambazo zitashiriki katika maonyesho hayo mwaka huu.
mada zipatazo sita zimeweza kujadiliwa na kutolewa mafunzo kwa washiriki ili kuhakikisha kuwa wanafuata na kuzingatia hatua hizo ambazo kama wakifuata na kuheshimu basi watapata mafanikio makubwa katika biashara zao na pia kuzidi kuwa vutia washiriki wengine ambao bado hawajaonyesha nia ya kushirikia maonyesho ya saba saba.
baadhi ya mada au masomo yaliyotelewa kati ya sita ni elimu juu ya wajibu wa kila mshiriki kuhusu afya,usalama wa vyakula na usafi wa mazingira uliotolewa na afisa afya wa manispaa ya Temeke bwana William muhemu.
Ambapo alikazia zaidi kuhusu kila mshiriki kuhakikisha kuwa wakati wa maonyesho h ayo kila moja anakuwa msafi na kufuata kanuni za afya ili kuhakikisha kuwa shughuli zote za maonyesho ya 37 ya saba saba yanakwenda vizuri bila kutekea kwa maambuzi ya magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi hutokea katika mikusanyiko mikubwa ya watu ambao hawafuati sheria na taratibu za afya pindi waendapo na watokapo katika maliwat na pia katika ulaji mbaya ambao mara nyingi watu hujikuta wakilishwa kinyesi cha binadamu bila wao kujua kutokana na kula katika magenge ya watu wanaotoa huduma bila kuwa wasafi na hivyo kusabisha kulipuka kwa magongwa ya milipuko kama kipindu pindu.
mada nyingine iliyopata wasaa wa kujadiliwa ni pamoja na mada ya upakiaji au auandaa na usafishaji wa bidhaa ambao uanatakiwa uwe na viwango madhubiti unaokubalika na mamlaka ya viwango Tanzania TBS kwa kuhakikisha kila mjasirialamali anafuata njia sahihi za uandaa na usindikaji wa bidhaa yake katika viwango vinavyokubalika na Tbs mada hiyo ilitolewa na bi Mary Meela kutoka TBS.
Mada nyingine ni masoko ya ndani na nje na mfumo wa ufuatiliaji na masoko ya kimataifa iliyotolewa na Bwana Pius Mikingoti wa GS1 Tanzania, mada nyingine ni madaraja na viwabgo vya bidha vinavyotengezwa na kusafirisha au kuuzwa kwa mteja /mlaji au mtuamiaji iliyotolewa na Bwana kiteka na mada nyingine ni kuhusu kodi ambayo mada hii imeandaliwa na kutolewa na bi. Rose Mahendeke kutoka TRA.
IDD SIMBA NA WENZAKE WAACHIWA HURU KATIKA KESI YA KUHUJUMU UCHUMI

Mahakama imewaachia huru washitakiwa kwa sababu Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk Eliezer Feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Simba anayetetewa na wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa, washitakiwa hao wapo huru.
Happiness Katabazi
Viongozi wa Chadema na Wananchi Waachiliwa Huru kwa Dhamana.. (Video)
Jeshi la polisi nchini limewaachilia kwa dhamana viongozi wa Chadema na wananchi wote waliokuwa wanashikiliwa na limemtaka mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe kuwasilisha ushahidi wa mtu aliyelipua bomu kwenye mkutano kwa Mh. Rais kama hana imani na jeshi la polisi.
Madam Rita na Water Chilambo Wakizindua Bongo Star Search 2013 (Video)
Shindano la kusaka vipaji vya uimbaji muziki la Epiq Bongo Star Search, EBSS, leo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo uliofanyika makao makuu ya Zantel umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Paulsen a.k.a Madam Rita ambaye ni mwanzilishi na mmoja wa majaji shindano hilo, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan pamoja mshindi wa shindano hilo mwaka jana, Walter Chilambo.
POETRY ADDICTION Ya FidQ Na CheusiDawaTV Ni Mwezi Huu..!
Poetry Addiction ni kitu kipya kitakachoanaza hivi karibuni chini ya uangalizi wa Fid-Q na CheusiDawaTV … Wameandaa kitu TAREHE 29 JUNE kwa ajili yako … Itahusisha wasanii na activities zingine in it … Wanna know more???? … Check hapa chini;

Subscribe to:
Posts (Atom)