Video ya Mahojiano Aliyofanyiwa Mtanzania Aliekamatwa na Dawa za Kulevya Misri.
Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
صبايا الخير: تهريب المخدرات من الأجانب إلى داخل مصر .. لقاء مع مهربة تنزانية
صبايا الخير: تهريب المخدرات من الأجانب إلى داخل مصر .. لقاء مع مهربة تنزانية
Pata nafasi kuona video ya mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina dawa za kulevya
Soma SABABU ZA JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU YA MABOMU JIJINI ARUSHA
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo . Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..
Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na kuanza kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta mvutano kati ya viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa mabumu yalianza kusikika.
Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee
Breaking News! Sugu na Lema Wamenusurika Kufa, Gari la Tundu Lissu Lapigwa Bomu Arusha!! KIMENUKA
Hivi ndivyo hali ilivyo katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha Tanzania
MBUNGE wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi amenusurika kufa wakati akielekea Jijini Arusha kuwahi kuaga miili ya marehemu waliouawa kwa mabomu yaliyolipuliwa siku chache zilizopita kwenye mkutano wa Chadema jijini hapa.
Joseph Mbilinyi aliamua kwenda kuungana na Wananchi wa Arusha na wanachama wa Chadema, amepata ajali hiyo maeneo ya Kateshi Wilaya ya Hanang.
Ajali hiyo imetokea baada ya gari la Mbunge huyo kugongana na gari la abiria lililokuwa katika mwendo kasi,na katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya gari la mbunge huyo kuharibika vibaya.
Mbali na Gari Sugu kuahribika vibaya taarifa kutoka Arusha pia inaeleza kwamba Gari la Tundu Lissu pia limepigwa bomu kama ilivyokuwa gari la Lema.jijini Arusha hali bado si shwari kwani Askari Polisi wanaendelea kutawanya waandamanaji walioamua kuingia mitaani huku wakiwa na mji kwenye madumu kwa ajili ya kuwa kila wanapopigwa mabomu na Polisi
Lema anusurika kufa, akimbilia kwa wachoma kiti moto!

WAKATI hali ikizidi kuwa mbaya jijini Arusha kufuatia mapambano ya raia na Jeshi la Polisi,Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amelazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya Nguruwe, (kiti moto).
Lema ambaye alinusurika kupigwa na bomu lilorushwa na Askari wa Jeshi la Polisi na kuharibu gari lake alikuwa akijaribu kuwatuliza wananchi walioanza kukusanyika katika vikundu, wakijadii amri ya Serikali ya kukataza miili ya watu waliofariki Dunia katika shambulio la kigaidi isiagwe katika viwanja hivyo.
Kabla ya Lema kupigwa mabomu na kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe hao alikuwa akisema, "jaribuni kuvumilia tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali ya kuleta miili ya wapendwa wetu hapa,kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wanausalama ambao wanalinda amani,ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wamesha kufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshma zote"alisema Lema kabla ya kupigwa bomu na Polisi.
Kauli hiyo ilizidi kiwachefua Polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo, kwa ajili kuweka hali ya usalama wa eneo hilo ambapo walisema kwamba hakutakuwa na suala la kuaga maiili ya watu hao katika eneo hilo.
Mwandishi wa Habarimpya.com pia alikimbilia kwa wachoma kito moto kwa nia ya kujificha kufuatia mabomu kurushwa kila kona ndipo alipokutana na Mbunge huyo,hata hivyo alipojaribu kuzungumza naye alikataa kujibu lolote huku akiwa ameinamisha kichwa chini,kabla ya kuchukuliwa na gari ndogo aina Toyota Corola na kutokea kusiko julikana.
Habarimpya.
Vodacom Yapanua Wigo Huduma na Ajira kwa Watanzania
Meneja wa duka jipya la Vodacom lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza Bi.Miriam Minja,akifungua duka hilo kwa mara ya kwanza tayari kwa kutoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo,akishuhudiwa na Mkuu wa Idara ya Mauzo na Maduka wa Vodacom Tanzania, Bi.Upendo Richard(kulia)na Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa kampuni hiyo Bi.Joseline Kamuhanda.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Millennium Tower ghorofa ya kwanza.Tayari kabisa kwa kutoa huduma kwa wateja wake.
Miriam Minja (right) the Manager of Vodacom Shop at Millennium Towers, Dar es Salaam, shows the features of a phone to Lameck Hanold, a customer who visited the shop during its official opening. Looking on on the left is Vodacom Tanzania Head of Key Accounts and Franchise, Upendo Richard.
Hili Ndio Jenereta Linaloendeshwa kwa Haja Ndogo
Genereta hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k, Sasa genereta hilo linafanyaje kazi?
Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo kiitwacho electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen. Kisha hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji kwaajili ya kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.
Hiyo gas cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa, liquid borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi.
PIMP My Ride
Alot of people do modify and turn parts of their car. From paint jobs
to custom interior and with stereo systems that are louder than most of
the club systems, cars like these are a popular way for owners to
express their personality and their style ability what they are capable of..

Ndege Maalumu za Kivita Kutawala Anga Dar
Kwa mujibu wa taarifa ya idara hiyo, katika kuhakikisha usalama wa kutosha wakati wa ziara ya Obama tayari maofisa wao wameshakamilisha maandalizi ya kiusalama katika nchi zote anazotarajiwa kutembelea.
Meli ya kivita kutua bandarini
Katika kuchukua hatua hizo, meli kubwa kabisa ya kivita yenye hospitali maalum zipo tayari kwa ya kambi maalumu katika bandari maalum za nchi atakazotembelea, kwa ajili ya kukabiliana na dharura yoyote ya kiafya ya Obama na familia yake.
Ili kuwawezesha maofisa wa kijasusi wa Marekani, ndege ya kijeshi ndiyo itakayobeba magari 56 zikiwemo limousine 14 na magari matatu maalumu ya...

Subscribe to:
Posts (Atom)