Utafiti ulifanyika kwa miaka minne umeweza kuvumbua kitu mfano wa
meza kubwa ambacho ni 'touchscreen'.Kifaa hiki kinaweza kutumika kwa
walimu kufundishia na wanafunzi kusomea na kuandika.
Watafiti hao kutoka Durham Univesity wamegundua kitu hiki kinachoitwa
'Star Trek classroom' au 'classroom of the future' ambacho
hakitawafanya waalimu washike chaki tena wala wanafunzi wabebe
madaftari.
Watafiti hao wamesema pia ugunduzi huo umeonyesha kuwasaidia
wanafunzi, katika kuwa na uwezo zaidi katika hesabu tofauti na katika
mfumo wa kuandika kwenye madaftari.
Aidha wanasema dawati hilo linawafanya wanafunzi wafanye kazi kwa
pamoja, kitu ambacho kinaongeza juhudi kwa hata yule aliyekuwa na tabia
ya kutegea.
Mtafiti Mkuu, Profesa Liz Burd anasema hata wakati wanatengeneza
lengo lao kubwa lilikuwa ni kuona wanafunzi wanashiriki moja kwa moja
darasani.
Dawati hilo linaweza kutumiwa na wanafunzi wawili mpaka watatu, mwalimu anaweza kuwatumia kazi kutoka dawati jingine.