Pages

Matano Kuhusu King GK na DSTV

King GK na DSTV Baada ya ukimya wa zaidi ya miaka mitano ambao pia ulimfanya asitake kuongea kwenye chombo chochote cha habari, amekua akikataa interview kwa kipindi chote, hatimae Kamanda mkuu wa kikosi cha East Coast, King GK ametoa ya moyoni.
Kwenye backstage ya KTMA 2013 kwenye Exclusive interview, GK amezungumza mambo matano makubwa kuhusu yeye na muziki wake.

1. Baada ya ukimya wa zaidi ya miaka mitano, single yake mpya ya kurudi kwenye game rasmi inatoka kwenye kipindi kisichozidi mwezi mmoja kutoka sasa.
2. Uhusiano wake na Mwana FA na Ay uko poa kwa sasa.
3. Mpaka sasa amesharekodi nyimbo mpya zisizopungua sita zikiwemo kolabo ambapo Ay na Mwana FA wameshirikishwa.
4. East Coast bado ipo na itazidi kuwepo.
5. Hawezi kutaja tarehe rasmi ya kurudi kwa sasa kwa sababu anataka iwe surprise.

Kauli kama hizo kutoka kwa GK ni good news kwa kila shabiki anaemfahamu baada ya miaka mingi ya ukimya wa East Coast, ambayo ilianza kuwa kimya baada ya mastaa kadhaa kuanza kujiondoa kutokana na kutofautiana wakiwemo Ay na FA.
GK alikua mmoja wa wageni walioshiriki kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali wa KTMA 2013. 
  DSTV

GARI INAUZWA! TOYOTA GLANZA TURBO BEI ni SH. MILIONI TANO!


Toyota Glanza Spot (Turbo Charger) Inauzwa kwa sh.milioni tano tu .Gari ipo ipo Dar es Salaam .Piga Simu 0714604974 or 0684885441 kwa mawasiliano zaidi..

Balotelli’s Engagement Is Confirmed With A £100,000 Engagement Ring

Mario Balotelli’s girlfriend Fanny Negeusha Mario Balotelli’s girlfriend Fanny Negeusha has appeared to confirm their engagement by posting a picture of herself wearing a dazzling diamond ring on her Instagram page.
According to reports, the 22-year-old footballer popped the question with the £100,000 (N250 Million) jewel this weekend.
Belgian model Fanny later confirmed the news by posting a picture of the diamond, alongside the caption: ‘It’s official!’Fans were quick to post their congratulations to the couple both in English and French following Fanny’s post. Mario and Fanny, who started dating six months ago, are now said to be putting plans for the lavish ceremony in action.
The pair had apparently spoken about getting married before, but the timing hadn’t been right.
However, now the pair are planning to take a luxury holiday in the near future to discuss details for their big day.
The engagement comes after the pair split briefly last month following allegations that Mario had made lewd comments about his model girlfriend.
Mario spoke of his love for Fanny during a magazine interview earlier this year, saying: ‘In a short time she found herself in sync with me. I could spend my whole life with someone like this.’ The footballer had previously been in a relationship with 25-year old presenter Raffaella Fico who claims her four-month old child Pia is his daughter.
Mario reportedly denies the fatherhood claims, and has asked for a paternity test to prove it before he sees the baby.

Sikiliza Kauli ya Ubalozi wa Tanzania Kuhusu Mtanzania Anaedaiwa kutaka Kunyongwa Egypt

Sharifa Mahmud
Baada ya watu wengi kuzipata habari na bila kujua imekuaje kwa Mtanzania anaedaiwa kukamatwa na dawa za kulevya nchini Egypt na kwamba alikua anakaribia kunyongwa, balozi Mohamed Haji wa Tanzania nchini Egypt ameongea Exclusive na millardayo.com na kueleza yote anayoyafahamu kuhusu hii ishu.

Namkariri akizungumza
1. Ni kweli kuna raia wawili Watanzania wamekamatwa na dawa za kulevya ambao ni Mbarak Abdallah Salim (28) na Sharifa Mahmud (27) wakazi wa Magomeni Kagera Dar es salaam, wanaundugu wa mtoto wa shangazi na mjomba.

2. Walikamatwa tarehe 16 May 2013 wakati wakiingia Misri, kwa mujibu wa maelezo safari yao ilianzia Dar es salaam kwenda Mombasa, Nairobi mpaka Misri.

3. Dawa za kulevya walizokamatwa nazo zimetajwa kwamba ni Heroine kilo saba.

4. May 18 2013 ndio tuliitwa kwenda kutazama Raia wetu, nikatuma maafisa wawili wazuri kwenda kutazama ili raia wetu wasimbambikiwe kesi.

5. Baada ya hapo waliwekwa rumande na tukapata nafasi ya kuwaunganisha na nyumbani huku Tanzania wakaongea kwenye simu kilichowapata.

6. 26 May 2013 ndio walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande wote wawili.

7. Hawa ndio Watanzania wa kwanza kukamatwa na kesi kama hii na ikithibitishwa wamefanya kweli, hili kosa ndilo litakua doa la kwanza kwa Tanzania hapa Misri.

8. Ishu ya kunyongwa, tunajaribu kufanyia kazi lakini hakuna kumbukumbu za mgeni yeyote kwa sisi tunavyojua ambae amewahi kunyongwa kuhusu ishu ya dawa za kulevya.

9. Tunajitahidi kuwasiliana na mamlaka zinazohusika ili kujua siku gani watapelekwa tena Mahakamani alafu tutawafahamisha nyumbani. Kwa ushahidi unaweza kumsikiliza balozi hapa chini na pia kutazama video hapo chini ya ushahidi wa kukamatwa na dawa za kulevya…

All the News About my Renewal with Real Madrd are False: Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo  
Sakata la usajili wa mchezaji Cristiano Ronaldo limezidi kupamba moto - wakati taarifa kadhaa kutoka barani ulaya zikisema kwamba Ronaldo anatarajia kusaini mkataba mpya na Real Madrid huku wengine wakisema yupo njiani kurejea Manchester United - leo hii mapema mchana Cristiano Ronaldo alitumia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter kukanusha taarifa zote zinahusu kuongeza mkataba wa kuichezea Real Madrid. Hata hivyo Ronaldo ameendelea kukaa kimya kuhusu taarifa za kutaka kurejea United.
Kwa wiki kadhaa taarifa za kurudi Man United kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 65 zimekuwa zikisambaa huku Raisi wa Madrid Florentino Perez akisisitiza anataka kumbakisha Cristiano kwa gharama yoyote.

NI KWELI LANGA AMEFARIKI DUNIA LEO!??

 LANGA KILEO A.K.A LANGA
TAARIFA ILIYOTUFUKIA CHUMBA CHA HABARI, INAELEZA KUWA MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYADA LANGA KILEO A.K.A LANGA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA.

LANGA AMBAYE INADAIWA KUWA ALIPATWA NA MALARIA KALI SANA HALI ILIYOPELEKEA KUKIMBIZWA HOSPITALI SIKU YA JANA.

 TAARIFA KAMILI YA UHAKIKA ITAKUJA 

RapCityStunner Ft Hefner na Reezon - My Way (Audio)

My Way-

MWANA FA AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA LADY JAYDEE (Audio)

Baada ya kutibuana na Lady Jaydee, Mwana FA ameamua kuvunja ukimya na kuwataka mashabiki wachukulie poa maana ni hali ya kawaida tu katika maisha ya kibinadamu.....
Ugomvi wa wasanii hawa ulianza baada ya Mwana FA ku re -tweet post moja ya shabiki wake ambayo ilikuwa ikiiponda show ya Lady Jaydee...
Lady jaydee alijaribu kumuonya mara kadhaa lakini FA hakusikia na badala yake aliretweet post ya shabiki mwingine ikimponda Lady Jaydee....
Uvumilivu ulimshinda Lady Jaydee na kuamua kujibu mashambulizi kwa kumuita Mwana Fatuma na na mengine mengi.....
Wasikilize hapo chini wakifunguka

Mahojiano na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) Nchini

Karibu katika sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya Jamii Production na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali.
Katika sehemu hii, Mhe Amina ameeleza mengi ikiwemo...
1: Historia ya maisha yake.
2: Aliingia vipi kwenye kazi ya diplomasia?
3: Ni nini wajibu wake? Anawajibika kwa nchi ya Marekani ama na mashirika ya kimataifa kama IMF na World Bank?
4: Ni wapi ulipo mpaka kati ya majukumu ya mabalozi wa nchi wanachama wa AU na yeye anayewakilisha Umoja?
5: AU ina mikakati gani katika kufunda ama kuwalea viongozi wa afrika?
6: Kuna MAFANIKIO GANI ya Umoja wa Afrika hasa ukizingatia kuwa tangua kuanzishwa kwake tumeshuhudia nchi zikizidi kugawanyika badala ya kuungana kama Ethiopia na Eritrea na hata Sudan na Sudan ya Kusini?
7: Ni nini kinachokwamisha Umoja wa Afrika katika migogoro kama ya Kongo?
8: Nchi zetu ziko huru, zinajitawala, lakini ni kwa MANUFAA YA NANI?
9: Ni kweli kuwa Umoja wa Afrika unaendelea kuwepo si kwa mafanikio yake, bali kwa kukosekana kwa UMOJA M'BADALA?
10: Ni kweli kuwa kuna mamluki wanaokwamisha harakati za Umoja wa Afrika toka nje ya bara letu?
11: Tofauti ya mifumo ya utawala na nguvu za kijeshi na uchumi zinaathiri vipi UMOJA WA AFRIKA?
KARIBU UUNGANE NASI

Rasimu ya Katiba Chadema Waitisha Kikao cha Dharura

Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kimeitisha kikao cha dharura cha kamati kuu kujadili na kutoa msimamo wa rasimu ya katiba mpya na kuwataka Watanzania kutokua na haraka kuendelea kuichambua rasimu kwa makini ili kuiboresha.