SIMBA SPORTS CLUB YAANDAA MPANGO MKAKATI
Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-
1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.
Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013 Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-
1. Joseph Itang’are
2. Swedy Mkwabi
3. Francis Waya
4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Ngahyoma
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mutahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga
Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.
Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.
Mpango mkakati huo utakuwa tayari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.
Imetolewa na
Evodius Mtawala
Katibu Mkuu,
Simba Sports Club.
Was Rapper Eminem Stabbed 4 Times In NYC??
Worse yet, users who comply with instructions to share said links via social media will suck their Facebook friends and Twitter followers into the scam as well. Don't do it!
An identical scam claiming Justin Bieber was the victim of a stabbing attack made the rounds in 2011. Even the photo was the same.
Tips & tricks:
How to Spot a Facebook Survey Scam
VODACOM NA SAMSUNG WAZINDUA Samsung Galaxy S4.
Samsung Tanzania Country Manager, Kishor Kumar, illustrates the features of the new Samsung Galaxy S4 to Vodacom Tanzania Manager for Franchise and Operations, Elihuruma Ngowi (right), Samsung Tanzania Manager for Sales and Distribution, Sylvester Manyar and Vodacom Tanzania Post Paid and Enterprise Acquisition Manager, Ibrahim Kiongozi (left) during the launch of the device in Oysterbay, Dar es Salaam. Upon purchase of the Samsung Galaxy S4, customers will get free 5GB internet for 30 days when activated with Vodacom SIM card. The device also comes with 24 months of warranty that will cover any device feature malfunctions.
BABA JONII KUTAMBULISHA BOONGE LA MIXTAPE KESHO KWA BIRTHDAY YAKE 16TH MAY
Adam Mchomvu a.k.a baba jonii Radio presenter clouds fm mwenye crown ya best presenter, anatarajia kutoa mixtape yenye ngoma kumi na nane alioshirikiana na wasanii mbali mbali kama Jose Mtambo, Banana Zorro, Illimatix, Cliff mitindo, G.nako, Niki wa 2, Babuu wa kitaa, TID, na wasanii wengine wengi kama zawadi kwa mashabiki wake ibaki kama kumbukumbu kwa kile anachokifanya hewani (on air) ... mixtape itaingia kitaani soon baada kupreview ngoma hizo ndani ya double XL (XXL) kuanzia saa tisa alasiri kwa hot 3 @ 3 ..... big up baba la baba!
BABAJONII MIXTAPE VOL 1
BABAJONII MIXTAPE VOL 1
Ikulu Yamruka Profesa Lipumba Kuhusu Dai la Rais JK Kujiongezea Muda
MWENYEKITI wa Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa Serikali ya sasa kukaa madarakani”.Katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa madarakani hadi mwaka 2017” kwa sababu kuna“wasiwasi kuwa mchakato wa sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof. Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi. Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango hiyo.
Taarifa hiyo imedokeza kuwa itakuwa ni vyema kwa Mheshimiwa Lipumba kuisaidia jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane.
Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.
Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu.
MWANA FA AMELIPWA MILIONI 18 NDANI YA MIEZI MITATU KWENYE RINGBACK TONE
Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
Subscribe to:
Posts (Atom)
