Mtakatifu Francis, amekubali ombi la Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Norbert Mtega (68),pichani, kustaafu katika utume wa kuongoza jimbo hilo.Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde, kutoka kwa Balozi wa Papa nchini, Askofu Mkuu Frascisco Padilla, ilieleza kuwa, Papa amekubali ombi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ombi la Askofu Mtega kwa Papa, lilitokana na kuwa na matatizo ya kiafya, hivyo kushindwa kuwahudumia waumini inavyopaswa. Hata hivyo, kikanisa ni siri ya mtu mwenye hadhi ya Askofu, anapoomba kwa Papa kustaafu.
“Baba Mtakatifu Francis amekubali ombi la Mhashamu Askofu Mkuu Norbert Mtega, kustaafu kutoka majukumu ya utawala wa kichungaji wa Jimbo Kuu la Songea, kwa sababu ya..