
Sifael Paul na Erick Evarist
BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja ‘mtata’ wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda (jina tunalo) kuwa amembaka, Uwazi lina kisa cha aibu ya karne.
Flora Bahati Lyimo.
Katika uchunguzi wake, hivi karibuni gazeti hili lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
VYANZO
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo gazeti hili likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
MAZITO
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).
Spika Anne Makinda. MAZOEA YAANZA
Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya...