Pages

Papaa Masai ft AliKiba - N'garin'gari (Audio)

Papaa Masai ft Ally Kiba - N'garin'gari

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO, VIJANA NA UTAMADUNI AMOS MAKALLA ATANGAZA KULIVALIA NJUGA SWALA LA JIDE NA RUGE

Na Mwandishi Wetu IKIWA ni siku moja tu tangu Naibu Waziri wa Habari Michezo Vijana na Utamaduni Amos Makala kutangaza hadharani kulivalia njuga suala la mzozo kati ya Mkurugenzi wa wa Kampuni ya Clouds Media Group Ruge Mutahaba na msanii nyota wa kike wa Bongo Fleva Judith ‘Wambura Lady Jaydee’ Ruge ametoa ya moyoni.
Tanzania Daima ambayo ilimpigia simu Ruge na kumuuliza ana lipi la kusema baada ya Makala kutamka kwamba atawaita wawili hao na kuzungumza nao sambamba na kuleta suluhu.
“Mimi kana nilivyosema katika tamko langu wiki iliyopita kwamba niko tayari tuitwe na watu watusikilize pande zote mbili hasa mlalamikaji na ukweli uweze kuwa wazi zaidi kwa sababu hadi sasa Lady Jaydee amekuwa akisema mambo mengi kiasi kwamba hata nashindwa kumuelewa”
Na siyo Waziri Makalla tu pia ikiwezekana hata kama kuna watu wengine wanataka kujitokeza ili kutuweka katika kiti moto watuulize maswali na kila mmoja wetu aote majibu mbele ya hao watu mimi niko radhi kufanya hivyo” anasema Ruge.
Wakati huohuo Ruge ameongeza kwamba tayari ameshafuata taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kumfungulia jalada la malalamiko ya kutukanwa na Lady Jaydee na taarifa hiyo amepelekewa msanii huyo akiitwa katika vyombo vya sheria. Lakini ninaweza kusema jambo hili linaweza kuzungumzika nje ya vyombo vya sheria kwani sisi tunaliona ni jambo dogo na la mzaha lakini lina athari kubwa katika jamii inayotuzunguka anasema Ruge.
Mwanzoni mwa mwezi huu Lady Jaydee aliamua kuibuka na kuituhumu Clouds Media Group kwa kutumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter nab log yake kwamba wana muhujumu kimuziki , kuzuia matangazo ya mgahawa wake wa Nyumbani Lounge na kipaji chake kwa ujumba tuhuma ambazo Ruge na Clouds wanazikanusha vikali.
Mwandishi wa habari hii alijaribu kumtafuta Lady Jaydee azungumzie kuhusu kauli ya Waziri kwa kupitia simu ya mumewake Gadner Habash simu iliita bila kupokelewa.

SUPER D AFYATUA DVD TATU MPYA ZA MAFUNZO YA MASUMBWI

Rajabu Mhamila ‘Super D Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali
CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe.

mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Katuni ya Leo -Joto Hasira

Joto Hasira

HardMad Anaomba Kura Yako!!

HardMad
Hardmad Tunda

MOTHER'S DAY SPECIAL- JUMAPILI KILIMANJARO PASSION RESTAURANT-WASHINGTON DMV

KILIMANJARO PASSION RESTAURANT

Quote of The Day

Quote of The Day

Paris Jackson Wants to Move out of Grandmother’s Home and Move in with Biological Mother

Paris Jackson
There are reports that Michael Jackson’s daughter, Paris, wants to move out of the home she has been living in with her grandmother, Katherine, and her two brothers, Prince and Blanket, since her father passed away almost four years ago and move in with her biological mother, Debbie Rowe. Paris and Debbie were first seen together in public last month celebrating her 15th birthday, since then, they have been photographed shopping and on Debbie’s horse farm. Sources say Paris thinks her 84-year-old grandmother is too old fashion but the straw that broke the camel’s back was when Kathe... more »

Taarifa ya Wizara Kuhusu Kupitia Upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwar mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya ...

YANGA KULAMBA MILLIONI 70 ZA UBINGWA WA VODACOM

Ligi Kuu ya soka Tanzana Bara,
Mdhamini wa Ligi Kuu ya soka Tanzana Bara, Kampuni ya Vodacom imetangaza kutumia kiasi cha Shilingi Mil 200 kwa ajili ya kutoa zawadi ya fedha taslimu katika ligi inayomalizika mei 18 ambapo sasa Machampioni wa msimu huu watajinyakulia Shilingi Milioni 70.
Mbali ya bingwa, Vodacom pia itatoa fedha kwa timu inayomaliza nafasi ya pili, ya tatu na ya nne katika msimamo wa ligi ambazo ni Sh. 35 Milioni, huku Sh. 25 Milioni na Sh. 20 Milioni zote zikiwa na ongezeko ikilinganishwa na zawadi za fedha zilizotolewa katika msimu wa 2012 / 2013.
Zawadi hizo zimetangazwa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kampuni hiyo kupitia Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim, ikiwa ni pamoja na kuainisha zawadi za washindi wa mchezaji mmoja mmoja pamoja na timu iliyoonyesha nidhamu kwa msimu huu.
"Mwaka huu tutatumia kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya zawadi za...