 |
Ibrahim Mzee Ibrahim
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Zanzibar,(DPP)
|
Nyaraka za barua za mawasiliano kuhusu maendeleo ya jalada la kesi ya
mauaji ya Padri Evarist Mushi inayomkabili Omar Mussa Makame, zimevuja
baada ya wakili anayemtetea mtuhumiwa huyo kuziwasilisha mahakamani jana
mjini Zanzibar.
Barua hizo pamoja na taarifa za kikao
kilichofanyika Aprili 4 mwaka huu kujadili jalada la uchunguzi wa kesi
hiyo inadaiwa kiliwahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Othman Masoud Othman, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP)
Ibrahim Mzee Ibrahim, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali
Mussa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Upelelezi, (DDCI) Yusuph
Ilembo. Wakili wa upande wa utetezi Abdallah Juma Mohamed alitoa
taarifa hizo wakati akipinga hoja ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali,
Abdallah Issa Mgongo, baada ya kuiomba Mahakama Kuu kuahirisha shauri la
kesi hiyo kwa madai upelelezi bado haujakamilika.
Wakili huyo
alisema kwamba amefanikiwa kupata barua yenye kumbukumbu namba
BUB/P89/VOLV/54 ya Machi 25 mwaka huu, ambayo imeandikwa na Inspekta wa
Jeshi la Polisi Suleiman Suleiman kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa
wa Mjini Magharibi ambayo ilikuwa ikimtaka mkuu wa...