Pages

Siri ya Mtungi Sehemu ya 9

Kupotea kwa pikipiki yake nje ya nyumba ya ufukweni ya Lulu kunamfanya mpiga picha Cheche kuchanganyikiwa. Itakuwaje kama Cheusi atagundua uhusiano wake na Lulu? Cheche anarundika oungo juu ya uongo. Dafu anaahidi kumsaidia kuitafuta pikipiki -- lakini kwa sababu tu anahisi kwa kufanya hivyo atakuwa karibu zaidi na Lulu.
Wakati huohuo, tangu Nusura alipoolewa na Mzee Kizito, Duma amekuwa hana uelekeo na maisha yake. Kovu anamtambulisha kwa mfanya biashara aitwaye Golden kule kwenye kigrosari cha Tula. Lakini Kovu anapolewa na kumtukana bibi yule, Duma anamgeuka na kumtetea Tula -- kitu kinachomfanya yeye na Tula wagundue kuwa wana mambo yanayofanana.

Kutoka TFF:Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Limeondoa Utaratibu wa Wadau Wake Kuingia Bure Kwenye Mechi kwa Kutumia Tiketi Maalum (Free Pass)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeondoa utaratibu wa wadau wake kuingia bure kwenye mechi kwa kutumia tiketi maalum (free pass).
Kutokana na uamuzi huo hakutakuwa tena na pasi za bure kwa ajili ya kushuhudia mechi zilizo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa TFF katika viwanja mbalimbali nchini.
Uamuzi huo umetokana na ukweli kuwa free pass zimekuwa zikipunguza au kuchukua mgawo wote wa TFF kwenye mechi, na wakati mwingine Shirikisho hulazimika kutoa fedha za ziada kugharamia pasi hizo.
Pasi zote ambazo imekuwa ikitoa kwa wadau wake hukatwa katika mgawo wa TFF katika mechi husika. Shirikisho hivi sasa linapata asilimia nne tu ya mapato katika mechi za Ligi Kuu, ligi ambayo hivi sasa inaendeshwa na Kamati yake ya Ligi.

RUVU SHOOTING KUIKABILI YANGA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Machi 16 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi Jacob Adongo kutoka Musoma mkoani Mara ndiye aliyepewa jukumu la kuchezesha mechi hiyo namba 146. Adongo atasaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Milambo Tshikungu kutoka Mbeya wakati mwamuzi wa mezani ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam.
Mtathmini wa waamuzi ni Army Sentimea wakati Kamishna wa mechi hiyo inayokutanisha vinara Yanga na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya saba ikiwa na pointi 29 chini ya ukufunzi wa Charles Boniface Mkwasa na Msaidizi wake Selemani Mtungwe ni Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya ...

Ney wa Mitego ft Diamond Platinumz - Muziki Gani (Audio) Special reqst.

diamond platinumz, Ney wa Mitego

Odinga Amefikisha Malalamiko Mahakamani

 Raila Odinga
Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama makuu.
Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta.

Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu.
Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita udanganyifu kwenye uchaguzi.

Soma Jinsi Lulu Alivyo Banwa Twitter Kuhusu Kifo cha Kanumba

Elizabeth Michael a.k.a Lulu,Wakati zimebaki siku chache tu kutimia mwaka mmoja tangu msanii marehemu Steven Kanumba afariki dunia, msanii Elizabeth Michael a.k.a Lulu, ambaye bado anakabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusidia ya msanii huyo, Lulu azungumza...
Ikiwa ni kwa mara ya kwanza, Lulu (@hotlulumichael) ametweet maneno kadhaa katika ukurasa wake wa twitter zikionesha na kuthibitisha anavyomkumbuka na k**-miss Marehemu Kanumba.
Cheki tweets zenyewe hapa chini:

KanumbaKanumba

Kala Jeremiah ft Ben Pol - Karibu Dar (Video ya Mdau)

Taarifa Kutoka Simba Sports Club

Simba Sports Club
Ndugu wanahabari,
KUMEKUWAPO na taarifa za kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Simba uliopangwa kufanyika Kesho (Machi 17, 2013) jijini Dar es Salaam kujadili mustakabali wa klabu.
Ikumbukwe kwamba Mkutano Mkuu wa Wanachama ndiyo.. chombo cha juu kabisa cha maamuzi kwa klabu yetu. Katiba ya Simba SC imeupa Mkutano Mkuu hadhi ya juu mno na ndiyo maana imeweka utaratibu wa kufanyika kwake.

Miongoni mwa utaratibu ni kwamba ni lazima uitishwe na Mwenyekiti aliye madarakani wa klabu. Kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, ndiye atakayepanga ajenda, mahali na..

Nyaya za Transfoma za TANESCO Zenye Thamani ya Tsh.20 Mil Zimekamatwa Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma David A. Misime-ACP
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma David A. Misime-ACP
POLISI Mkoani Dodoma inawashikilia watu watatu baada ya kuwakuta wakiwa na nyaya za Transfoma za jumla ya 20 milion mali ya Tanesco.
Nyaya hizo aina ya kopa zenye uzito wa kilo 76 na nusu zilikutwa kwa watu hao baada ya msako wa polisi wakishirikiana na Shirika la umeme Tanzania Tanesco

Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema nyaya hizo za matumizi ya Transfoma hutumika kwa kufanyia Winding na nyingine ni kwa ajili ya kuzuia Radi [earthing] na kwamba imebainika ziliibiwa maeneo ya kizota na Ihumwa baada ya transfoma zake kuangushwa.
Misime aliwataja waliokamatwa kuwa ni Abdul Bakari 17 mkazi wa Chang'ombe, Stanel Shayo 26 muuza vyuma chakavu Nkuhungu na Peter Kessy 50 mkazi wa Area E manispaa ya Dodoma.

Aliongeza kuwa jeshi hilo linamsaka Jamal Said Sondo wa Chang'mbe Juu aliyekimbia ya mfanyakazi wake Abdul Bakari kukamatwa
Kamanda huyo amewataka wote wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu wajiepushe na kununua nyaya na vifaa vingine vya Tanesco pamaja na vyuma vyote viavyohusiana na miundo mbinu.

Wakati huohuo Jeshi hilo linamshikilia Denis Sadala 38 mkazi wa Mazase Wilayani Mpwapwa Kwa kumkuta akimiliki Gobore bila kibali, huku likiendelea kumsaka Matagi Charles 33 mkazi wa kijiji hicho aliyekimbia na kutelekza Gobore alilokuwa akimiliki kinyume na Sheria.
Na John Banda, Dodoma

Mada: Yesu ni Mungu, Je Yesu Alitahiriwa? (Video)

Exclusive: Lil Wayne In Critical Condition After More Seizures!

Lil Wayne
Lil Wayne is in ICU in critical condition after suffering yet another seizure, and we're told it doesn't look good ... TMZ has learned.
We broke the story ... the 30-year-old rapper was rushed to Cedars-Sinai Hospital in L.A. Tuesday night after suffering multiple seizures. He was released Wednesday but just hours later one of his bodyguards found him in his room, on the floor and unconscious.

Wayne was rushed to the hospital again, but this time he did not stabilize. He was taken to ICU, where he was placed in restraints because he was shaking uncontrollably.
We're told Wayne is currently "unstable," and has been placed in an induced coma. He is breathing through tubes.

We're told several people are at Wayne's bedside crying, and a number of rap artists and family members are on the way. Sources say the scene is violent as Wayne shakes uncontrollably.
Sources say there's evidence Wayne went on a Sizzurp binge after being released Wednesday, because doctors found high amounts of codeine in his system.

We're told Wanye's stomach was pumped 3 times to flush the drugs from his system. TMZ