Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika, hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa miaka mingine mitatu.
Hatua hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa wao.
Habari za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya Tanzania kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza la ...