Pages

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA CCM DMV MAREKANI NI JUMAMOSI Machi 16, 2013

CCM DMV
TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA CCM DMV
Ndugu Wana CCM DMV mnaombwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi bila kukosa,Ni nafasi ya kuwachagua viongozi wako utakao wapenda kujenga Chama imara.

SIKU: JUMAMOSI Machi 16, 2013
MUDA: SAA 10 JIONI (4pm)
MAHALI: TUTAWATANGAZIA

Ili uweze kupiga kura hakikisha una kadi yako ya Chama na uwe mwanachama hai, na kama huna kadi au umepoteza tafadhali wasiliana na Katibu wa Tawi wa muda
Yacob Kinyemi, Simu (202)-629-7841, email: yacob1972@yahoo.com

Nafasi zinazowaniwa ni:
1) Mwenyekiti wa tawi
2) Katibu wa Tawi
3) Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Tawi
4) Katibu wa Fedha na Uchumi wa tawi
5) Mwenyekiti wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
6) Katibu wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
7) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)
8) Katibu wa Jumuiya ya Wanawake ya Tawi (UWT)
9) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Tawi
10) Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Tawi

SIFA ZA MGOMBEA:
Awe na umri kuanzia miaka 18
Awe mwachama wa CCM mwenye kadi
Fomu za kugombania nafasi za uchaguzi ziwakilishwe kwa M/Kiti ( HIDAYA MAHITA)wa Kamati ya Uchaguzi kwa njia ifuatayo:
Fax: 1(888)835-5784 Email: ccmwashdc@gmail.com
Mailing address: 1709 HAMPSHIRE GREEN LANE#33 SILVER SPRING MD 20903
MWISHO WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU HIZO NI TAREHE 8 MARCH 2013

Moto wateketeza maduka zaidi ya kumi Tegeta

Moto umeteketeza maduka zaidi ya kumi, katika eneo la Tegeta Sokoni, manisipaa ya Kinondoni jijini Dar-es-Salaam,na kuwasababishia Wafanyabiashara hao hasara kubwa.

Camp Mulla - If You Believe Official Music (Video)

"If You Believe" - Miss Karun , Thee MC Africa and Shappa Man
Music Produced and Composed by: Kanyeria and Kus Ma
Video Director: Enos Olik
Camp Mulla sings for Peaceful Election by releasing their debut single of 2013 dubbed "If You Believe".General Elections in Kenya are fast approaching, slated for 4th March 2013.... for communities and our country to review and propose possible solutions with regard to peace ... ranging from a peaceful procession to advanced future growth & development for our economy. Just before the March elections, we urge all Kenyans to pray for peace, to love one another and in unity face the future together. This song is both a prayer and an awareness campaign for Peace and Prosperity in our beloved Nation. Never again should we allow our country to go through violence because of elections. We must choose peace over anything else. We believe that peace starts with the individual. It starts with you and me!

Chriss the Don ft Geez Mabovu na Kabayser - Ngoma Droo (Audio)

Chris the Dn ft Geez Mabovu na Kabayser

Wyre Nominated for International Reggae and World Music Awards

Dancehall artist Wyre
Dancehall artist Wyre the love child is riding high this year. After several nominations last year this year seems to have started in a similar way. Wyre has been nominated for the Best New Entertainer category at the prestigious International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).
Wyre will be battling it out with some of reggae’s icons across the world like D Major who is one of the most celebrated artists internationally and Jamaica’s upcoming artist Chronixx.

The IRAWMA awards were established in 1982 and are aimed at acknowledging and honoring the accomplishments and contributions of reggae and music artists, including songwriters, performers, promoters and musicians.
The prestigious awarding ceremony is also committed to promoting greater participation and acceptance of Reggae, Caribbean and World Music Internationally. The event will this year be held on May 4th in Florida.

Rick Ross Aongezewa Ulinzi Na Polisi

Rick Ross Aongezewa Ulinzi Na Polisi
 Rapper kutoka Label ya Maybach Music Group [MMG], Rick Ross ameongezewa ulinzi na jeshi la polisi la New Yorkbaada ya rapper huyo kupata vitisho vya kuuwawa tena kutoka kwa watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa TMZ, rapper Rozay huyo atakuwa na ulinzi wa Masaa 24 kutoka kwa polisi hao wa NY.
Ross anaetamba kwa sasa na album yake ya GOD FORGIVES I DONT na pia mixtape BLACK BAR MITZVAH yupo katika maandalizi ya album yake ya 4 inayokwenda kwa jina la MASTERMIND

Sakata la Binti Kiziwi Kukamatwa na Madawa ya Kulevya China

 Jacqueline Patric 
SIKU chache baada ya mrembo wa video ya wimbo wa Binti Kiziwi wa Ally Mohammed ‘Z. Anto’, Sandra Khan ‘Binti Kiziwi’ kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kunaswa na madawa ya kulevya nchini China, Jacqueline Patrick ‘Jack’ ambaye ni modo kiwango Bongo, amesema anajua kila kitu kuhusu tukio la kukamatwa kwake, Amani linakuhabarisha.
Akizungumza na mwandishi wetu katika mahojiano maalum juzi, jijini Dar es Salaam kuhusu uvumi ulioenea kwamba yeye ndiye aliyemchoma Binti Kiziwi kwa polisi na kusababisha kudakwa kwake, alisema tuhuma hizo si za kweli bali ni mbinu za watu wanaotaka kumchafua.

“Ngoja nikuambie ukweli, siku Binti Kiziwi anakamatwa mimi nilikuwepo uwanja wa ndege na niliona kila kitu. Unajua mwanzo alianza kulalamikia tumbo kumsumbua ghafla, akachukuliwa na kupelekwa kupewa huduma ya kwanza.
“Akiwa huko kwenye matibabu alipigwa ultrasound ndipo alipogundulika kuwa kumbe alikuwa na vitu tumboni.Katika hali kama hiyo unadhani ni mjinga gani anaweza kujitokeza na kudai huyo ni ndugu yake?”

“Mimi sijui chochote lakini nilichojua yule ni Binti Kiziwi na ni Mtanzania mwenzangu, tena staa kama mimi kwa hiyo sikuwa na sababu ya kumchoma ila ilivyogundulika hivyo nisingeweza kujitokeza maana na mimi pia ningetakiwa kuisaidia polisi kwenye uchunguzi.
“Kubwa kuliko yote, yeye ni ndugu yangu kabisa. Mama yake na mama yangu ni ndugu, nisingeweza kumchoma.”
“Jambo la muhimu nililoamua kufanya ilikuwa ni kutoa taarifa kwa ndugu zake wengine ili waweze kumsaidia.
Nilifanya hivyo kwa wakati. Siku zote nimekuwa karibu naye, hata nikienda China huwa nakwenda kumtembelea gerezani,” alisema Jack.

Masheikh, Askofu Waingia Matatani kwa Uchochezi

Masheikh, Askofu
POLISI mkoani Mwanza wanamshikilia Imamu wa Msikiti wa Ijumaa, huku likitangaza kuwasaka masheikh wawili wengine pamoja na Askofu (majina yote yanahifadhiwa) kwa kuhusika na uchochezi wa kidini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu alisema Imamu huyo wa msikiti alitiwa mbaroni kwa madai ya kubainika kwamba wanahusika na usambazaji wa CD za uchochezi ambazo zimekuwa zikihamasisha vurugu pamoja na mauaji ya kidini ikiwa ni pamoja na suala la kuchinja.

Kwa upande wake Askofu Mpemba wa Kanisa la Tanzania Field Evangelist yeye anasakwa kutokana na kutoa mkanda wa video (DVD) yenye jina la ‘Inuka Chinja Ule’ wakati mashehe wawili wanasakwa kwa kuhusika na uandaaji wa mikanda ya video mitatu (DVD) zenye majina ya ‘Unafiki katika Sensa, Kadhia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Uadui wa Makafiri’.

Wakati huohuo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Morogoro, limesema huenda likajitenga na Bakwata Taifa kufuatia hatua ya Sheikh Mkuu, Mufti Issa Shaaban bin Simba kumvua madaraka Sheikh wa Mkoa wa Morogoro, Yahya Semwali bila kufuata utaratibu.
Mwananchi

Yule Mtoto Mlemavu wa Ngozi (Albino) Aliyekatwa Mkono wa Kushoto Mkoani Tabora Huyu Hapa

Mwigulu Matonange(10
Mtoto Mwigulu Matonange (10)ambaye amekatwa mkono wa kushoto na watu wasiojulikana mkoani tabora akiwa na baba yake Gimbishi kwa mwaka huu walemavu wa ngozi(Albino)wamekua wakikatwa mikono ya kushoto, ikiwa ni tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo waliokumbwa na ukatili huo walikatwa mikono ya kulia.
--
BAADA ya kuibuka upya kwa matukio ya kuuawa na kukatwa viungo vya miili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), wanaharakati nchini wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina sababu za mauaji hayo, kuimarisha ulinzi hasa katika maeneo wanayoishi watu wa kundi hilo.

Wakati wanaharakati hao wakieleza hayo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mauaji hayo yanatokana na baadhi ya watu kuwa na imani za kishirikina, kwamba wakipata viungo vya watu wenye ulemavu watapata utajiri.
Alisema tayari Serikali imemuagiza Ofisa Maendeleo ya Jamii Rukwa ambao ulikumbwa na mauaji hayo, kukutana na maofisa maendeleo wa wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi.

Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea....>>>>>>

Ni Lil Wayne vs Pitbull. Lazma Kinuke Soon!

Lil Wayne ameamua kujibu diss ya Pitbull kwenye Twitter. Ugomvi huo ulianza baada ya Lil Wayne kudiss team ya Miami Heat na kusema kwamba amelala na mke wa Chris Bosh.
Wasanii kama Trick Daddy na Pitbull hawakupenda maneno hayo. Pitbull aliamua kumdiss Lil Wayne kwenye wimbo wake mpya “Harlem Shake (Welcome 2 Dade County).