Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa Zantel, Awaichi Mawalla(Pichani katikati) amesema itajumuisha vijana walioingia kumi bora, akiwamo Menina Atick, Nsami Nkwabi, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
Mshiriki Norman Severino akiongea mbele ya waandishi wa habari
Katika ziara hiyo pia, ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2006, wapenzi wa muziki watapata fursa ya kumshuhudia mshindi wa Epiq BSS, Walter Chillambo ambaye atakuwa akizundua wimbo wake siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Afisa biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kuwajengea vijana hao msingi katika kazi yao ya muziki baada ya shindano la Epiq BSS kuisha.
‘Lengo letu kuu la kudhamini Epiq BSS haikuwa kumpa mshindi zawadi, la hasha, bali tulikuwa na mpango madhubuti wa kubadilisha maisha ya vijana hawa kupitia vipaji vyao’ alisema Khan.
‘Lakini pia dhumuni la Zantel ni kuonyesha kuwa...