GHARAMA za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu za mikononi kwenda mwingine nchini kuanzia Machi Mosi, mwaka huu, zitashuka kutoka Sh. 115 hadi Sh. 34.92 kwa dakika moja.
Uamuzi huo umefanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa kampuni za simu nchini wa mwaka 2013, pia kuanzia Januari Mosi, mwakani, gharama hizo zitapungua hadi Sh. 32.40.
Vilevile, Januari, 2015 gharama hizo zitashuka hadi Sh. 30.58; Januari, 2016 zitashuka hadi Sh. 28.57 na Januari, 2017 zitashuka hadi Sh. 26.96 kwa dakika moja. Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma pichani, alisema umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2003 Sura 172.
Profesa Nkoma alisema viwango hivyo ni vya kikomo cha juu na pia ni elekezi, lakini akasema kampuni za simu zina uhuru wa kukubaliana kibiashara ili mradi makubaliano yao yasizidi gharama zilizoelekezwa na TCRA. Alisema gharama hizo zitatumika kwa mawasiliano ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na simu za kimataifa zinazoingia katika mitandao nchini.
Hivyo, ameziagiza kampuni zote za simu kufanya makubaliano mapya baina yao na ...