MAENEO ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana yaligeuka
uwanja wa fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa
mali, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.
Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land
Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro
wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa
lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza
kero za wakulima.Picha na Juma Mtanda
Vurugu hizo zimehusisha wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa
upande mmoja wa Morogoro, Mtwara Mikindani wananchi waliizingira nyumba
ya Diwani wa Kata ya Mikindani kwa madai ya kuwahifadhi watu wanaodaiwa
kuwa washirikina ndani ya nyumba yake, huku Dar es Salaam eneo la
Kariakoo, polisi na Wamachinga wakipambamba na Mgambo wa Jiji.
Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara
(60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea
vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa,
baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye
mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu, Kilosa.
Pamoja na mauaji hayo, wasafiri waliokuwa wakitumia Barabara ya Morogoro
– Dodoma, nao walionja machungu ya vurugu hizo, baada ya kukwama kwa
saa 5 kutokana na wananchi wa kijiji hicho, kufunga barabara kwa mawe,
magogo ya miti na kuchoma magurudumu ya gari.
Wananchi hao walichukua hatua hiyo huku wakisisitiza kutaka kuonana na
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ili kumaliza mvutano huo.
Katika vurugu hizo wanakijiji hao walivunja vioo vya madirisha ya baadhi
ya nyumba tano za kulala wageni, kuharibu gari dogo aina ya Landcruser
pamoja na kupora mali mbalimbali zi nazodaiwa kumilikiwa na
wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.
Kabla ya kufanya uharibifu huo saa 2:30 asubuhi, wananchi hao walifanya
maandamano sambamba na kusimama katikati ya barabara, hali
iliyosababisha polisi kufika eneo hilo kwa ajili ya kuwadhibiti.
Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo la tukio 5:20 asubuhi na
kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi,
hatimaye kufungua barabara hiyo.
Pamoja na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, wananchi hao pia walifunga
barabara ya...




