Jaji Mkuu Azindua Kitabu cha Sheria Chenye Maandiko ya Kesi Mbalimbali Pamoja na Jarida la Makala
Wanachuo Kipawa Sasa Kulipa Ada kwa M-Pesa

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo eneo la Kipawa kilipo chuo hicho Dar es Salaam, Mkuu wa Ukuzaji Biashara; M-Pesa Jackson Kiswaga amesema kuanza kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa azima ya Vodacom ya kuyaleta maisha ya watanzania kiganjani kupitia teknolojia ya simu za mkononi. Amesema katika mipango ya kuwezesha malipo ya ..
Mwandishi wa Redio Kwizera Issa Ngumba Ameuliwa Porini na Watu Wasiojulikana!!

Taarifa kutoka Kigoma zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa mwili wa mwanahabari huyo umekutwa nje kidogo na mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma RPC Kishai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa bado jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi .
Mbunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe pia amepata kuzungumza na mtandao huu na kudai kuwa ameguswa na kifo cha mtangazaji huyo na kutaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya kifo chake
Pia Kabwe ameeleza jinsi ambavyo mwanahabari huyo alivyoweza kuifanya kazi yake kwa jamii ya Kigoma kwa ufanisi zaidi na kuwa wakati mwingine yeye kama mbunge alikuwa akizunguka na mwanahabari huyo katika jimbo lake.
" Kweli nimeguswa sana na kifo cha kusikitisha cha mwanahabari huyo nilimfahamu vema kwa utendaji kazi wake ila nawapa pole sana waandishi wote nchini kwa msiba huu mkubwa .....na zaidi nitapata kueleza mengi mara baada ya uchunguzi"
Taarifa za awali zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Kakonko baada ya kupotea kwa mwanahabari huyo zilisema kuwa Bw Ngumba alipotea tangu January 05 mwaka huu majira ya saa 11 jioni ambapo alimuaga mke wake Bi. Rukia Yunus kuwa anakwendwa Muhange senta wilayani Kakonko na kwamba hajarudi nyumbani hadi sasa.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Muhange wanaendelea kumtafuta katika mapori ya kijiji hicho baada ya rafiki zake kueleza kuwa aliwaanga kuwa anakwenda kutafuta dawa msituni.

Aidha jeshi la polisi Wilayani Kibondo liliomba kampuni za mitandao ya simu anayotumia Bw Ngumba kusaidia kutambua simu zake zilipotumika kwa mara ya mwisho ili kurahisisha upatikanaji wake. Akizungumza kwa njia ya simu, Mke wa Bw Issa Ngumba, Bi Rukia Yunus amesema kuwa wananchi walio wengi ambao walikuwa wakimtafuta maporini wamerudi kijiji hapo baada ya kumkosa.
Maswali yaliyo jitokeza!!
1. Kawaida redio hiyo hutangaza taarifa/habari za aina gani?
2. Ngumba amekuwa akiandika habari/taarifa za aina gani?
3. Je, ni mwandishi mwololo au ana mtima wa nyundo?
... 4. Je, ni mtafiti/mchunguzi na mchambuzi (alikuwa na kipindi maalum redioni)?
5. Mahusiano yake na wenzake yalikuwa ya namna gani?
6. Mahusiano yake na wenye chombo yalikuwaje?
7. Mara ya mwisho aliandika habari zipi (zilihusu nini, nani na wapi)?
8. Anafahamika kwa kuandika nini kilichosisimua nywele za wengi?
9. Kazi yake iliyowahi kuibua mjadala miongoni mwa wenzake, mwajiri na wasomaji?
10. Alikuwa anapanga kufanya nini/kufuatilia nini (kile ambacho wenzake walifahamu)?
11. Alikuwa na uhusiano wowote na polisi (upi)?
12. Uhusiano wake na watawala wilayani ulikuwa wa aina gani?
13. Je, ni mwandishi aliyejua mambo mengi na ya ndani ya utawala wilayani?
14. Je, ni mwandishi aliyejua biashara za wazi na siri za "wakubwa?"
15. Mbali na kituo chake cha redio, alikuwa akipeleka wapi kazi zake (zipi)?
16. Uhusiano na mkewe ulikuwa wa aina gani (kwa mujibu wa watu wa karibu)?
17. Alikuwa na tabia gani (majivuno, ukarimu, wepesi/uzito wa kuelewa, ushabiki wa mambo (yapi); au alikuwa mpigania haki, mpenda kujielimisha na mtafutaji aliyetaka kuleta mabadiliko katika kazi/maisha/familia yake (vipi)?
18. Alikuwa na watoto (wangapi, wako wapi)?
Maswali haya nimempelekea pia mwandishi Kayanda aliyeko Kigoma. Ni muhimu tujue angalau haya machache.

Silaha 439 Zasalimishwa Kwa Hiari Polisi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ASP, Advera Senso, baadhi ya silaha zilizosalimishwa na idadi yake katika mabano ni pamoja na shortgun (29), gobore (352), SMG (11), riffle (20), bastola (22), airgun (1), rocket launcher (2) na SAR (2).
Kutokana na tatizo la kuzagaa na matumizi holela ya silaha zinazomilikiwa isivyo halali na kinyume cha sheria nchini, Desemba 4, mwaka jana, Waziri Nchimbi aliagiza kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja mtu yeyote ama kikundi chochote kinachomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha katika vituo vya polisi au ofisi yoyote ya serikali iliyo karibu nao.
Waziri Nchimbi aliagiza pia silaha hizo kusalimishwa kwa wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, vitongoji, wakuu wa wilaya, mikoa na madhehebu ya dini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zoezi hilo limefanyika kote nchini kuanzia ...

Mbunge wa Kenya Atinga Bungeni na Kiduku -Mohawk

Serikali ya Kongo na Waasi wa M23 Warejea Katika Mazungumzo Mjini Kampala

Serikali ya Kongo na waasi wa kundi la M23 wameendelea tena na mazungumzo ya kutaka kutatua mgogoro unaendelea Mashariki mwa Kongo.
Mazungumzo hayo yanayoendeshwa na waziri wa Ulinzi wa Uganda Dkt. Crispus Kiyonga yameanza hapo jana mjini Kampala nchini Uganda.
Nia kuu ya mazungumzo hayo ni kutafuta suluhisho kwa njia ya amani la mgogoro unaofukuta katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini.
Awamu ya kwanza ya mazungumzo baina ya serikali ya Kongo na waasi wa M23 ilianza Disemba 7 2012 lakini yakasitishwa mnamo Disemba 18 kwa ajili ya sikukuu ya Christimas.

Chadema: Umri wa Urais uwe Miaka 18

Subscribe to:
Posts (Atom)